Madhara yatokanayo na unywaji wa Red bull

asante,nita iprint niwape ndugu na jamaa zangu,nilikuwa natumia sana hii kitu,siku moja rafiki yangu akaniambia ukichanganya na pombe madhara yake huwa maradufu,hapo nikapunguza kabisa ,na hili la sasa itakuwa marukufu,ukizangatia sumu yenyewe inauzwa kwa sh,2500/-
 
Nimeshawishika baada ya kuambiwa ni "energy drink" ka kopo kamoja tu ka redbull kamenifanya nikose raha usiku kucha, mapigo ya moyo yamebadilika kama gari kwenye barabara ya kiwango cha vumbi! Vururuvuru kila idara sasa! Khaaa rebbull!
 
SOMA HAPA:

FYI


RED BULL NI HATARI



RED BULL Huuzwa katika maduka makubwa (Supermarkets) na madogo (Retail Shops) katika nchi ya Tanzania na watu wazima na watoto wetu wengi wana mazoea ya kunywa kinywaji hiki ambacho kinaweza kusababisha kifo! Kemikali zinazopatikana katika kinywaji cha RED BULL zilitengenezwa maalum katika maabara za kijeshi za Ma rekani kwa ajili ya kutuliza mzuka wa maaskari wao wakati wakitekeleza mauaji ya kikatili sana dhidi ya wananchi wa Vietnam miaka ya sitini na sabini. Kemikali hizo zilitumika pia kama dawa ya kuwazindua watu waliozirai (stress coma"). Hazikukusudiwa kutumiwa kama kinywaji au kilevi cha kawaida! Duniani kinywaji hiki (RED BULL) huuzwa kama kitu cha kuleta msismko (Energizer Drink) na matangazo yake yanataja sifa zake kama ifwatavyo.

"Ni kinywaji kinachompa mtu nguvu ya kustahimili na umakini. Humpa mtu kasi ya vitendo" ... na kadhalika.

RED BULL imesambaa katika nchi 100 kwa mpigo (nchi masikini!). Na matangazo yake kuwalenga vijana na watoto, hasa wanamichezo. Hawa ni rahisi kushabikia kinywaji hiki kibaya na kudhurika kiafya baadaye.

Katika hali yake ya matumizi ya sasa kinywaji hiki kiligunduliwa na Mjerumani Dietrich Mateschitz ambaye alikikuta huko Hong Kong kikiwa ni mojawapo ya madawa yaliyotumika katika kutengeneza dawa ya mswaki wa meno.Dawa hiyo ilitengenezwa kwa kemikali ambazo zina kafeni na taurini ("caffeine and "taurine). Mjerumani huyo aliona vijana wajinga wa huko wakishabikia unywaji wake akaona mwanya wa kufanya biashara na akafanikiwa kukileta ulaya.

ATHARI ZA KUNYWA RED BULL

Kinywaji kinachotengenezwa na kusambazwa leo hivi kina kemikali mbaya iitwayo "Glucuronolactone", kemikali hatari ambayo ilitengenezwa na idara ya jeshi la Marekani wakati wa vita na Vietnam kwa ajili ya kutuliza mvurugiko wa mwazo wa maaskari wake uliotokana na mauaji ya kinyama waliokuwa wanafanya huko Vietnam .

Kwa sababu ya madhara makubwa ya kinywaji hiki nchi za FRANCE na DENMARK zimepiga marufuku kinywaji hiki na kibatiza jina la "MKOROGO WA MAUTI".

Katika nchi hizi, utafiti uligundua kuwa maaskari wa Marekani waliotumia kinywaji chenye kemikali ya "GLUCURONOLACTONE" waliishia kupata madhara ya maumivu makali ya kichwa, uvimbe wa ubongo na hata ugonjwa wa ini (Migraines, Cerebral tumours and liver diseases). Ni kwa sababu hiyo wamarekani waliacha kuwapa maaskari wao hicho kinywaji katika miaka ya sitini na sabini.

Jambo la kushangaza ni kuwa lebo ya RED BULL inaonyesha wazi kuwa kinwaji hiki imetengenezwa kwa kemikali hatari ya "GLUCURONOLACTONE"!

Ni kwa sababu hiyo serikali za Denmark na Ufaransa nazo zikapiga marufuku unywaji wa RED BULL.

Pamoja na wauzaji wa RED BULL kuweka bayana kuwa ndani mwake mna hiyo kemikali hatari ya "GLUCURONOLACTONE" lebo ya RED BULL hailezi madhara makubwa yanayoletwa na kemikali hiyo. Madhara ambayo hayakuwekwa bayana kwa mnywaji ni kama yafuatayo:

1. Ni hatari kwa mtu ambaye hafanyi kazi au mazoezi mazito sana kukitumia kwani kina tabia ya kuongeza msukumo wa damu na kasi ya mapigo ya moyo kiasi kwamba mtumiaji anaweza kupatwa na ugonjwa wa moyo.

2. Mtumiaji anaweza kupatwa na ugonjwa wa damu kuvuja ubongoni kwani RED BULL ina kemikali zinazoifanya damu iwe nyembaba ili moyo upate kusukuma damu nyingi bila kutumia nguvu nyingi.

3. Ni hatari kuchanganya RED BULL na pombe ya aina yoyote kwani mchanganyiko wake huwa ni sumu ("Deadly Bomb") inayoathiri musuli za ini la mtumiaji na kuiacha katika hali ambayo haitapona kamwe.

4. RED BULL Ina vitamini B12 kwa wingi, vitamini ambayo hutumiwa kama dawa ya kuwazindua wagonjwa mahututi. Matumizi ya vitamini hii katika watu wazima ina athari za kuleta shinikizo la damu na humfanya mtu ajisikie kama mlevi.

5. Unywaji wa RED BULL mara kwa mara huvuruga mfumo ya neva za fahamu na husababisha maradhi mithili ya mfadhaiko wa akili usioponyeka.

HITIMISHO:


RED BULL ni kinywaji HATARI SANA ambacho hapana budi kipigwe marufuku katika nchi zote zinazoendelea kwani ni dhahiri kimetengenezwa na kusambazwa ili kiathiri afya za wananchi wasiojiweza wa nchi hizi masikini. Kwa kuwa wengi katika nchi hizi hutumia pombe za kila aina ni wazi kuwa kinywaji hiki kinalenga kuwamaliza watu wetu – kana kwamba ukimwi uliobuniwa na hao wabaya wetu hautoshi!

N I VYEMA TUKAWALINDA WATOTO NA VIJANA WETU LA SIVYO HATUNA WARITHI!

Tafsiri – EGM 2009
 
Ni kinywaji hatari. Pale Morogoro kuna kijana alikata roho mara baada ya kumaliza kikopo kimoja cha Redbull.
 
Heshima yenu wakuu. Kuna jirani yangu ameniletea carton nzima ya RedBull na kudai amepewa zawadi ya birthday. Nilipomuuliza kwa nini ananipa carton nzima amedai kaambiwa zina madhara na hivyo hatumii. Kabla sijafungua hili carton naombeni mnipe madhara ya kinywaji hiki.
 
Vinywaji vingi vya jamii hiyo siyo vizuri, sifahamu memngi ila najua preservatives siyo nzuri katika mwili wa binadamu
 
Huyo jirani hakupendi kama anajua vina madhara na yeye hatumii ameona wewe ndo wa kufa na hayo madhara??selfish neighbour indeed....

Kuhusu madhara nishasikia mara kibao. tusubiri wataalam waje watueleze kiundani
 
Y akupe wkt vnamadhara,nawew kwnin upokee kama amekuwarn madhara!?
 
Hiyo ni energy drink, kikawaida inabidi mtu anakunywa moja tu inatosha sa unakuta sistaduu anakunywa redbull 6 mmmh!
 
Hiyo ni energy drink, kikawaida inabidi mtu anakunywa moja tu inatosha sa unakuta sistaduu anakunywa redbull 6 mmmh!

Nasikia kuna dada mmoja amewahi kunywa 3 akazimia...
 
Angalia Expire date uskurupuke kunywa kwanza,then,kama haijaexpire unaweza ukaweka hata 3 za kunywa na wwe kawape wengne,sasa kantoni nzima unataka ugonge peke yako!TOO MUCH OF STH IS HARMEUL
 
Redbull ni kinywaji kilitengenezwa maalumu kutumika na wanajeshi tena wakati wa vita tu. Lengo ni kuwaondolea woga na depression. Zina kiwango kikubwa sana cha caffein. Kwa ujumla ni kinywaji usichopaswa kunywa kabisa.
 
madhara yaletwayo na caffeine
moyo kwenda mbio
high blood pressure
kukosa usingizi...etc
 
haswa zina madhala tafuta thread ya trh 28sept 2011 au google na andika 'Madhala ya redbull jamiiforum' nimeshindwa weka link coz natumia mobile muda huu,u will see the aim and sideeffect of redbull
 
mimi hizi nakunywa... mara nyingi huwa zinakimbilia kulegeza joint hasa za miguuni..na ukinywa nyingi zinaua kabisa nguvu za kiume...unaweza ukaenda raundi moja kwa shida sana lakini ukimaliza hurudii tena....ushauri unywe wakati umechoka unahitaji nguvu mpya itakusaidia.!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…