Madhila ya Force Account: Mwalimu afungwa kwa kula pesa ya ujenzi

Tatizo ni mfumo mbovu wa nchi
 
Madarasa mangapi yamejengwa kwa Force Account?Madarasa mengi yamejengwa kwa force account.Kwa hiyo faida ni kubwa kuliko madhara.
 
Kabla ya fedha kutolewa lazima Eng apitishe certificate, pia DEO na DED lazima asaini hiyo cheque ndiyo waende bank, How Mwl anaweza kuiba peke ake?
 
Ilipaswa pia tujiulize kabla ya force account pesa ilikua haiibiwi? Wizi upo kwenye DNA ya watanzania. Kwa maana hata miradi ambayo haitumii force account bado watu wanapiga tu
Hata kama zilikuwa zinaibiwa lakini sasa AMERAHISISHIWA HUYO MWIZI kwa kiwango cha kutisha!! Ni sawa na mtu kulala bila kufunga mlango halafu akaibiwa!! Huwezi kusema kwani wanaofunga milango huwa hawaibiwi? Haiwezekani mtu aamue kutokufunga mlango usiku kwa kisingizio kuwa hata hao wanaofunga milango hutokea wakaibiwa pia!!
 
Tatizo ni bodi ya uhasibu, kisheria kuna kiwango fulani cha pesa kikifika lazima kisimamiwe na mhasibu.
Bahati mbaya wanasheria wengi hawaelewi juu ya hii sheria kwa sababu inambana hata anayevunja sheria.
Kumkabidhi mwalimu kusimamia mamilioni ya pesa ni kosa kisheria.
 
Force account ni janga
NI Mambo ya kuchanganya,miaka Ile ya awamu "force works" kazi ujenzi zilifanywa na watendaji wa serikali waliosomea fani hizo.kazi inaprogramiwa na afisa mpango,fed anaidhinisha,mhandisi.na watu wake wanatekeleza.mweka hazina analipa.leo hii mwenyeki ambaye hajawahi hata kujenga Banda la mbuzi anasimamia ujenzi wa shule/mradii wa 2.0 bilionI.huyo mwalimu waliompa hiyo kazi ndio wanapaswa kufungwa.
 
Lakini kuna kamati, pia msimamizi mkuu wa ujenzi ni Eng
 
Ninyi inaelekea hamjakaa ofisi za serklai au shirika la umma.
Huyo mwalimu is a stupid fall guy.
Hizo hela hakula peke yake na si ajabu ndiye aliyehusika kuzipokea toka benki.
Hapo kala na watendaji wa serikali na hata madiwani wake.
Kesi imepelekwa MAHAKAMANI na amekutwa na hatia kula fedha za serikali kwa niaba ya vifisadi uchwara kijijini.

Tatizo lenu ni kfikiri hela ya serikali mpaka wote waliokula wapatikane, hapana , wajanja wamemwangushia jumba bovu huyo mwalimu.
 
Pesa zingine huwa sio za kuiba, ukiiba kidogo utafungwa zaidi.
 
Sh ngapi kala
 
Yaani naweza ku imagine.

Huyu hapa mwalimu kijijini, choka mbaya, mshahara wenyewe unafika kwa kuchelewa sana huko kijijini.
Mara anaambiwa shule yake imekumbukwa, mamilioni hayo hapo, jenga darasa la watoto 35 na utaongezewa pesa kujenga darasa lingine la pili.

Wajanja toka wilayani, halmashauri wote wako kijijini "kumpa mawazo na kukagua" mradi kila wiki.
Wanadai posho, hela ipo, wanamwambia mwalimu akileta kauzibe atahamishwa.

Mwalimu anakumbuka kale kamshahara wala hakamalizi mwezi.
Mwalimu hana linginne, anagawaposho, naye anajigawia nakamati yake na hao wasimamizi toka wilayani na Halmahauri.

Mara anaingia mkaguzi-Auditor...............mwalimu suruali inaaguka chini!!!
 
Nilichotaka ujue ni kwamba hela ya serikali huwa hailiwi na mtu mmoja, kwakua umeshaelewa sina jingine.
 
Nilichotaka ujue ni kwamba hela ya serikali huwa hailiwi na mtu mmoja, kwakua umeshaelewa sina jingine.
Nafikiri umeelewa maana ya fall-guy.
Na ndiyo maan mahakama imemkuta na hatia mtu mmoja na kumfunga.
Wajanja wamesepa.
 
Siyo mimi nimemfunga, nimeonyesha jinsi maamuzi mabaya yasiyofikiria sera za manunuzi kwa fedha za umma na madhara yake.
Wanafungwa watu kwa kupewa fedha wasizojua kuzitumia kama ipasavyo kwa kazi za serikali.
Fedha za umma wanazitafuna balaa...watoa huduma za kandarasi wakishilikiana na wafanyakazi wa umma wasio waaminifu. CAG mara kadhaa anawadai hata wakandarasi ambao hawatumii forced account warudishe fedha sababu hawakufanya kazi stahiki.
Watanzania tunaiba sana
 
Upo sahihi kabisa hapo wahusika ni wengi sn mpk DED
Mleta mada haelewi kitu kuhusu madili ya pesa z serikali ndomaana anampoint mwalimu kama mnufaika pekee huku akihusisha wizi huo na zaifu wa force account, kana kwamba huko nyuma hakukuwah kuwa na wizi au labda hiyo force account ina signatory mmoja kitu ambacho sio.

Mkuu wa shule kaingizwa kingi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…