Madiwani 11 wa CHADEMA wakiongozwa na Meya wa Jiji la Mbeya wahamia CCM

Madiwani 11 wa CHADEMA wakiongozwa na Meya wa Jiji la Mbeya wahamia CCM

View attachment 1367934

Hey guys try this 👆 registration is total free. You earn everytime you invite someone who joins for free too. Someone from Nigeria invited me, apparently its only 9 days old in Nigeria, and making waves. I said why not since I'm only putting my email address up there, no money required.

Let's give it a try
Nigerians again!
For those who wants free money, downloadable money,
I wish you good luck.
 
Suala la kuhama vyama wanachama wa kawaida au viongozi wachcahe au wastaafu ni kawaida sana sikatai.
Kuhama wanachama wengi ndani ya muda mfupi sio kawaida ni tatizo.
Kuhama viongozi wahandamizi wengi ndani ya uda mfupi ni tatizo zaidi.
Kuhama viongozi wa ngazi za juu kabisa wawe wastaafu au waliopo madarakani ni tatizo kubwa sana sana.
Kuhama viongozi wawakili wa wananchi kwenye majimbo au kata ni tatizzo kubwa mbele ya walio wapa nafasi ya kuwawakilisha na kuwasemea kupitia chama walichokiamini ajenda au itikadi zake.
Watu tunajisahu au tuna Umri mdogo kukumbuka mambo na kutojua HISTORIA,
Chama cha kwanza chenye nguvu baada ya kuundwa mfumo wa vyama vingi kilikuwa UMD chini ya kina FUNDIKILA na KASANGA TUMBO. Pia walikuwepo NCCR, TLP, CUF na leo CDM ambayo zamu yake ya kufa imefika.
Kama wapinzani hawatijifunza chanzo cha haya kila siku watatudanganya kwa visababu vyepesi vya uongo.
Hebu waunde tume na wakawahoji wale waliohama zamani waeleze ukweli kwa nini walihama
LISSU LEMA, MSIGWA, ZITTO, PROF. SAFARI hata MAALIM watuambie masaibu yaliyowapata mpaka wakachukua uamuzi wa kuhama vyama vyao vya awali
 
Watu tunajisahu au tuna Umri mdogo kukumbuka mambo na kutojua HISTORIA,
Chama cha kwanza chenye nguvu baada ya kuundwa mfumo wa vyama vingi kilikuwa UMD chini ya kina FUNDIKILA na KASANGA TUMBO. Pia walikuwepo NCCR, TLP, CUF na leo CDM ambayo zamu yake ya kufa imefika.
Kama wapinzani hawatijifunza chanzo cha haya kila siku watatudanganya kwa visababu vyepesi vya uongo.
Hebu waunde tume na wakawahoji wale waliohama zamani waeleze ukweli kwa nini walihama
LISSU LEMA, MSIGWA, ZITTO, PROF. SAFARI hata MAALIM watuambie masaibu yaliyowapata mpaka wakachukua uamuzi wa kuhama vyama vyao vya awali
TUPO SAMBAMBA HADI HAPA.
Tusikubali majibu rahisi kwa hoja au maswali mazito.

Kuhama ni kawaida lakni tunaona kunapokuwa na wimbi kama hili la sasa basi chama kinacho hamwa kama sio chama tawala basi kinajikuta kinenda ukingoni.
Vyama karibu vyote ulivyotaja walijitetea na kujiamini kama sasa wanavyofanya CDM.

Tuombe awamu hii CDM asifuate anguko kama la watangulizi wake.
Sababu ikitokea hivyo nahisi CCM itakuwa na kiburi na kutawala karne moja au zaidi.
 
Fungua akili, macho na masikio. Usilishwe maneno
Suala la wanasiasa kuhama ni pana lakini linaelezeka.
Utapata jibu sahihi kama utajua;
Kwa nini Godbless Lena alihama TLP akaenda CDM
Kwa nini Msigwa alihamia CDM kutoka TLP
Kwa nini LISSU alitoka NCCR kwenda CDM
Kwa nini Hamad Rashid alitoka Cuf akaunda ADC
Kwa nini Zito, Kitila, Migamba, Mwampamba na wenzao walitoka CDM wakaunda ACT
Kwa nini Maalim Seif alikimbia CUF akajisajili ACT
Kwa nini Lowasa alitoka CCM akaenda kuinunua CDM, achilia mbali wale walihamia C M kama Kutoka upinzani kama Mwampamba, Mwigamba, Mashinji, Aman Kabourou, Dr. Slaa, Said Arfi
Kwanini kuna wanasiasa waliokata tamaa na wakaamua kustaafu kama kina PROF. SAFARI!?



Anyway, mifano ni mingi inayoonyesha sababu na mazingira tofauti yanayopelekea wanasiasa kuhama.
Ya mwisho kabisa ni kununua.
Je hao uliwataja hapo juu nao mliwaita wananunuliwa kama mnavyowatuhumu hawa wanaohama sasa hivi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkakati wa kuisambaratisha Chadema kwa gharama yeyote ile unaendelea.
Sidhani kama watafanikiwa. Wanachoshindwa kutambua ni kwamba hao wanaohama hawataipigia kura ccm. Watajisikiaje wakijua ni mpango ndani ya Chama Chadema watu wachukue pesa waseme wamehama hahahhh nacheka kwa kidhungu!

Bushiru hajajifunza huko Lindi aendelee kujidanganya.
Watu wanachukua elfu kumi kumi wanaendelea na maisha
Akili nyingi kila mtu ana zake!
 
Hata hiki kinachofanyika ni SIASA pia.

Senti bai yuzingi tecno T301
Kama ni siasa tuseme ni siasa za kipuuzi. Huwezi kutegemea chama kama Ccm kufanya siasa za majitaka kama hizi. Kujipitisha serikali za mitaa bila kupingwa, kununua wabunge/madiwani wa upinzani na kuwapitisha kibabe kwenye chaguzi za marudio, halafu baada ya hapo wana kwenda kuaacha solemba. Hii ni kuua talent ya mtu na pia kuharibu future yake bila kusahau familia itakwenda kusota for life.
Hizi sio siasa Ccm wana takiwa kufanya halafu ati mwenyekiti ni Dr, katibu mkuu ni Dr.... Etc SHAME!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu uongozi wa juu wa CDM unahusika sehemu moja tu, kushindwa kuzuia hii hali isiendelee.
Wawe wabunifu kutafuta suluhisho la tatizo lililopo mbele yao ndio maana ya uongozi.

Matumaini ya wanachama wao wa kawaida yapo kwao, haitoshi kulalamika wananunuliwa huku haufanyi kitu kukabiliana nao zaidi ya kulalamika kama wanasubiri hisani ya viongozi wa chama shindani kukomesha hili tatizo.

Kazi ya uongozi ni kutafuta majibu, ni kama wnavyotaka Raisi awajibike kwa makosa ya watendaji wake ngazi ya wilaya au kata.
Chadema imefanya kila lililo lake , haiwezi kuwalazimisha walioamua kuiabudu pesa badala ya utu wao na heshima waliyopewa na chama na wananchi
 
Hoja ya kuhama hama bila kuiweka mezani baada ya uchaguzi huu hakutakua na chadema,ni swala la muda tu
 
Itabidi nikubali tu hoja yako ingawa mmh!
hatuwezi kuwaweka mahabusu hawa wasaliti , hatuna uwezo huo , kumbuka hawa ni watu tuliowatoa miongoni mwa hao hao raia wengine , na nakuhakikishia kwamba Chadema itawaleta tena raia wengine waaminifu na watashinda nafasi hizo hizo

Laana ya usaliti ni mbaya sana
 
Katibu Mkuu wa CCM, Bashiru Ally amesema kati ya Madiwani hao, 10 ni Madiwani wa Kuchaguliwa na Mmoja ni wa Viti Maalumu huku timu hiyo inayoongozwa na Meya ikiwa na Viongozi Watatu wa Juu wa CHADEMA.

Amesema kuwa Madiwani hao wanatoka katika Jiji la Mbeya kwenye Halmashauri inayoongozwa na CHADEMA na Mbunge wa Jimbo hilo ni Joseph Mbilinyi (Sugu) na kuwa huo ni ugeni mkubwa tangu aanze kupokea Wageni.

Aidha, amesema ameongea na Madiwani hao na kumueleza kwanini wanafanya uamuzi huo wakati huo na amefurahi sana maana kazi yake ni kuifanya CCM kutoa ushawishi na kupata wafuasi kila kona ya Nchi.
Kuna jisongi moja Zembwela aka Ndimu alikua anakapenda sana kanamaneno haya KAMSAKATA KATUMBAKU hahaaaa wa mama J Bby.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chadema imefanya kila lililo lake , haiwezi kuwalazimisha walioamua kuiabudu pesa badala ya utu wao na heshima waliyopewa na chama na wananchi
kamanda Kyela Mwakyembe anapita bila kupingwa, msipotubu laana ya Dr.Slaa itawapiga vibaya
 
Back
Top Bottom