Baraza jipya la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru lipo Mkoani Katavi kwa siku tano kujifunza kuhusu hewa ukaa.
Madiwani wote zaidi ya 60 na wakuu wa idara watakuwa nje ya halmashauri kwa zaidi ya wiki moja kwaajili ya safari hiyo.
Tsh Milioni 1.8 italipwa kwa kila diwani katika safari hiyo huku wakuu wa idara wakipata chini ya hapo kiasi kinachokadiriwa kutopungua Milioni 1
Kwa ujumla wake safari hiyo inakadiriwa kugharimu kiasi cha fedha kisichopungua Milioni 115.
SAFARI HII INATUACHA NA MASWALI MENGI BILA MAJIBU NA MASHAKA BILA MATUMAINI.
Kwanini Safari hii ihusishe Madiwani ambao tunajua ni kama wameenda kutalii na sio wataalamu wa jambo hili la hewa ukaa ili wakirudi waje kutoa elimu kwa wananchi?
Kwanini safari hii katika kipindi hiki kigumu cha ongezeko la gharama za usafiri kwa kupanda bei ya mafuta tukizingatia kuwa hata Mh Rais ameamua kuanza kupunguza misafara yake?
Kwanini fedha hizo nyingi zisielekezwe kwenye miradi iliyokwama kwa muda sasa kutokana na uhaba wa fedha ( Mfano: kukamilisha ujenzi wa Madarasa shule ya Msingi Mea Mtwaro ambayo ujenzi wake umekwama tangu mwaka jana) na badala yake wanaenda kula madiwani tukiwa tunajua hakuna tija yoyote itapatikana?
Kwanini Wabunge walipwe fedha hizo kama sehemu ya Msafara wakati tunajua wazi kuwa wapo bungeni na hawajashiriki safari hiyo?
MADIWANI MADIWANI mnatufikiriaje wananchi wa Wilaya ya Tunduru na Watanzania?
Hivi ni kweli kipaumbele chetu ni ziara za masomo ambazo hazina tija?
Je ni vijana wangapi wapo mtaani hawa ajira wala mitaji ambao wangeweza kupewa hizo fursa za mafunzo, ujuzi ambao wangeupata ungesaidia katika kuunda vikundi vidogo vidogo na kuanzisha miradi ya hewa ukaa?
Je ni shule ngapi hazina vyoo, vyumba vya madarasa, madawati, motisha kwa walimu ambapo pesa hizo zingeweza saidia kutatua baadhi ya changamoto?
ADDO SHAIBU NA ENGINEER CHILOMBE wabunge wetu, je munabairiki mambo kama haya kufanyika katika halmashauri yenu?
Ombi kwa serikali, kama ambavyo safari imewezeshwa basi tunaomba mrejesho baada ya mafunzo nifaida ipi itazalishwa kupitia Madiwani ili kufidia matumizi ya pesa hii
Inchimaga nkafyechele