Takribani madiwani 20 wa chadema waliojiunga ccm kuunga juhudi za Rais Magufuli wameangukia pua kwenye kura za maoni huku eti wakidai wamehujumiwa na wajumbe.
Hatua hiyo imedhihirisha wazi kwamba wenye ccm yao wapo na sio wahamiaji kama walivyopigwa mweleka kwenye kura za maoni na wengi wao wakiambulia kura moja na sifuri.
Wajumbe wako sahihi .
Hawawezi kumpa kura mtu aliyewatukana na kikitukana Chama chao kwa miaka nenda rudi eti Leo wamerudi kwa sababu ya Rushwa ya fedha na madaraka ndio wapewe kura.
Wajumbe wamewatumbua majipu yanayopenda Rushwa ya madaraka.
Wamerudi CCM na kuacha Ubunge kwa ahadi ya kupewa majimbo au uteuzi.
Hii ni Rushwa ya ahadi ya madaraka.
Waliotoka upinzani kwa ahadi ya uteuzi hawafai kamwe mana ni wapenda Rushwa.
Mtu msafi kabisa anaweza kukaa ndani ya Chama bila Madaraka.
Kuhama Chama au kujiunga na Chama kwa sababu ya ahadi ya madaraka ni Rushwa.
Watanzania wote tuwaunge mkono wajumbe wa CCM kwa kukomesha vitendo vya Rushwa ya fedha na madaraka.
Hili suala la Rushwa ya madaraka limeharibu sio tu vyama kama taasisi Bali hata taasisi za umma zimekosa watu wenye maadili na kujikuta watu wanakiuka katina na sheria za utumishi wa umma kwa sababu ya kukimbila uteuzi na kuahidiwa kupitishwa kwa kupewa ushindi wa mezani.
Hii ikiacha italeta utendaji uliogubikwa na ubinafsi wa mtu kujipendekeza kwa malengo ya kupata uteuzi bila kufuata sheria.
Mtu anaajiriwa kama Mhandishi badala ya kufanya kazi yake ya uhandishi yeye anafanya kazi za Chama cha siasa wakati kila Chama kina watendaji wake wanaolipwa kwa kazi hiyo.
Naipongeza sana serikali kwa kuamua kukaa mbali na hao watu wanaojipendekeza kwa Rushwa ya madaraka na fedha. Huu ni ubinafsi bora wakatwe wakae pembeni ili watafutwe watu waliopigania Chama katika shida na raha. Sio waone Chama kinafanya vizuri ndio wanajiuza kwa kutamani uteuzi ambao ni kwa ajili ya wenye Chama na sio wavamizi ambao hawako tayari kukaa bila madaraka.
Kwao Umuhimu wa CCM sio Sera wala itikadi Bali ni madaraka na uteuzi