Kwa siasa za miaka hii, kuna wapinzani wataondoka kuunga juhudi si kwa mapenzi yao Bali ni hofu ya kuogopa kesi zisiziosha, kufilisiwa kiuchumi, na Hata usalama wao. Takwimu zinaonyesha wapinzani wengi ndo wamepoteza maishaa ama kupotea hasa ktk vipindi vya uchaguzi kuliko wa chama tawala.
Kodi zetu zinatumika ******* sana. Chakubanga anajimegea tu mabilioni kununua hiyo mifugo.
Hahahaa nililitegemea sana hili
Viva Magufuri
Ipo siku hawa watalia wakigara gara chini wakiomba kurudi upinzani, na hio siku haiko mbali! maskini roho zao!Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Dk Maulid Madeni amesema amepokea barua za kujiuzulu za madiwani watano wa Chadema Jiji la Arusha.
Mbali na barua hizo za kujiuzulu, madiwani hao pia wamemuandikia barua katibu wa CCM Wilaya ya Arusha wakiomba kujiunga na chama hicho tawala nchini Tanzania.
Kutokana na kujiuzulu kwa madiwani hao, Jiji hilo sasa lina madiwani 28 ambapo 20 ni wa Chadema na CCM wanane.
Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, CCM ilipata diwani mmoja lakini hivi karibuni madiwani saba wa Chadema walijiuzulu na kujiunga na chama hicho tawala.
Akizungumza na Mwananchi leo Jumamosi Novemba 30, 2019, Dk Madeni amesema Jiji tayari limeanzia mchakato wa kuzifikisha barua hizo katika ngazi nyingine.
"Ni kweli madiwani hawa wamejiuzulu na barua ninazo,” amesema.
Madiwani waliojiuzulu ni George Nditika (Baraa), Veronica Hosea, Glory Kaaya, na Jeni Severe (wote Viti Maalum) na Godfrey Soilel (Simon).
Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema alipoulizwa kuhusu madiwani hao amesema alikuwa na taarifa zao kuwa watajiuzulu.
Novemba 19, 2019, meya wa Chadema Jiji la Arusha, Kalist Lazaro alijiuzulu na kuhamia CCM.
Mwandishi ameona mpaka aibu kusema wa viti maalum.
Makapi na viongozi njaa,unajua kabisa hailipi na haina maana kabisa,ukaishia madiwani watano.
CCM MMEKWAMA SANA. Na huo mchezo wakutapanya kodi zetu kwa sifa za kijinga utawatokea puani siku moja.
Mtayajutia haya matumizi mabaya ya pesa za UMMA. Muda utaamua
Chadema ipo kwenye mioyo ya watu na si madiwani ,hata wakiondoka wote ,kama uchafuzi ukafanyika kwa uhuru na haki cjadema inaweza kuweka sura mpya na kushinda kwa kishindoKichaka kinazidi kuungua ,chadema nawaonea huruma
Wamejitambua hao madiwaniDomokrasia+njaa
Ova
Madiwani siyo watu?Chadema ipo kwenye mioyo ya watu na si madiwani ,hata wakiondoka wote ,kama uchafuzi ukafanyika kwa uhuru na haki cjadema inaweza kuweka sura mpya na kushinda kwa kishindo