Madiwani watano wa CHADEMA jiji la Arusha wajivua madaraka

Madiwani watano wa CHADEMA jiji la Arusha wajivua madaraka

Hao ni makahaba wa kisiasa waache waende kwa mabwana zao wengine
 
Sasa viti maalumu kama nao sio vituko ni nini? Haina hata ladha
Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Dk Maulid Madeni amesema amepokea barua za kujiuzulu za madiwani watano wa Chadema Jiji la Arusha. Mbali na barua hizo za kujiuzulu, madiwani hao pia wamemuandikia barua katibu wa CCM Wilaya ya Arusha wakiomba kujiunga na chama hicho tawala nchini Tanzania.

Kutokana na kujiuzulu kwa madiwani hao, Jiji hilo sasa lina madiwani 28 ambapo 20 ni wa Chadema na CCM wanane. Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, CCM ilipata diwani mmoja lakini hivi karibuni madiwani saba wa Chadema walijiuzulu na kujiunga na chama hicho tawala. Akizungumza na Mwananchi leo Jumamosi Novemba 30, 2019, Dk Madeni amesema Jiji tayari limeanzia mchakato wa kuzifikisha barua hizo katika ngazi nyingine.

"Ni kweli madiwani hawa wamejiuzulu na barua ninazo,” amesema. Madiwani waliojiuzulu ni George Nditika (Baraa), Veronica Hosea, Glory Kaaya, na Jeni Severe (wote Viti Maalum) na Godfrey Soilel (Simon). Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema alipoulizwa kuhusu madiwani hao amesema alikuwa na taarifa zao kuwa watajiuzulu. Novemba 19, 2019, meya wa Chadema Jiji la Arusha, Kalist Lazaro alijiuzulu na kuhamia CCM
 
Hao viongozi waende hata wote huko ccm na hakuna mtu anaweza kuwazuia watu kwenda kutafuta maisha, lakini wananchi msimamo wetu uko imara, hatuikubali ccm na ushahidi hata kwenye uchaguzi hatukujiandikisha kupiga kura.
Tatizo ni ccm kudhani matatizo na upinzani dhidi yao uko katika vyama!!!
Wanajisahaulisha kwamba wameshachokwa na wananchi...
#Katiba mpya... #tume huru ya uchaguzi
 
Back
Top Bottom