Madiwani watano wa CHADEMA jiji la Arusha wajivua madaraka

Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Dk Maulid Madeni amesema amepokea barua za madiwani watano wa CHADEMA kujiuzulu katika jiji la Arusha

====

Sasa kama wameahidiwa kulipwa kiinua mgongo na kuakikishiwa kurudishwa bila kupingwa wao wafanyeje?

Wametumia haki yao. Tusubiri wabunge watakaojisalimisha pia.
 
Hao ni wale wa VITI MAALUMU, wamejua uchaguzi ujao hawatapata maana CCM inachukua kwa nguvu so wameamua kuchukua fedha za kununuliwa kwao mapema, wakijumlisha na pensheni zao watakuwa wamelamba dume, hasara ni kwa CCM.
Pension hawapati maana hawakumaliza muda wao! Na huko waendako hawana chao!
 
haiya sasa CHADEMA muanze kujiandaa kisaikolojia mapema
maana mwakani mtakua na wakati mgumu sana
 
Naanza kuelewa hii mbinu. Yaweza kuwa na matokeo mazuri, ngoja tuone
 
Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Dk Maulid Madeni amesema amepokea barua za madiwani watano wa CHADEMA kujiuzulu katika jiji la Arusha

====
Clip inayosambaa ya Kibajaji inayomuongelea Mwenyekiti Mbowe imekuwa ni mwiba, si kwa Mbowe tu, bali ni kwa Chadema nzima.

Maana amewafungua macho raia, viongozi na wanachama. Cdm kisipojitathimini kitabaki ni chama cha familia.
 
Mtu anayeweza kupoteza muda wake kumsikiliza Kibajaji na kuchukulia maneno yake kama reference ni mpumba.vu. Naamini wewe si mojawapo.
 
Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Dk Maulid Madeni amesema amepokea barua za kujiuzulu za madiwani watano wa Chadema Jiji la Arusha. Mbali na barua hizo za kujiuzulu, madiwani hao pia wamemuandikia barua katibu wa CCM Wilaya ya Arusha wakiomba kujiunga na chama hicho tawala nchini Tanzania.

Kutokana na kujiuzulu kwa madiwani hao, Jiji hilo sasa lina madiwani 28 ambapo 20 ni wa Chadema na CCM wanane. Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, CCM ilipata diwani mmoja lakini hivi karibuni madiwani saba wa Chadema walijiuzulu na kujiunga na chama hicho tawala. Akizungumza na Mwananchi leo Jumamosi Novemba 30, 2019, Dk Madeni amesema Jiji tayari limeanzia mchakato wa kuzifikisha barua hizo katika ngazi nyingine.

"Ni kweli madiwani hawa wamejiuzulu na barua ninazo,” amesema. Madiwani waliojiuzulu ni George Nditika (Baraa), Veronica Hosea, Glory Kaaya, na Jeni Severe (wote Viti Maalum) na Godfrey Soilel (Simon). Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema alipoulizwa kuhusu madiwani hao amesema alikuwa na taarifa zao kuwa watajiuzulu. Novemba 19, 2019, meya wa Chadema Jiji la Arusha, Kalist Lazaro alijiuzulu na kuhamia CCM
 
Mtu anayeweza kupoteza muda wake kumsikiliza Kibajaji na kuchukulia maneno yake kama reference ni mpumba.vu. Naamini wewe si mojawapo.
Mkuu kwenye kubadilishana mawazo kuna matusi tena?

Basi endelea kutukana hadi uridhike.
Tukana sana, una ngao ya keyboard hakuna wa kukugusa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…