Madudu ukaguzi maalum wa CAG upande wa REA 2015-2020

Walinda Legasi ngoja kama nawaona hv [emoji12][emoji12][emoji12]
 
Hachafuliwi weee [emoji1][emoji23][emoji23] acha uoga
 
Inasikitisha sana... Mambo ya serikali ndivyo yalivyo...
 
Sasa kwa nini kwenye makadirio wa quote tuu za 100kVa wakati walijua na ndogo zitahitajika.
 
Habithi laamal wewe, paper on table currently is 2021/2022
 
Usijifanye mjuaji wakati umeandika pumba tu. Kama usemavyo ni kweli kwanini wapange bajeti ya transform za 100kv kisha wanunue za 50kv? Huoni hoja ya mleta mada hapo au umejitoa ufahamu kwa mapenzi yako kwa legacy?
 
Umewahi kufanya kazi ya kuandaa specifications za mradi wowote?? Acha kubisha vitu usivyovijua. Anayeandaa hizo specs hata mahali hizo transfoma zitafungwa hapajui, kwa kifupi ni makadirio matupu ili upate figures ya kuweka kwenye bajeti.
 
BTW ni 'kVA' sio 'kv' 🤣
 
Usitetee ufisadi hapa. Kama fedha zilizotolewa ni za 100kv, badala yake zikanunuliwa za 50kv bila kuonesha salio, huo ni Ufisadi. Sijui unabisha nini hapa.
 
Usitetee ufisadi hapa. Kama fedha zilizotolewa ni za 100kv, badala yake zikanunuliwa za 50kv bila kuonesha salio, huo ni Ufisadi. Sijui unabisha nini hapa.
Unajua hizo za 50 kVA zilinunuliwa ngapi badala ya zile za 100 kVA??
 
Sasa tukuamini wewe au tumwamini CAG aliyeenda field kufanya ukaguzi?
Huyo ni mbishi tuu hana lolote eti anasema "yalikuwa ni makadirio matupu ili upate figures ya (za) kuweka kwenye budget".What a contradiction.
 
Tukianzia hapo tufanye na 2015-2010 ili tumkamate yule mwizi na genge lake.
 
Kwenye wizara hiyo wakati wa Kalemani kulikuwa na ufisadi wa hali ya juu. Kuna watu walipelekewa umeme, mtu mmoja, umbali wa zaidi ya kilometer 20 kwa gharama ya REA, lakini unapelekwa kwenye kabiashara kwa ndugu yake Kalemani. Kabiashara kenyewe, uwekezaji wake haufiki hata shilingi milioni 500.

Waziri alikuwa anacheza na media ili aonekane anafanya kazi sana wakati kwenye uhalisia ilikuwa tofauti. Umeme unapelekwa kwenye kijiji fulani, zinaunganishwa nyumba 2 au 4, waziri anaenda hapo na wanahabari kibao kutangaza tukio la kuwasha umeme kijiji fulani, lakini nyumba zilizounganishwa ni 2 au 4. Halafu timu ya ujenzi inahamia kijiji kingine. Kuna vijiji vingine mpaka leo, licha ya umeme kufika kijijini kwao karibia miaka 5 iliyopita, waliounganishiwa umeme, hawafiki hata 5% japo wameomba muda mrefu.

Kati ya Wizara ambazo efficiency ni very poor, Wizara ya Nishati ni miongoni. Mpaka sasa, hii Wizara haijapata unafuu wowote. Na kati ya mashirika ya hovyo kabisa galiyojaza watu ambao hawafanyi kazi, TANESCO, nadhani ni shirika la kwanza. Muda mwingi wamejazana ofisini, na kubakia wanazungukazunguka lakini hakuna cha maana wanachokifanya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…