Madudu ukaguzi maalum wa CAG upande wa REA 2015-2020

Madudu ukaguzi maalum wa CAG upande wa REA 2015-2020

Sasa tukuamini wewe au tumwamini CAG aliyeenda field kufanya ukaguzi?
CAG hajasema pesa imeliwa, amesema transfoma zilizonunuliwa haziendani na specifications. Na ndio maana nikasema angekuwa na watu makini wangejua kwanini vijijini zinafungwa transoma za 50 kVA zaidi. Yes, ni kasoro ya kiukaguzi ambayo inaelezeka kirahisi kabisa.

Plus, Kichele haendi site, ni hao vijana wengine wameajiriwa juzi tu hapo, kuja mambo mengi hawayajui na hawana utaalamu nayo. Ripoti ya CAG sio msahafu, na ndio maana kamati za bunge huwa zinapitia hoja zote upya na kuomba ufafanuzi kutoka kwa wahusika. Kuna hoja nyingi tu za CAG huwa zinatupikiwa mbali.
 
UKAGUZI wa Ufanisi wa Mamlaka ya Nishati Vijijini (REA) uliofanywa na CAG umeimulika REA kuanzia mwaka 2015/2016 mpaka 2019/2020.

Ukaguzi umefanyika kwa maombi ya wafadhili; Shirika la Kimataifa la Maendeleo Sweden (Sida).

Kwamba Machi 2016, Tanzania na Sida waliingia mkataba wa ufadhili wa kutandaza umeme vijijini. Fedha zilitoka SEK 600 milioni (Sh133 bilioni).

Uzembe wa kuchelewa kupakua malighafi Bandari ya Dar, ulisababisha REA watumie Sh775.76 milioni kulipa tozo ya uchelewaji (demurrage charge). Fedha za ufadhili zikatumika ndivyo sivyo kwa uzembe.

CAG amebaini kuwa transfoma zilizofungwa uwezo wake ni 50KV, wakati bajeti ilikuwa 100KV. Fedha za wafadhili zilipigwa cha juu.

Upembuzi yakinifu haukufanyika. Hata udongo haukupimwa. Nguzo zimewekwa pasipo vipimo. Pesa ya upembuzi yakinifu (feasibility study), imepigwa.

Wateja 51,425 tu kati ya 98,689 walioomba kuunganishiwa umeme, ndio wameungabishiwa. Hiyo ni sawa na asilimia 52.1.

CAG ameandika; nyaraka za Sida zinaonesha REA walitakiwa kusambaza umeme kwenye nyumba 86,000, hivyo kuhudumia watu 430,000 kupitia gridi ndogo (Green Min and Micro Grid). Wameishia nyumba 17,302, yaani asilimia 20.

Uzembe wa kutohuisha taarifa za utafiti wa mradi, ulisababisha REA kuingia gharama za ziada Sh160 milioni.

Kuna jumla ya Sh5.94 bilioni, ambazo REA wamekuwa wakizitenga kama bajeti ya matangazo na elimu lakini hakuna maelezo ya zilivyotumika.

Mwaka 2018/2019, REA walitengeneza bajeti ya kununua transfoma na kuunganishia wateja umeme Sh254.8 bilioni. CAG akagundua, gharama halisi ilikuwa Sh117 bilioni. Kwa hiyo kulikuwa na udanganyifu wa Sh137.8 bilioni. Ufisadi.

Lingine, REA wilitumia Sh125.57 milioni, kununua transfoma 12 zilizo chini ya kiwango.

Siasa zikaingia. Tozo ya umeme kwa mwezi ikapitishwa Sh11,000. Serikali ikasema tozo Sh1,000. Gharama za uendeshaji zikawa kubwa kuliko mapato. Umeme ukazima vijijini.

Sehemu kubwa, CAG ameeleza tatizo la uchelewaji. Miradi ambayo ilipaswa kukamilika mwaka 2019/2020, mpaka sasa bado.

Hayo yalitokea Waziri wa Nishati akiwa Kalemani, aliyempokea Simbachawene kutoka kwa Muhongo. Rais simtaji. Hamkawii kusema namchukia John.

Ndimi Luqman MALOTO
Hakuna msafi ndan ya mfumo wa utawala huu!! Sio awamu ya tano pekee!!
 
Tunashukuru kwakuto mtaja raisi na tunashukuru kwa kuto mchukia John😂😂😂
 
Katika miaka 6 ya Magufuli amesambaza vijiji vingi na umeme wa bei nafuu kuliko marais wote tanganyika mpaka nyumba za nyasi ziliwekewa umeme, wakati kabla ya Magufuli ulikuwa ukiwasha umeme unaoneka bonge la tajiri, Sasahivi tumerudi kulekule kama una kuanzia sh,350,000 hauwezi pata umeme kutoka elfu 29.Magufuli amuwezi kimchafua kizembezembe kazi zake alizozifanya bado zinamtangaza, kipindi cha Magufuli hadi dawasco walikuwa unafungiwa maji bure unaanza kulipa taratibu, Sasahivi kajaribu uone.Magufuli hata hatungiwe riport namna hipi tulioshudia tawala zilizopita hatuelewi hayo maripoti.
Kwa hiyo unaipinga report ya CAG!?
Kumbe ndo mlimtimua Assad.
 
Katika miaka 6 ya Magufuli amesambaza vijiji vingi na umeme wa bei nafuu kuliko marais wote tanganyika mpaka nyumba za nyasi ziliwekewa umeme, wakati kabla ya Magufuli ulikuwa ukiwasha umeme unaoneka bonge la tajiri, Sasahivi tumerudi kulekule kama una kuanzia sh,350,000 hauwezi pata umeme kutoka elfu 29.Magufuli amuwezi kimchafua kizembezembe kazi zake alizozifanya bado zinamtangaza, kipindi cha Magufuli hadi dawasco walikuwa unafungiwa maji bure unaanza kulipa taratibu, Sasahivi kajaribu uone.Magufuli hata hatungiwe riport namna hipi tulioshudia tawala zilizopita hatuelewi hayo maripoti.
Hapa we ungejibu hoja tu kuonyesha kuwa taarifa hiyo ya CAG ni ya uongo...
 
Kweli nchi imejaa upumbavu wa hali ya juu tunajadili report ya 2021/2022,wewe unapiga kaunta ataki ya kingese hivi, endeleeni kutumika, watanzania hawatadanganyika tena
Kwa hiyo tufunike ya nyuma kisa tu Jiwe alihusika!!
 
Afu zikapigwa kelele tumefikisha umeme vijiji kadhaa, kwa pesa za ndani na kukatwa kwenye manunuzi ya umeme.

Kumbe msaada na pesa imeliwa. Iyo ndio ccm sasa
Kama tuneweza kusambaza umeme kwa vijiji elfu9 tutashindwa vijiji elfu3 kweli?kwa pesa za ndani,au nasema uongo ndugu zangu?
 
Nguzo zipi hazina viwango!hizi za Zege au za miti? mbona hatuoni hizo nguzo zikimeguka au kuangua tangu zisimikwe?enzi za Kikwete nguzo zilikuwa zinatoka mfindi zinapanda meli zipelekwa South Africa tunakuja kuuziwa nguzo moja kwa laki 8, Magufuli alivyoingia tu kakomesha huo mchezo, Sasahivi wanaanza maripoti eti nguzo zilikuwa chini ya kiwango,ili waanze mchezo wao, generator kuna mwekezaji mkubwa hapo Arusha alikuwa anatengeneza zinamdodea watu wanaagiza za nje wanaweka cha juu,wanaacha za ndani yule, mwekezaji akamlilia Magufuli alipotembelea hicho kiwanda,ndipo Magufuli alipoamuru tanesco waanze kununua hizo transformers,ili kuwezesha muwekezaji na watanganyika kupata ajira,wazee wa 10% walinchukia Magufuli, baada ya kifo chake wanaanza kutunga uongo ili waanze mchezo wao wa kuagiza nje ili wapate cha juu,huyu huyu CAG aliisha wahi andika riport kuhusu stendi ya mabasi ya kisasa ya Magufuli kuwa ilijengwa kimakosa na itakuja kusababisha foren ya kutisha pale Mbezi, Sasahivi anajionea aibu.
Mkuu hiyo stand ilikuja fanyiwa maboresho. Ila hii stand imepwaya, haina sehemu mahususi za kupokelea wageni kwa maana penye viti vya kukalia wale wanao kuja kupokea wageni wao, kama ilivyo stand ya Dodoma na hata za daladala.
 
Kwenye wizara hiyo wakati wa Kalemani kulikuwa na ufisadi wa hali ya juu. Kuna watu walipelekewa umeme, mtu mmoja, umbali wa zaidi ya kilometer 20 kwa gharama ya REA, lakini unapelekwa kwenye kabiashara kwa ndugu yake Kalemani. Kabiashara kenyewe, uwekezaji wake haufiki hata shilingi milioni 500.

Waziri alikuwa anacheza na media ili aonekane anafanya kazi sana wakati kwenye uhalisia ilikuwa tofauti. Umeme unapelekwa kwenye kijiji fulani, zinaunganishwa nyumba 2 au 4, waziri anaenda hapo na wanahabari kibao kutangaza tukio la kuwasha umeme kijiji fulani, lakini nyumba zilizounganishwa ni 2 au 4. Halafu timu ya ujenzi inahamia kijiji kingine. Kuna vijiji vingine mpaka leo, licha ya umeme kufika kijijini kwao karibia miaka 5 iliyopita, waliounganishiwa umeme, hawafiki hata 5% japo wameomba muda mrefu.

Kati ya Wizara ambazo efficiency ni very poor, Wizara ya Nishati ni miongoni. Mpaka sasa, hii Wizara haijapata unafuu wowote. Na kati ya mashirika ya hovyo kabisa galiyojaza watu ambao hawafanyi kazi, TANESCO, nadhani ni shirika la kwanza. Muda mwingi wamejazana ofisini, na kubakia wanazungukazunguka lakini hakuna cha maana wanachokifanya.
Umeongea point kubwa sana, huu upuuzi bado upo mpaka leo, wanaingia kwenye kijiji umeme wanaweka kwenye nyumba mbili alafu wanatangaza kijiji/ kitongoji kizima kuwa kina umeme. Ushenzi huu unanikera sana
 
Bichwa lako umelijaza matope wee chadema .

Hayaz Mbona hazianguki ??.

Mimi sio mtalaam wa masuala ya Umeme., Ninachojua ,nguvu ya Transfoma inategemea na idadi ya Kayak zipatazo huduma.

Unataka afunge. Transfoma ya 100KVA, kwa Kijiji ambacho kina watumiaji Umeme wasozidi hata mia mbili ??.

Hayaz bwana mtalaam , miundo mbinu ya Kupitisha Umeme wa 100KVA huko vijijin , ipo?.

JPM ni mwanasayansi, alijua alichofanya.

MAMA NLNA KIKUNDI CHAKE NI MAJIZI.

MAMA KATHIBITISHE, NI MWEPESIIIII, HAFAI KUA RAIS.
Watu wa JPM mna shida ya akili, CAG huyo huyo akisema serikali ya Samia imejaa ufisadi mnakuja humu kumpongeza kwa uzalendo. Ila huyo huyo akionyesha udhaifu wa JPM mnasema Hana akili!! Ndio nini Sasa?

Kama CAG ni muongo basi hata Samia sio fisadi!! Si muongo ama
 
Nguzo zipi hazina viwango!hizi za Zege au za miti? mbona hatuoni hizo nguzo zikimeguka au kuangua tangu zisimikwe?
Performance audit haikagui nyufa bali expected standards. Yaani kama mabati yanatakiwa 50 basi ukiweka 30 utaambiwa Kuna walakini hata kama jengo haitovuja Maji kwa kupelea bati!!

Sasa waTanzania mnataka mpaka siku umeme uanze kuleta shida ndio muanze kusema Kuna hujuma imefanyika. Kwa reasoning hii Wacha tuendelee kuibiwa maana hata ukiuziwa KIFAA feki maadam kinafanya kazi basi HAKUNA UFISADI.
 
Back
Top Bottom