Madudu ukaguzi maalum wa CAG upande wa REA 2015-2020

Sasa tukuamini wewe au tumwamini CAG aliyeenda field kufanya ukaguzi?
CAG hajasema pesa imeliwa, amesema transfoma zilizonunuliwa haziendani na specifications. Na ndio maana nikasema angekuwa na watu makini wangejua kwanini vijijini zinafungwa transoma za 50 kVA zaidi. Yes, ni kasoro ya kiukaguzi ambayo inaelezeka kirahisi kabisa.

Plus, Kichele haendi site, ni hao vijana wengine wameajiriwa juzi tu hapo, kuja mambo mengi hawayajui na hawana utaalamu nayo. Ripoti ya CAG sio msahafu, na ndio maana kamati za bunge huwa zinapitia hoja zote upya na kuomba ufafanuzi kutoka kwa wahusika. Kuna hoja nyingi tu za CAG huwa zinatupikiwa mbali.
 
Hakuna msafi ndan ya mfumo wa utawala huu!! Sio awamu ya tano pekee!!
 
Tunashukuru kwakuto mtaja raisi na tunashukuru kwa kuto mchukia John😂😂😂
 
Kwa hiyo unaipinga report ya CAG!?
Kumbe ndo mlimtimua Assad.
 
Hapa we ungejibu hoja tu kuonyesha kuwa taarifa hiyo ya CAG ni ya uongo...
 
Kweli nchi imejaa upumbavu wa hali ya juu tunajadili report ya 2021/2022,wewe unapiga kaunta ataki ya kingese hivi, endeleeni kutumika, watanzania hawatadanganyika tena
Kwa hiyo tufunike ya nyuma kisa tu Jiwe alihusika!!
 
Afu zikapigwa kelele tumefikisha umeme vijiji kadhaa, kwa pesa za ndani na kukatwa kwenye manunuzi ya umeme.

Kumbe msaada na pesa imeliwa. Iyo ndio ccm sasa
Kama tuneweza kusambaza umeme kwa vijiji elfu9 tutashindwa vijiji elfu3 kweli?kwa pesa za ndani,au nasema uongo ndugu zangu?
 
Mkuu hiyo stand ilikuja fanyiwa maboresho. Ila hii stand imepwaya, haina sehemu mahususi za kupokelea wageni kwa maana penye viti vya kukalia wale wanao kuja kupokea wageni wao, kama ilivyo stand ya Dodoma na hata za daladala.
 
Umeongea point kubwa sana, huu upuuzi bado upo mpaka leo, wanaingia kwenye kijiji umeme wanaweka kwenye nyumba mbili alafu wanatangaza kijiji/ kitongoji kizima kuwa kina umeme. Ushenzi huu unanikera sana
 
Watu wa JPM mna shida ya akili, CAG huyo huyo akisema serikali ya Samia imejaa ufisadi mnakuja humu kumpongeza kwa uzalendo. Ila huyo huyo akionyesha udhaifu wa JPM mnasema Hana akili!! Ndio nini Sasa?

Kama CAG ni muongo basi hata Samia sio fisadi!! Si muongo ama
 
Nguzo zipi hazina viwango!hizi za Zege au za miti? mbona hatuoni hizo nguzo zikimeguka au kuangua tangu zisimikwe?
Performance audit haikagui nyufa bali expected standards. Yaani kama mabati yanatakiwa 50 basi ukiweka 30 utaambiwa Kuna walakini hata kama jengo haitovuja Maji kwa kupelea bati!!

Sasa waTanzania mnataka mpaka siku umeme uanze kuleta shida ndio muanze kusema Kuna hujuma imefanyika. Kwa reasoning hii Wacha tuendelee kuibiwa maana hata ukiuziwa KIFAA feki maadam kinafanya kazi basi HAKUNA UFISADI.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…