Madudu ya Vyama vya Siasa kwenye Ripoti ya CAG

Madudu ya Vyama vya Siasa kwenye Ripoti ya CAG

benzemah

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2014
Posts
1,533
Reaction score
3,187
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)amebaini kasoro katika vyama vya siasa vikiwamo visivyo na bodi za wadhamini zenye ufanisi.

Vyama hivyo ni pamoja na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Chama cha Wananchi (CUF) na Democratic Party (DP) na CCM.

Hayo yamo kwenye ripoti ya mwaka ya CAG kuhusu ukaguzi wa Serikali Kuu kwa mwaka wa fedha ulioisha Juni 30, mwaka jana.

Taarifa ya CAG imeeleza kuwa bodi za vyama hivyo hazikuwa na ufanisi katika kusimamia utendaji kazi wa vyama vyao kwa mujibu wa kifungu cha 21(1) cha Sheria ya Vyama vya Siasa Sura ya 258 (iliyorejewa 2019).

Sheria hiyo inasema vyama vya siasa vilivyosajiliwa vinatakiwa kuwa na bodi ya wadhamini iliyosajiliwa yenye jukumu la kusimamia mali za chama, uwekezaji na biashara nyingine yoyote.

Aidha, Sheria ya Usajili, Udhamini Sura ya 318 (iliyorejewa 2002) inampa mamlaka Kabidhi Wasii Mkuu wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) Kusajili Bodi za Wadhamini.

CAG amependekeza Bodi za Wadhamini za vyama hivyo kuhakikisha zinafanya vikao vyote vilivyotajwa katika katiba zao ili kusimamia kwa ufanisi masuala ya kifedha.

Akirejelea Kanuni za Fedha za Chama cha Wanarchi (CUF) za mwaka 2014, ripoti inasema bodi ya wadhamini ya chama inatakiwa kuandaa na kuwasili-sha ripoti za mali kwa Baraza Kuu la Uongozi.

Hata hivyo, CAG amebaini kuwa Baraza la Wadhamini halikuzingatia kanuni hii na hivyo haikuwasilisha ripoti ya mali kwa Baraza Kuu la Uongozi. Hali hii inatajwa kuwa inapunguza uwezo wa Baraza la Uongozi kutambua mali za chama zilizopo na hali yake.

Kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na CUF, CAG amebaini vina udhaifu katika kusimamia miradi yao ya uwekezaji.

"Napendekeza Bodi za Wadhamini za CUF na CCM zikutane mara kwa mara na menejimenti ili kujadili maendeleo ya miradi ya uwekezaji na kuhakikisha mapato yanayoto-kana na uwekezaii yanasaidia katika uendeshaji wa shughuli za vyama ili kufikia bajeti," CAG amependekeza.

Aidha, CAG amebaini katiba ya Chadema inaitaka Bodi ya Wadhamini ya chama hicho kufanya mikutano isiyopungua mitatu kila mwaka.

"Hata hivyo, nilibaini kuwa Bodi ya Wadhamini ya CHADEMA haikufanya mikutano yoyote katika mwaka huu wa fedha," inasema ripoti ya CAG. Kwa mujibu wa ripoti, Menejimenti ya CHADEMA ilihusisha suala hili na ukosefu wa fedha, jambo ambalo lilisababisha kushindwa kuitisha vikao vya bodi.

"Kushindwa kufanya vikao kunatia shaka zaidi kuhusu uwezo wa bodi kukagua mali na uwekezaji wa chama, amesema CAG. Pia, amesema inatia shaka uwezo wa chama hicho katika kubaini matumizi mabaya ya fedha ambayo yanaweza kuhatarisha upotevu wa rasilimali za chama.

Kwa upande wa DP, ukaguzi ulibaini kuwa chama hicho kwa sasa kina wajumbe watatu tu, kwani wajumbe wawili walikuwa wamejiuzulu tangu Juni 2021 na hakuna mbadala wao.

Kutokana na kutokuwapo kwa wajumbe hao wawili, Bodi ya Wadhamini haikuitisha vikao vyake katika kipindi cha kuanzia mwezi Juni 2021 hadi Juni 2022 na kusababisha kutoku-wepo kwa usimamizi kuhusu utendaji wa kifedha wa chama, mali, uwekezaii na biashara.

Jambo lingine ambalo limebainika katika ukaguzi ni vyama vya Chadema, DP, NRA, UMD na UPDP kutowasilisha tamko la kila mwaka la mali kwa Msajili wa Vyama vya Siasa.
 
Wanasiasa wote wapuuzi tu , wezi wezi waongo waongo na n.k

USSR
 
Back
Top Bottom