Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Wakili wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), William Maduhu, amesema hawakuona ushahidi wowote unaoonesha kuwa vijana kutoka nchi jirani walikodiwa kuja kushiriki katika maandamano yaliyofanyika nchini mwaka jana Oktoba.
Maduhu ameyasema hayo Mei 16, 2026, katika Mjadala wa Kitaifa Kuhusu Khatma ya Nchi, akieleza kuwa akiwa wakili katika kesi hizo alichambua hati za mashtaka za watu 1,651 na hakubaini mtuhumiwa yeyote kutoka nje ya Tanzania, huku akisema Ripoti ya Chande pia haikutoa maelezo yoyote kuhusu madai hayo.
Ameongeza; "Walikuja mbele yetu vijana ambao walikuwa wana-boxer, maanake walikamishwa wakiwa majumbani hawakuwa na madhumuni. Wengine wanawake wamevaa madela, walikuwa majumbani. Wengine waliokuwa wamekuja pale hawana miguu, wamefungwa na kamba, sio bandage, kamba ya katani! Mtu amefungwa mkono hapa na kamba mahakamani pale. Tumeiambia Tume, lakini kwenye ripoti yake haijasema chochote."