Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wamekufa wengine yeye atakufa next timeMbona hujafa hadi umekuja kupost hapa?😂
Kwa siku za karibuni hapa JF kuna mjadala mkali sana unaendelea kuhusu taaluma ya ufamasia na maduka ya dawa hapa Tanzania. Kupitia mijadala hiyo, nimejifunza mambo kadhaa ambayo hapo kabla sikuyajua kwa kina. Nimegundua mambo haya:
1. Mtu ili kuanzisha na kuendesha biashara ya duka la dawa, huihitaji uwe ni mfamasia kitaaluma bali unahitaji kukodisha cheti cha mfamasia yoyote na kukitundika kwenye duka lako la dawa, na kuanzia hapo utauza dawa yoyote hata kama elimu yako ni darasa la saba! Hii ni sawa na rubani mwenye leseni ya kurusha ndege za abiria kuikodisha leseni yake kwa kampuni ya ndege ili itundikwe ndani ya ndege, halafu mtu yoyote anaweza kushika usukani wa ndege na kuamua kuirusha ndege!
2. Kumbe wafamasia kitaaluma hawajui (hawakufunzwa) na hawapaswi kumpima mgonjwa (examination), kugundua ugonjwa (diagnosis), kuidhinisha dawa za kutumia (Prescription) au kumtibu mgonjwa kwa dawa (drug administration). Mfamasia anapaswa tu kumgawia mgonjwa dawa (drug dispensing) kwa mujibu wa kibali cha Daktari. Ajabu ni kuwa huku mitaani maduka ya dawa ndio hospitali zisizo rasmi, tukiumwa tunaenda na pesa kwenye duka la dawa na kutibiwa faster!
3. Kiujumla karibu dawa zote hazipaswi kuuzwa na duka lolote la dawa mpaka kibali rasmi cha dawa kutoka kwa Daktari (Prescription). Ajabu ni kuwa huku mtaani dawa yoyote unaweza ukauziwa na duka lolote la dawa ukienda na pesa tu!
Baada ya kupitia hayo yote nimegundua wazi kubwa, kiujumla maduka ya dawa hapa Tanzania huenda kwa sehemu kubwa yanatuibia, kutuumiza, kuharibu afya zetu na kutuua!
uko sahihiKuondolewa na wasifanye kazi hapo sijui. Kilichositishwa ni mafunzo, hayatotolewa tena endapo watu watahitaji
Umeisoma hiyo Pharmacy ACT ?Kuanzisha pharmacy ni jambo moja na kuendesha pharmacy ni jambo lingine. Mimi mgonjwa ninayefika duka la dawa kununua dawa, cheti cha mfamasia kilichotundikwa kinanisaidia nini?
Wewe ukienda Dukani kununua Bidhaa leseni ya biasharaa inakusaidia nini???Kuanzisha pharmacy ni jambo moja na kuendesha pharmacy ni jambo lingine. Mimi mgonjwa ninayefika duka la dawa kununua dawa, cheti cha mfamasia kilichotundikwa kinanisaidia nini?
Anaijiaa bhasi[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Yani wanavyotapa tapa ila Addo hairudi yani wakitaka warudi darasaniiUmeisoma hiyo Pharmacy ACT ?
Mkuu 'Zanzibar ASP', Samahani, naona hujajifunza chochote hapa bali umekubali kupotoshwa au kuimarisha mawazo potofu uliyokuwa nayo toka mwanzo.1. Mtu ili kuanzisha na kuendesha biashara ya duka la dawa, huihitaji uwe ni mfamasia kitaaluma bali unahitaji kukodisha cheti cha mfamasia yoyote na kukitundika kwenye duka lako la dawa, na kuanzia hapo utauza dawa yoyote hata kama elimu yako ni darasa la saba! Hii ni sawa na rubani mwenye leseni ya kurusha ndege za abiria kuikodisha leseni yake kwa kampuni ya ndege ili itundikwe ndani ya ndege, halafu mtu yoyote anaweza kushika usukani wa ndege na kuamua kuirusha ndege!
Hili nalo umepotoka, pamoja na kuwa kweli kwamba siyo kazi ya MFamasia kutambua matatizo yanayomhusu mgonjwa. Hii ni kazi ya taaluma nyingine, na hili siku zote linajulikana. Nashanga sana kwamba wewe ndio leo umelifahamu. Wewe tokea utotoni mwako umekuwa huendi kutibiwa hospitali? Uliwahi hata siku moja kwenda Famasi moja kwa moja kupata dawa kabla ya kumwona daktari? Huu ni uongo ulio wazi kabisa kwa malengo uliyonayo mwenyewe, na kujaribu kuhalalisha jambo ambalo hata kama hukulijua, bado hulijui na unajiapiza umejifunza hapa JF.2. Kumbe wafamasia kitaaluma hawajui (hawakufunzwa) na hawapaswi kumpima mgonjwa (examination), kugundua ugonjwa (diagnosis), kuidhinisha dawa za kutumia (Prescription) au kumtibu mgonjwa kwa dawa (drug administration). Mfamasia anapaswa tu kumgawia mgonjwa dawa (drug dispensing) kwa mujibu wa kibali cha Daktari. Ajabu ni kuwa huku mitaani maduka ya dawa ndio hospitali zisizo rasmi, tukiumwa tunaenda na pesa kwenye duka la dawa na kutibiwa faster!
LOooh,Kiufupi hizo ndio tiba tunazopata huku Mtaani kwetu, na kwenda kwa mbele kwa "Wataalamu" ni kujilipua tu....kwa hiyo kufunga maduka labda mtatusaidia kukimbilia kwa kina Mwampesa, GwaJuma and co...wao Magonjwa yote wanatutibu kwa kutoa tu sadaka elfu kumi au ishirini.
Nilihisi tu kuna jambo juu ya kelele hizi nyingi na za ajabu sana.Ilikuwa hadi wapate mafunzo ya ADDO kwanza ndipo wanaruhusiwa kuyamiliki na kuuza.
Pia watu ambao walikuwa hawana elimu ya afya walikuwa wanapatiwa mafunzo ya ADDO ya umiliki wa DLDM na walipaswa kuweka mtu anayeweza kuuza ambaye anazitambua dawa.
Sasa ADDO imesinamishwa ndio unaona kelele zote hizi.
Hata hivyo hizi kelele ni kama njia tu, agenda kubwa hapa ni suala la maslahi tu kwenye hii Business of Pharmacy. Imeonekana Wafamasia wanafaidi sana kwenye hii business yao
Maeneo ya kijijini kwetu kuna mtu amefariki ndo amezikwa jana Mungu amlaze mahali pema peponi. Kisa tu alienda duka la dawa wakamuuzia dawa akarudi home kumbe tatizo lake ilibidi akae wodini hata siku mbili coz Sugar ilikua juu na Bp ilikua juuTuanze kwanza, kuna wangapi wameherabiwa afya na kuuwawa na hayo maduka ya dawa unayoyaongelea? Kuna takwimu zilizokusanywa? Serikali ikikurupuka na kuyabana maduka ya dawa inaweza kuleta matatizo tena haswa kwa wale watu wenye kipato cha chini. Gharama zitaongezeka kwa sababu urasimu unaongozeka.
Nani kakwambia maduka ya dawa ni hospitali? Ondoa ujinga huo kwanza. Ukiwa waharisha usiende duka la dawa kuuliza dawa, nenda hospitali kwanza, wakikuandikia dawa ndipo waweza nunua popote pale kwenye duka la dawa.Kwa siku za karibuni hapa JF kuna mjadala mkali sana unaendelea kuhusu taaluma ya ufamasia na maduka ya dawa hapa Tanzania. Kupitia mijadala hiyo, nimejifunza mambo kadhaa ambayo hapo kabla sikuyajua kwa kina. Nimegundua mambo haya:
1. Mtu ili kuanzisha na kuendesha biashara ya duka la dawa, huihitaji uwe ni mfamasia kitaaluma bali unahitaji kukodisha cheti cha mfamasia yoyote na kukitundika kwenye duka lako la dawa, na kuanzia hapo utauza dawa yoyote hata kama elimu yako ni darasa la saba! Hii ni sawa na rubani mwenye leseni ya kurusha ndege za abiria kuikodisha leseni yake kwa kampuni ya ndege ili itundikwe ndani ya ndege, halafu mtu yoyote anaweza kushika usukani wa ndege na kuamua kuirusha ndege!
2. Kumbe wafamasia kitaaluma hawajui (hawakufunzwa) na hawapaswi kumpima mgonjwa (examination), kugundua ugonjwa (diagnosis), kuidhinisha dawa za kutumia (Prescription) au kumtibu mgonjwa kwa dawa (drug administration). Mfamasia anapaswa tu kumgawia mgonjwa dawa (drug dispensing) kwa mujibu wa kibali cha Daktari. Ajabu ni kuwa huku mitaani maduka ya dawa ndio hospitali zisizo rasmi, tukiumwa tunaenda na pesa kwenye duka la dawa na kutibiwa faster!
3. Kiujumla karibu dawa zote hazipaswi kuuzwa na duka lolote la dawa mpaka kibali rasmi cha dawa kutoka kwa Daktari (Prescription). Ajabu ni kuwa huku mtaani dawa yoyote unaweza ukauziwa na duka lolote la dawa ukienda na pesa tu!
Baada ya kupitia hayo yote nimegundua wazi kubwa, kiujumla maduka ya dawa hapa Tanzania huenda kwa sehemu kubwa yanatuibia, kutuumiza, kuharibu afya zetu na kutuua!
Umenigusa sana... kula 💕Gharama za hospital ni kubwa sana mkuu! Hadi kumuona daktari sio chini ya shilingi 5000, vipimo, foleni, na adha nyingi. Maduka ya dawa yanasaidia sana, japo wanatoa dawa kiholela ila inasaidia.
Mkuu ungelitoa na vijimifano kidogo kwa namba mbili(2).Mengine unayotakiwa kuyajua juu ya taaluma ya ufamasia na maduka ya dawa
MAKUNDI YA DAWA ZA BINADAMU 👇👇
1. Prescription Only Medicines ..(Cheti cha daktari kinahitajika )..hizo zenye "Dose;As directed by Physician".
2. Pharmacy Only Medicines(Cheti cha daktari hakihitajiki).
3. General Sale Medicines(Cheti cha daktari hakihitajiki)..hizi utazikuta hata dukani kwa mangi/mpemba n.k. mfano DAWA TATU/ACTION/HEDEX/PANADOL & PANADOL EXTRA/GLUCOSE /COFTA/TUMBOCID/ MOSQUITO (spray and repperants),CASTROL OIL/GLYCERINE/MEDICATED SOAPS /TOOTH PASTE/CONDOMS n.k.
KUHUSU DAWA ZIAZOTOLEWA KWA CHETI CHA DAKTARI (Prescription Only Medicine);
Dawa hizi zinazotolewa kwa cheti cha daktari kwa sababu zinachukuliwa kuwa hatari ikiwa hazitatumiwa chini ya usimamizi wa mtaalamu wa afya aliyeidhinishwa.
Dawa hizo kwa ujumla zinakusudiwa kutibu matatizo makubwa zaidi ya kiafya. Hii inaweza kujumuisha kisukari, saratani,magojwa ya moyo,bakteria,virusi nk.
Baadhi ya nchi kama vile Uingereza wapo wafamasia na manesi ambao wameidhinishwa kutoa(TO PRESCRIBE) baadhi ya dawa hizo.👇👇👇👇👇Nurses and pharmacists can prescribe as effectively as doctors - NIHR Evidence
Unamaanisha huko mbeleni mahospitalini hakutokuwa na manesi? Watakuepo wafamasia na madaktari tu?Kwanza tambua kuwa ADDO ilianzishwa kwa sababu Pharmaceutical Personell walikuwa wachache, kwa sasa wapo wengi. Hizo nafasi zinaenda kwa wahusika.
Angalia hata mahospitalini, manesi walikuwa wanafanya kazi pharmacy kutokana na uhaba wa watu wa famasi. Ila kwa sasa watu wa Famasi wameongezeka na ile namba ya manesi inazidi kupungua kadri wanavyostaafu(maana hawawezi kutolewa kwa nguvu) hatimaye itaisha na nafasi zichukuliwe na wahusika.
Acha kujitoa ufahamu, hujaona mtu anaachwa kuhudumiwa hospitali kwasababu hana pesa?Kuna kitu kinaweza kuvuka gharama ya uhai au afya ya mtu?
Standard za msingi zinaweza zisiwe na gharama kubwa bali zinahitaji umakini tu.