Maduka ya dawa Tanzania yanatumika kutuibia, kututesa, kuharibu afya zetu na kutuua?


Unatakiwa kujifunza zaidi. Inaonekana knowledge gap kwako ni Kubwa Sana Yaani.
 
Kuanzisha pharmacy ni jambo moja na kuendesha pharmacy ni jambo lingine. Mimi mgonjwa ninayefika duka la dawa kununua dawa, cheti cha mfamasia kilichotundikwa kinanisaidia nini?
Umeisoma hiyo Pharmacy ACT ?
 
Madaktari mmecharuka toka ADDO mzuiwe kila mtu ale kwa urefu wa kamba
 
Kuanzisha pharmacy ni jambo moja na kuendesha pharmacy ni jambo lingine. Mimi mgonjwa ninayefika duka la dawa kununua dawa, cheti cha mfamasia kilichotundikwa kinanisaidia nini?
Wewe ukienda Dukani kununua Bidhaa leseni ya biasharaa inakusaidia nini???
 
Mkuu 'Zanzibar ASP', Samahani, naona hujajifunza chochote hapa bali umekubali kupotoshwa au kuimarisha mawazo potofu uliyokuwa nayo toka mwanzo.

Chukulia mfano wa hilo hapo uliloandika hapo juu.
Niambie, ni sheria gani Tanzania inayoruhusu maduka ya dawa kutumia vyeti vya Famasia bila Famasia kuwa mwangalizi/msimamizi wa shughuli zinazoendelea dukani humo.

Nieleze kwa uhakika ni wapi katika jukwaa hili palipoelezwa hayo uliyoweka hapo juu!

Kama wewe uliona au kusikia kuwa hayo yanafanyika, umejiridhisha kwamba ndio utaratibu ulioruhusiwa na sheria na mamlaka inayosimamia taaluma ya Famasia? Kwa nini ulalamike na kujiapiza kabisa hili "umejifunza" jukwaani hapa? Ni nani katika wachangiaji aliyesema kuwa hivyo ndivyo inavyotakiwa kuwa ndani ya Famasi?
Hili nalo umepotoka, pamoja na kuwa kweli kwamba siyo kazi ya MFamasia kutambua matatizo yanayomhusu mgonjwa. Hii ni kazi ya taaluma nyingine, na hili siku zote linajulikana. Nashanga sana kwamba wewe ndio leo umelifahamu. Wewe tokea utotoni mwako umekuwa huendi kutibiwa hospitali? Uliwahi hata siku moja kwenda Famasi moja kwa moja kupata dawa kabla ya kumwona daktari? Huu ni uongo ulio wazi kabisa kwa malengo uliyonayo mwenyewe, na kujaribu kuhalalisha jambo ambalo hata kama hukulijua, bado hulijui na unajiapiza umejifunza hapa JF.

Hili swala la "Drug administration" linatumika kuwachanganya tu watu.
Drg administration inahusu mgonjwa kumeza, kupaka, kudunga sindano, kuweka machoni au sikioni au sehemu za siri, n.k.

Katika njia zote hizo za kumpa mgonjwa dawa, ni njia chache sana, kama ya kudunga sindano inayohitaji NESI (na kiukweli si daktari), amdunge sindano mgonjwa.
Dawa nyingi nyingine, anayehusika katika ku'administer' dawa ni mgonjwa mwenyewe, baada ya kufahamishwa namna ya matumizi ya dawa aliyopewa, kama vidonge. Kama mgonjwa ni mahututi yupo hospitali, atapewa dawa hizo na nesi. Au kama ni mtoto nyumbani, mama anachukua jukumu la kumpa mtoto dawa kama ilivyoelekezwa.

Sasa hili unalosema Famasia hawezi ku'administer' dawa ni jambo ambalo sio la ukweli, bali ni upotoshaji. Kwa sababu dawa nyingi zaidi ni mgonjwa mwenyewe anaye'administer' na wala siyo daktari.

Lakini tusiishie hapo. Unaposema Famasia hajui ku'adminster' dawa, huo ni uongo, kwa sababu kati ya Daktari, nesi na Famasia, ni Famasia pekee anayejua kwa undani zaidi njia sahihi inayofaa kwa mgonjwa kutumia dawa, kwa kumeza, au kuweka machoni, au kuweka kwenye ngozi, n.k., kwa sababu yeye anaifahamu vizuri zaidi dawa

Kuepuka kuandika kirefu sana, ngoja nikwambie hili la mwisho:

Unapoona daktari akiandika dawa, usidhani daktari huyo kila kitu kipo kichwani mwake. Katika kutibu kuna "GUIDELINES", taratibu zinazotakiwa kufuatwa, na katika kila ugonjwa kuna dawa zake maalum zilizoainishwa zitumike. Kwa hiyo usidhani daktari anajua kila nittygritty ya kila kitu katika matibabu hayo. Katika upande wa dawwa, ukimchuka Famasia na Daktari kawaweka uwanjani na kuwapa maswali nje ya "GUIDELINES" utakuta daktari haendi mbali..

Hayo mengine ya huko chini ya upotoshaji bado sijayasoma.
Lakini bandiko lako hapa ni mwendelezo ule ule wa watu wenye maslahi, maslahi ambayo yameguswa, sasa wanageukia taaluma husika na kuanza kuwatupia lawama.
Ndiyo, kuna lawama stahiki, kama hizo za kutumia vyeti kwenye Famasi bila Famasia mwenyewe kuwepo hapo mahala. Lakini hili ni kosa, kama makosa mengine yanayofanywa, tena zaidi upande huo unaolilia kwamba ni wajuaji zaidi wa dawa kuliko watu waliosomea fani wenyewe.

Sikuhakiki andiko hili, kama kuna makosa, kunradhi.
 
LOooh,
Hili la mkasa ulioueleza hapa lilikuwa halijaingia akilini mwangu kabisa.

Ahsante sana kwa kunifungua macho.

Sasa nimeelewa vizuri maana ya kampeni hii dhidi ya Famasi.

Ahsante sana mkuu 'May Day', kwa kuueleza mkasa huu.

Hii ni vita ya kibiashara, tena biashara haramu?
 
Nilihisi tu kuna jambo juu ya kelele hizi nyingi na za ajabu sana.

Now I know.
 
Kule
Maeneo ya kijijini kwetu kuna mtu amefariki ndo amezikwa jana Mungu amlaze mahali pema peponi. Kisa tu alienda duka la dawa wakamuuzia dawa akarudi home kumbe tatizo lake ilibidi akae wodini hata siku mbili coz Sugar ilikua juu na Bp ilikua juu
 
Nani kakwambia maduka ya dawa ni hospitali? Ondoa ujinga huo kwanza. Ukiwa waharisha usiende duka la dawa kuuliza dawa, nenda hospitali kwanza, wakikuandikia dawa ndipo waweza nunua popote pale kwenye duka la dawa.
 
Gharama za hospital ni kubwa sana mkuu! Hadi kumuona daktari sio chini ya shilingi 5000, vipimo, foleni, na adha nyingi. Maduka ya dawa yanasaidia sana, japo wanatoa dawa kiholela ila inasaidia.
Umenigusa sana... kula πŸ’•
Tatizo la hospitali si gharama peke yake... Kuna thamani ya mtu, muda na quality ya huduma.
Hospitali/zahanati/vituo vya afya vinachangia watu kutafuta shortcuts ikiwemo wenye smart phones kutumia google kujitafutia tiba!
 
Hii vita sijui mwisho wake lini..?mana madaktari njaa hawaamini wanachokiona...mafamasia tuendelee kushikiria hapo hapo.

Halafu mleta uzi hujui hata maana ya neno afya..rudi shule kajifunze mana ya neno afya.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeishia hapo kwenye 'usukani' wa ndege, wewe jamaa ni FUTUHI ila sikuwahi kudhani ni mweupe kiasi hiki…. ukiweza kumwamini koboko basi utaamini kila kitu.
 
Mkuu ungelitoa na vijimifano kidogo kwa namba mbili(2).
 
Kitu pekee ambacho mnatakiwa Mkijueee ADDO ishazikwaa.
 
Unamaanisha huko mbeleni mahospitalini hakutokuwa na manesi? Watakuepo wafamasia na madaktari tu?
 
Kuna kitu kinaweza kuvuka gharama ya uhai au afya ya mtu?
Standard za msingi zinaweza zisiwe na gharama kubwa bali zinahitaji umakini tu.
Acha kujitoa ufahamu, hujaona mtu anaachwa kuhudumiwa hospitali kwasababu hana pesa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…