Maduka ya dawa Tanzania yanatumika kutuibia, kututesa, kuharibu afya zetu na kutuua?

Sasa hapo mwenye makosa mwenye Duka au Sisi wananchi?
Kama unaipenda Afya yako huwezi kufanya hayo yote.
 
Sio tuu kusimamisha mafunzo ya ADDO; haya maduka/DLDM yalitakiwa yafungwe na yasiwepo kabisa.
 
Wewe ukienda Dukani kununua Bidhaa leseni ya biasharaa inakusaidia nini???
Akikujibu ni tag naona wivu unazidi kupamba moto dhidi ya WAFAMASIA.

Nguvu nyingi Zina tumika kuwapoteza WAFAMASIA lakini sidhani kama wataweza.
 
Upo sawa kabisa,alafu wanaleta longolongo hapa na ADDO zao, kwanza nafikili wote wenye viduka muhim na pharmacy walitakiwa shitakiwa wameisha umiza Sana afya za watu wetu,

Alafu mtu mmoja anakuja pinga uchambuzi wa doctor mbobezi , na prof just kwamba ni mfamasia ujinga mtupu
 
Tangu lini sikio likazidi kichwa, mtajua hamjui leteni ubishi na masinior wenu
 
Sio dawa zote zinaitaji kibali cha daktari ili ununue
 
Nini kifanyike Kwa maoni yako
 
Hapa kuna ulaji.

Hakuna mtu yoyote aliyeharibiwa na duka la dawa

Lawama wanazo manesi na mahospitalini huko ndio kuna uzembe
 
Ushauri wa prof kupitia bandiko jf uzingatiwe,
Utengenezwe utaratibu mpya wa uratibu wa biashara hii, au ipigwe burn kuliko humiza afya za wananchi
Yale yalikuwa maoni yake.Vipi ya kwako????

Halafu swala la afya za wananchi,wananchi wenyewee ndiyo wanatakiwa kufata sheria.Mwananchi yeyote asiende pharmacy bila kuwa na cheti cha daktari.Uzuri serikali inajitahidi kutoa elimu hiyo kupitia vyombo vya habari.

Kuna lile Tangazo kwenye tv Wakati WA taarifa ya habari Lina rudiwa karibia mara tatu tatu.Kwamba wananchi hawalioni????

Mgonjwa anajihisi tumbo kuuma,anaenda pharmacy.Anamkuta mfamasia.Mfamasia anamuomba cheti kutoka Kwa daktari. HILI TANGAZO ITV MUDA WA TAARIFA YA HABARI SAA 2 USIKU LINARUDIWA SANAA.

#nimelitafuta YouTube nimelikosa.
 
Mkuu ndo Hali alisi ilivyo mitaani,?kumbuka wapo wananchi ukiuliza ni serikali hii awamu ya ngapi hawajui ,je Hawa tunawasaidiaje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…