Ujenzi wa stand kuu Arusha bado ni kizungukumkuti hadi sasa licha ya maelekezo ya mara kwa mara kutoka serikalini kuwa ujenzi huo uanze mara moja.
Naibu Waziri wa Ardhi nyumba na Maendeleo mh. Geofrey Pinda alitoa maelekezo mwezi wa tatu mwaka huu kuwa ujenzi huo uanze ndani ya siku 30 lakini hadi sasa ujenzi huo bado kuanza.
Najiuliza tamko hilo la Waziri lilikuwa la kisiasa au mamlaka zimeamua kupuuzia kauli hiyo ya kiongozi wa Serikali?
Arusha kuna namna wanavyoendesha mji wao
Ni aibu mji wenye majengo yenye hadhi na mazuri ila hakuna stand ya maana,usafiri unatabu,daladala bado ni zile fupi unakosa comfort ukivitumia
Manispaa na uongozi woote wajitathmini watabaki nyuma abadan