Logikos
JF-Expert Member
- Feb 26, 2014
- 15,460
- 24,233
Maelewano na mshikamano ni Priceless - Kwahio chochote kile hata kama kina faida kiasi gani za kifedha hakiwezi kuziba pengo litakaloweza kuachwa na Jamii kutokuelewana....
Mfano kuna Wadau walienda vijijini kuwajengea watu nyumba za Kisasa kwa gharama kubwa na zingekuwa faida sana kwao (mwisho wa siku watu hawakuingia) baada ya kujiuliza ni nini kimetokea kumbe kulikuwa na upotoshaji kwamba nyumba zile ni za freemason.., Hivyo kosa la kutokuwahusisha watu kuanzia mwanzo kulisababisha mradi mzuri na wa faida kwao kuwa hasara kubwa kwa pande zote zilizohusika....
Suala la Bandari lina sura kama hii na sababu kuna sintofahamu je ni vema kuendelea hata kama kweli lina faida za kiuchumi kwa gharama ya kutokuelewana kwa Jamii ?
Kuna wale wanaosema tatizo sio Mkataba ni Uarabu wa Mwarabu..., Hata kama ni kweli Je hao wenye Hofu ya Mwarabu wana Hoja ? (Kama babu zao walitawaliwa na hilo hilo taifa na wengine kuchukuliwa utumwani utawalaumu kwa kusita kwao ? Hawa watu sio wabaguzi sababu waarabu ni ndugu zetu tunaishi nao ila wakisikia kuna Kampuni moja inayokuja na kupewa exclusivity wanaweza kudhani huu ni ukoloni unarudi; Ukizingatia hata kipindi cha Ukoloni zilikuwa ni Kampuni zenye back-up ya serikali zao ndio zilikuwa zinazoongoza ukoloni....; (Chartered Companies) mfano Germany East Africa Company....
Kwahio Busara ingetumika..., ili kuondoa hii sintofahamu na kupata vyote kwanini badala ya kampuni moja kupewa exclusivity zisipewe Kampuni zaidi ya moja na kwa muda mfupi mfupi wakati na sisi tunajifunza kwa kufanya nao...
Badala ya Kuwapa hawa ambao kuna watu wanawaogopa kwa uarabu wao (kwanini wasiwape wao na wengine) ukizingatia hawa DP World wana sifa ya kutoa Rushwa..., kwa nchi yetu hii ya wapenda rushwa si tutakuwa tunaharibu hata kabla ya kuanza ?
Narudia tena Social Harmony ni muhimu zaidi kuliko any Financial au Economical Gains