Maelezo binafsi ya Emmanuel Adebayor kuhusu mgogoro wake na Familia yake

Maelezo binafsi ya Emmanuel Adebayor kuhusu mgogoro wake na Familia yake

ndio mana mimi naunga mkono kauli ya floyd mayweather kwamba hawezi kuisaidia africa,pesa zake ni za watoto wake.extended family ni majanga.
 
ana matatizo huyo adebayor!!.. anashangaa matatizo ya familia yake??.. hatakiwi kuyashangaa as if yeye ni mzungu hayo matatizo ni changamoto tu kutokana na mazingira tunayosihi. Hawa kina Abeid pele, Kalausha Bwalya, Ikwechuku, nk haimaanishi familia zao hazikua na matatizo kama hayo lakini hatujui kwa sababu walijua ku handle kifamilia hayo mambo!.. anachojaribu kutuambia hapa ni kwamba familia yake ina watu wajinga wasio na uelewa akiwemo mama yake!!...yaani nautangazia ulimwengu kuwa ana mama mjinga!!.. haya hata wazungu wenyewe hawafanyi hata kama wana wazazi watata kiasi gani!! shame on him!
 
japo kaongelea upande mmoja naweza kukubaliana naye familia nyingi za afrika ni tabu
 
Ogopa sana Moyo usio na shukrani usioridhika ni hatari sana Watu ka hao ishi nao kwa akili sana
 
Hawezi kuongea yote hayo naona yamemfika shingoni, halafu kila mmoja anataka awe na utajiri wake.
Huyo dogo aliempeleka kujiendeleza na soka akaiba simu zote ndio balaaa ya wote
 
Ilo mbona linawezekana... Mshahara Million 300/=Tsh. tena kwa wiki.

Atashindwa vipi kulipa mil 1 kwa ndugu 20 tu. Yaani tena kwa mwezi.


Hashindwi, mbona kawapiga sana Tafu huko mwanzo?

tatizo ndugu wenyewe hawana shukrani, bado wanamzingua tu!,

wangekuwa watiifu kwake mbona easy tu
 
Pole Adebayo
mshana jr huyu Adebayor katoka familia ya kishirikina sana. Kinachomkera mama yake ni yeye kutompa matunzo stahiki (japo ilitakiwa mama yake atumie busara) na kuajiri wachawi wa kiafrika na kituruki anaowalipa hela nzuri.

Sasa hawa wachawi wakamwambia Ade kwamba familia yake ndo inamroga asifanye vizuri. (wakati haya ni mambo ya umri alipokuwa na umri mzuri alichanua mpaka kuwa mchezaji bora Afrika)

Tokea hapo anamchukia mama yake na familia yote.
 
Last edited by a moderator:
Nimepitia huu uzi kwa umakini, wakati nawaza niandike nini kila mara nikakuta naikumbuka signature ya Nyani Ngabu

Miafrika ndivyo tulivyo!

japo hua hainifurahishi sana
 
Last edited by a moderator:
Ilo mbona linawezekana... Mshahara Million 300/=Tsh. tena kwa wiki.

Atashindwa vipi kulipa mil 1 kwa ndugu 20 tu. Yaani tena kwa mwezi.

mkuu umefikiria kirahisi sana...huyo analipwa mil 300 kwa wiki na yeye ana familia yake inahitaji nyumba ya kuishi inahitaji chakula mavazi matibabu na starehe zingine...usisahau pia kuna kodi anakatwa karibia 50% ya pesa yote...anaishi eneo la matajiri nyumba ni expensive...bado bodyguards na mengineyo.

pia kwanini nimlipie mtu gharama za kuishi...kwanini asifanye kazi na ajiendeshe mwenyewe kimaisha?...watoto wa adebayo watarithi nini toka kwa baba yao akifa leo au kesho?

just think outside the box broo...au ndio kufikiria kiafrica zaidi..kwamba unapesa basi ndugu zangu nao niwagawie tuu.
 
Kosa la Emma ni kuwapa ndugu zake pesa na mali. Leo hii akipiga hesabu anajikuta ni nyingi lakini practically zimetumika na hazipo. Wapeni nyavu wakavue wenyewe hao...
Ndugu siyo wa kuchekea wasaidie,ila isiwe kila siku.Maana ukiwapa kila siku watabweteka kwanza matumizi yao ni ya juu kuliko hata mtafutaji mwenyewe.Hawana huruma,siku ukiishiwa nd wa kwanza kukusema vibaya,kukucheka
 
Back
Top Bottom