Maelezo kwa ufupi juu ya clip ikionyesha wanajeshi katili wakiua raia

Maelezo kwa ufupi juu ya clip ikionyesha wanajeshi katili wakiua raia

Sasa western kwani hayo hawafanyi ?

Wakati Babu zako walikuwa wanachinjwa kama mbuzi sio hao hao western walikuwa wanafanya ?
Sasa huo wakati wa mababu zako ulikuwepo, uliona??
Ukiachana na hilo wale walikua kutoka huko ng'ambo mbali kabisa, hamfanani kwa chochote hata lugha na tamaduni tofauti.

Sasa hao wapuuzi wanachinjana wao kwa wao.
 
Hii clip iliniumiza, na sasa nimeumia zaidi kwa kufahamu kwamba waliouawa hawakuwa na hatia!

Amjad hastahili kuwa hai mpaka hivi sasa, na ingependeza zaidi endapo wangepatikana wote waliotekeleza ukatili huo katika clip.
Finally Assad kaachia ngazi ..
 
Ahaaa naona vita ni kali sana humu ndan

Ndugu zako nao akina kosugi maralia 2 wakakimbia jukwaa

Yahudi anangusha kipondo ni balaa

Nikakukumbuka nikasema walau ungekuwepo walau hekima zako zingefanya kitu
Mkuu, nimecheka sana, siku yangu imekwenda vyema 😁
 
Hii clip nimeiona kutoka kwenye uzi alioanzisha mdau anaitwa GoldDhahabu wenye kichwa cha habari Hawa wanajeshi katili ni wa wapi? .

View: https://streamable.com/ly7v6f

Kuna maelezo mengi tofauti na sehemu kubwa si sahihi.

Tukio linaonyesha raia ambao wamefungwa mikono na kuzibwa macho wakikokotwa na askari, pasipo raia hao kujua wanaelekea wapi au pengine wakifahamu wanaelekea mahala salama wanaangukia kwenye shimo lililoandaliwa tayari na kupigwa risasi vichwani, baada ya askari hao kumaliza kuwapiga risasi mmoja baada ya mwingine, askari hao wakiwa wameshatanguliza matairi ya gari kwenye shimo, wanawasha moto na kuteketeza miili hio.



Hili tukio lilitokea 16 April 2013 nchini Syria katika mji mkuu Damascus, askari wanao onekana kutekeleza unyama huo wanatokea kitengo cha intelijensia katika jeshi la Syria (Military Intelligence Directorate (Syria)), na specifically hao askari wapo katika kitengo kinachohusika na ukatili, utesaji na mauaji pasipo huruma. Yaani kwenye Syrian Military Intelligence kuna hiki kitengo kwa ajili ya utesaji, mauaji na ukatili wa kila aina unaoufahamu.

Syrian Military Intelligence ipo chini ya raisi, inaendeshwa na Bashar Al Assad mwenyewe, kitengo hiki kimekuwa kimetumika pia kwenye siasa hasa kuwakandamiza wale wanaotaka kuleta upinzani lazima cha moto utakiona.

Hii clip imevuja mwaka 2022, inasemekana kuna mtu alipata access ya laptop iliyokuwa na clip hii, akacopy na kuihifadhi, inasemekana ni askari wa Syria.
Aliyetambulika kwenye hii clip ni Major Amjad Yousef ambae anaonekana kuwapiga risasi raia hao pasipo huruma, askari huyu katili inasemekana amejiunga na jeshi mwaka 2004, baadae baada ya mafunzo akajiunga na branch 227 katika Syrian Intelligence Service kitengo maalumu kwa ajili ya utekaji, kutesa na kuua hasa wapinzani katika serikali ya Syria.

Kwa ufupi hao raia wanauliwa kikatili inasemekana hawana kosa, kilikuwa ni kipindi cha mapigano ambapo waasi walikuwa wanakaribia eneo hilo, hivyo askari hao walitaka kuonyesha mfano kwa yeyote ambae atajaribu kuwa upande wa uasi. Raia hao inasemekana waliishi karibu kabisa na eneo ambalo kulikuwa na upinzani.

Raia waliouawa wakati huo ni 41, waliouawa kwenye hilo shimo. Hata hivyo inasemekana waliouawa wengine ni wanakadiriwa 200 au 300 katika maeneo mengine

Baada ya clip kuvuja, Amjad alikamatwa na serikali ya Syria 2022, Amjad amekamatwa pasipo warrant na hajafikishwa mahakamani, wachambuzi wa mambo wanasema kukamatwa kwa Amjad ni kuzuia waliojihusisha na unyama huo waliopo ngazi za juu wasifahamike.

Serikali ya marekani ilitoa sanctions juu ya Amjad Yousef mnamo March mwaka huu 2023 , secreatry of state Anthony Blinken alisema vikwazo hivyo ni kwa ajili ya mauaji hayo yaliyofanyika.

Bora tu dikteta Assad kapinduliwa!
 
Sio vitu vigeni kwa uzao ishmael, uzao wa chuki, ulipaji visasi na mauaji
 
Demokrasia gani waliyo jitahidi marekani Assange tu mpaka leo anaishi kama digi digi.

Hao ulaya unyama walio fanyia babu na bibi zako ni kwamba umesahau au hujui historia ?

Unyama anao fanya marekani hapo middle east kwa kushirikiana na dikteta mwenzake Israel huoni ?

Mauaji ya Marekani Vietnam unayafahamu ?
Tanzania vs USA , je unaeza walingaisha ?
 
Back
Top Bottom