Maelezo kwa ufupi juu ya clip ikionyesha wanajeshi katili wakiua raia

Hii clip nimeiona kutoka kwenye uzi alioanzisha mdau anaitwa GoldDhahabu wenye kichwa cha habari Hawa wanajeshi katili ni wa wapi? .

View: https://streamable.com/ly7v6f

Kuna maelezo mengi tofauti na sehemu kubwa si sahihi.

Tukio linaonyesha raia ambao wamefungwa mikono na kuzibwa macho wakikokotwa na askari, pasipo raia hao kujua wanaelekea wapi au pengine wakifahamu wanaelekea mahala salama wanaangukia kwenye shimo lililoandaliwa tayari na kupigwa risasi vichwani, baada ya askari hao kumaliza kuwapiga risasi mmoja baada ya mwingine, askari hao wakiwa wameshatanguliza matairi ya gari kwenye shimo, wanawasha moto na kuteketeza miili hio.

Hili tukio lilitokea 16 April 2013 nchini Syria katika mji mkuu Damascus, askari wanao onekana kutekeleza unyama huo wanatokea kitengo cha intelijensia katika jeshi la Syria (Military Intelligence Directorate (Syria)), na specifically hao askari wapo katika kitengo kinachohusika na ukatili, utesaji na mauaji pasipo huruma. Yaani kwenye Syrian Military Intelligence kuna hiki kitengo kwa ajili ya utesaji, mauaji na ukatili wa kila aina unaoufahamu.

Syrian Military Intelligence ipo chini ya raisi, inaendeshwa na Bashar Al Assad mwenyewe, kitengo hiki kimekuwa kimetumika pia kwenye siasa hasa kuwakandamiza wale wanaotaka kuleta upinzani lazima cha moto utakiona.

Hii clip imevuja mwaka 2022, inasemekana kuna mtu alipata access ya laptop iliyokuwa na clip hii, akacopy na kuihifadhi, inasemekana ni askari wa Syria.
Aliyetambulika kwenye hii clip ni Major Amjad Yousef ambae anaonekana kuwapiga risasi raia hao pasipo huruma, askari huyu katili inasemekana amejiunga na jeshi mwaka 2004, baadae baada ya mafunzo akajiunga na branch 227 katika Syrian Intelligence Service kitengo maalumu kwa ajili ya utekaji, kutesa na kuua hasa wapinzani katika serikali ya Syria.

Kwa ufupi hao raia wanauliwa kikatili inasemekana hawana kosa, kilikuwa ni kipindi cha mapigano ambapo waasi walikuwa wanakaribia eneo hilo, hivyo askari hao walitaka kuonyesha mfano kwa yeyote ambae atajaribu kuwa upande wa uasi. Raia hao inasemekana waliishi karibu kabisa na eneo ambalo kulikuwa na upinzani.

Raia waliouawa wakati huo ni 41, waliouawa kwenye hilo shimo. Hata hivyo inasemekana waliouawa wengine ni wanakadiriwa 200 au 300 katika maeneo mengine

Baada ya clip kuvuja, Amjad alikamatwa na serikali ya Syria 2022, Amjad amekamatwa pasipo warrant na hajafikishwa mahakamani, wachambuzi wa mambo wanasema kukamatwa kwa Amjad ni kuzuia waliojihusisha na unyama huo waliopo ngazi za juu wasifahamike.

Serikali ya marekani ilitoa sanctions juu ya Amjad Yousef mnamo March mwaka huu 2023 , secreatry of state Anthony Blinken alisema vikwazo hivyo ni kwa ajili ya mauaji hayo yaliyofanyika.

Hali inatisha sana.
Lakini tusiwasikitikie sana watu hao, Huenda pengine hata Ben Saanane, Azory Gwanda na watu wengineo wengi waliotekwa na "watu wasiojulikana" waliteswa na kisha kuuawa kwa namna hii hii.
Utawala wa kiimla ni kitu kibaya sana tena ni hatari sana hapa duniani.
Ukisikia mauaji ya halaiki ndio haya.
 
Har
Hii clip nimeiona kutoka kwenye uzi alioanzisha mdau anaitwa GoldDhahabu wenye kichwa cha habari Hawa wanajeshi katili ni wa wapi? .

View: https://streamable.com/ly7v6f

Kuna maelezo mengi tofauti na sehemu kubwa si sahihi.

Tukio linaonyesha raia ambao wamefungwa mikono na kuzibwa macho wakikokotwa na askari, pasipo raia hao kujua wanaelekea wapi au pengine wakifahamu wanaelekea mahala salama wanaangukia kwenye shimo lililoandaliwa tayari na kupigwa risasi vichwani, baada ya askari hao kumaliza kuwapiga risasi mmoja baada ya mwingine, askari hao wakiwa wameshatanguliza matairi ya gari kwenye shimo, wanawasha moto na kuteketeza miili hio.

Hili tukio lilitokea 16 April 2013 nchini Syria katika mji mkuu Damascus, askari wanao onekana kutekeleza unyama huo wanatokea kitengo cha intelijensia katika jeshi la Syria (Military Intelligence Directorate (Syria)), na specifically hao askari wapo katika kitengo kinachohusika na ukatili, utesaji na mauaji pasipo huruma. Yaani kwenye Syrian Military Intelligence kuna hiki kitengo kwa ajili ya utesaji, mauaji na ukatili wa kila aina unaoufahamu.

Syrian Military Intelligence ipo chini ya raisi, inaendeshwa na Bashar Al Assad mwenyewe, kitengo hiki kimekuwa kimetumika pia kwenye siasa hasa kuwakandamiza wale wanaotaka kuleta upinzani lazima cha moto utakiona.

Hii clip imevuja mwaka 2022, inasemekana kuna mtu alipata access ya laptop iliyokuwa na clip hii, akacopy na kuihifadhi, inasemekana ni askari wa Syria.
Aliyetambulika kwenye hii clip ni Major Amjad Yousef ambae anaonekana kuwapiga risasi raia hao pasipo huruma, askari huyu katili inasemekana amejiunga na jeshi mwaka 2004, baadae baada ya mafunzo akajiunga na branch 227 katika Syrian Intelligence Service kitengo maalumu kwa ajili ya utekaji, kutesa na kuua hasa wapinzani katika serikali ya Syria.

Kwa ufupi hao raia wanauliwa kikatili inasemekana hawana kosa, kilikuwa ni kipindi cha mapigano ambapo waasi walikuwa wanakaribia eneo hilo, hivyo askari hao walitaka kuonyesha mfano kwa yeyote ambae atajaribu kuwa upande wa uasi. Raia hao inasemekana waliishi karibu kabisa na eneo ambalo kulikuwa na upinzani.

Raia waliouawa wakati huo ni 41, waliouawa kwenye hilo shimo. Hata hivyo inasemekana waliouawa wengine ni wanakadiriwa 200 au 300 katika maeneo mengine

Baada ya clip kuvuja, Amjad alikamatwa na serikali ya Syria 2022, Amjad amekamatwa pasipo warrant na hajafikishwa mahakamani, wachambuzi wa mambo wanasema kukamatwa kwa Amjad ni kuzuia waliojihusisha na unyama huo waliopo ngazi za juu wasifahamike.

Serikali ya marekani ilitoa sanctions juu ya Amjad Yousef mnamo March mwaka huu 2023 , secreatry of state Anthony Blinken alisema vikwazo hivyo ni kwa ajili ya mauaji hayo yaliyofanyika.

Harafu kuna mtu ananiambia Nijiunge na jeshi?? Over My dead body.

Majeshi ya Duniani yanatumikia Wanasiasa kwa masilahi ya wanasiasa.

Wao wanaambulia Mabulungutu ya Pesa na Starehe tu.
 
Nimeangalia hadi mwisho ila imeniumiza.. haswa anapowaachia waone kama wanaweza kutembea kuendelea mbele then wanaanguka na paap..

Mola ndie atahukumu wa kuhukumiwa, na hivi wanajiweka juu ya wengine maishani.
Mambo yenu hayo inapofika uchaguzi roho huwa zinakuwa kama za hao wanajeshi😆😆
 
Ndo muache kushabikia vita,

Yanayofanyika vitani mengi Huwa hayaripotiwi.

Mungu tuepushe.
 
Hivi hawa washkaji wana familia kweli huko nyumbani yaani watoto au mke aseee !! Watu huwa wanasema kufanya kazi mochwari ni kipengele ila hii kazi ni ya moto asee naona bora hata anayenyonga wafungwa ana nafuu ! Hii kazi hata ukiiacha lazima upate Post Traumatic Disorder.

Hiki kitengo hata kwetu hapa kipo kweli ?
Ni almost 90% ya nchi zote duniani wanavyo sema vipo na vina fanya kazi kwa siri sana
 
Harafu kuna mtu ananiambia Nijiunge na jeshi?? Over My dead body.

Majeshi ya Duniani yanatumikia Wanasiasa kwa masilahi ya wanasiasa.

Wao wanaambulia Mabulungutu ya Pesa na Starehe tu.
Siyo Majeshi yote hapa duniani yanajihusisha na Uovu mbaya kama huo. Mambo kama haya mara nyingi yanafanyika kwenye nchi ambazo kuna tawala za kidikteta, tawalala zisizostaarabika zinazofuata hasa Siasa za Mrengo wa Ujamaa au Ukomunusti.
Ni nadra sana kukuta mambo kama haya yakifanyika kwenye nchi zenye tawala za Kidemokrasia, tawala zilizostaarabika ambako kuna Mifumo Imara kabisa ya Utawala wa Sheria na Utawala Bora ktk Mfumo wa uendeshaji wa shughuli za Serikali, huwezi kukuta mambo kama haya.
 
Nimesema serikali nyingi mkuu, hususani kwenye hizi serikali za dictatorship.
Udikiteta hauwezi kudumu hata miezi sita bila kufanya mauaji kama hayo.

Kwa kuwa Udikteta haukubaliki sehemu.yoyote duniani kwa hiyo njia pekee ya kuufanua uwepo madarakani ni kwa Kuua, kuteka, na kutesa.

Waliotekwa wote na serikali za namna hii hata wakiachiwa huwa hawasimulii kilichotokea.

That is complete soul damage kwa kadhia na gadhabu unazokutana nazo huko matesoni.

USA Navy Seal wana kitengo cha ku train watesaji na snippers.

Kile kitengo kinafundisha aina mbali mbali za utesaji.

Wanajeshi aliyesajiliwa kitengoni hapo anafundishwa na kubadilishwa nafsi step by step hadi roho yake inakuwa kama ya shetani na pengine zaidi ya shetani.

Taarifa zinasema unabadilishwa nafsi hypinotization kiasi kwamba Mwanakitengo akiambiwa Piga huyo Kisu cha tumbo anapiga tu bila kuuliza Why na hana huruma hata asilimia 1.

Ulimwengu huu unatisha sana nashangaa kwanini Mungu ameuacha uwe hivi.
 
Nimeangalia hadi mwisho ila imeniumiza.. haswa anapowaachia waone kama wanaweza kutembea kuendelea mbele then wanaanguka na paap..

Mola ndie atahukumu wa kuhukumiwa, na hivi wanajiweka juu ya wengine maishani.
Alafu wengi hapo waliyouliwa ni wapalestina refugee

Ova
 
Cha ajabu ni kwamba kuna watu fulani walianza kumfuatilia Amjad ambae ni huyo muuaji, wakamfuatilia hadi wakagundua alikuwa anatumia mtandao wa kijamii, wakamuuliza kile amefanya anajisikiaje, jamaa akasema anajivunia na hajutii alichofanya. Baadae akapotea kabisa kwenye social media baada ya kugundua amefahamika, na akatoa vitisho. Baada ya clip kuvuja akakamatwa.

Kuna watu ni katili aisee.
Huyu wakimkamata wamkate vipande vidogo vidogo shz type

Ova
 
Dunia inaongozwa na wahalifu walio vaa suti . Kuingia tu madarakani kila mbinu ovu watu wana tumia sembuse sembuse kuua watu ndio liwe jambo la ajabu kwao ?
Kweli.....ukiona tu mtu anavyoingia madarakani kwa uovu mwingi....you can easily predict what is going to happen in future.
 
Hivi hawa washkaji wana familia kweli huko nyumbani yaani watoto au mke aseee !! Watu huwa wanasema kufanya kazi mochwari ni kipengele ila hii kazi ni ya moto asee naona bora hata anayenyonga wafungwa ana nafuu ! Hii kazi hata ukiiacha lazima upate Post Traumatic Disorder.

Hiki kitengo hata kwetu hapa kipo kweli ?
Vitengo kama hivi hapa kwetu vipo ndiyo. "Watu Wasiojulikana" kazi zao nyingi za kila siku ni kama hizi unazoziona kwenye video hii. Ndio maana wengi wao ( kama siyo wote) hawapendi wajulikane kwenye jamii kwamba wanafanya kazi kama hii. Hao watu unaosikia kwamba wametekwa na "watu wasiojulikana" au maiti zimeokotwa kwenye viroba, wahanga wa matukio hayo wamekuwa wakifanywa kama hivi unavyoona kwenye video hii.
 
Kweli.....ukiona tu mtu anavyoingia madarakani kwa uovu mwingi....you can easily predict what is going to happen in future.
Mitawala ya Afrika ni mijitu ya ajabu sana. Ina akili za kishetani na kiqumer kuliko wanyama wa porini. Mungu atakuja kuyahukumu vibaya kama alivyoyahukumu madikteta mengine kama Bokasa na Idi Amin dada
 
Back
Top Bottom