Maelezo kwa ufupi juu ya clip ikionyesha wanajeshi katili wakiua raia

Maelezo kwa ufupi juu ya clip ikionyesha wanajeshi katili wakiua raia

Hakuna nchi yenye hizo taka taka democracy na free speech kama propaganda ulizo lishwa na vyombo vyao vya habari nawe ukaaamini.

Futa mawazo ya free speech dunia hii ya kibepari, bepari hana huruma na anaye fichua maovu yake.
Huwezi linganisha uhuru wa kuongea uliopo US na North Korea, hapo napo utabisha.
 
Halafu kuna watu wanadiss western countries.
Kudadeki hakuna kitu sipendi kama kuuana bila hatia.
Kwangu ni mara 100 huo ushoga wanaoupromote western ila sio kuuana kama kuku.
Kuzikana kama mnyama aliekufa kwa ugonjwa, sote nchi moja, race moja lakini unaua na kumchoma moto, Really!!?
Sasa western kwani hayo hawafanyi ?

Wakati Babu zako walikuwa wanachinjwa kama mbuzi sio hao hao western walikuwa wanafanya ?
 
Hii clip nimeiona kutoka kwenye uzi alioanzisha mdau anaitwa GoldDhahabu wenye kichwa cha habari Hawa wanajeshi katili ni wa wapi? .

View: https://streamable.com/ly7v6f

Kuna maelezo mengi tofauti na sehemu kubwa si sahihi.

Tukio linaonyesha raia ambao wamefungwa mikono na kuzibwa macho wakikokotwa na askari, pasipo raia hao kujua wanaelekea wapi au pengine wakifahamu wanaelekea mahala salama wanaangukia kwenye shimo lililoandaliwa tayari na kupigwa risasi vichwani, baada ya askari hao kumaliza kuwapiga risasi mmoja baada ya mwingine, askari hao wakiwa wameshatanguliza matairi ya gari kwenye shimo, wanawasha moto na kuteketeza miili hio.



Hili tukio lilitokea 16 April 2013 nchini Syria katika mji mkuu Damascus, askari wanao onekana kutekeleza unyama huo wanatokea kitengo cha intelijensia katika jeshi la Syria (Military Intelligence Directorate (Syria)), na specifically hao askari wapo katika kitengo kinachohusika na ukatili, utesaji na mauaji pasipo huruma. Yaani kwenye Syrian Military Intelligence kuna hiki kitengo kwa ajili ya utesaji, mauaji na ukatili wa kila aina unaoufahamu.

Syrian Military Intelligence ipo chini ya raisi, inaendeshwa na Bashar Al Assad mwenyewe, kitengo hiki kimekuwa kimetumika pia kwenye siasa hasa kuwakandamiza wale wanaotaka kuleta upinzani lazima cha moto utakiona.

Hii clip imevuja mwaka 2022, inasemekana kuna mtu alipata access ya laptop iliyokuwa na clip hii, akacopy na kuihifadhi, inasemekana ni askari wa Syria.
Aliyetambulika kwenye hii clip ni Major Amjad Yousef ambae anaonekana kuwapiga risasi raia hao pasipo huruma, askari huyu katili inasemekana amejiunga na jeshi mwaka 2004, baadae baada ya mafunzo akajiunga na branch 227 katika Syrian Intelligence Service kitengo maalumu kwa ajili ya utekaji, kutesa na kuua hasa wapinzani katika serikali ya Syria.

Kwa ufupi hao raia wanauliwa kikatili inasemekana hawana kosa, kilikuwa ni kipindi cha mapigano ambapo waasi walikuwa wanakaribia eneo hilo, hivyo askari hao walitaka kuonyesha mfano kwa yeyote ambae atajaribu kuwa upande wa uasi. Raia hao inasemekana waliishi karibu kabisa na eneo ambalo kulikuwa na upinzani.

Raia waliouawa wakati huo ni 41, waliouawa kwenye hilo shimo. Hata hivyo inasemekana waliouawa wengine ni wanakadiriwa 200 au 300 katika maeneo mengine

Baada ya clip kuvuja, Amjad alikamatwa na serikali ya Syria 2022, Amjad amekamatwa pasipo warrant na hajafikishwa mahakamani, wachambuzi wa mambo wanasema kukamatwa kwa Amjad ni kuzuia waliojihusisha na unyama huo waliopo ngazi za juu wasifahamike.

Serikali ya marekani ilitoa sanctions juu ya Amjad Yousef mnamo March mwaka huu 2023 , secreatry of state Anthony Blinken alisema vikwazo hivyo ni kwa ajili ya mauaji hayo yaliyofanyika.

Hii dunia ina unafiki mwingi. Kosa inategemea kalifanya nani.
Marekani hujifanya baba wa kulinda haki lakini akivunja haki yeye au washikaji zake huwa anafumba macho.
Kosa kubwa alilofanya Assange wa Wikileaks ni kuvujisha documents na video za askari wa Kimarekani wakiua raia wasiokuwa na hatia jambo ambalo liliweka wazi uovu mkubwa wa jeshi la Marekani.
Mojawapo ya video ni ile ambayo helcopter ya kimaremani ikishambulia msafara wa harusi na kuua watu na hata baada ya kujua wameua watu wasio na hatia, askari wa kimarekani alisikika akisema these mother fuckers...
Sio video hiyo tu, bado kuna video nyingi ziliomywsha askari wakiua na kudhalilisha wanawake.
Lakini baada ya hizo video kuvuja serikali ya Marekani badala kudeal na askari wake, ilimtamgaza Assange kama mhaini na kuandaa mikakati ya kumkamata.
Hakuna hatua zozote zilizochukuluwa dhidi ya hao askari wake na hata kipindi cha Trump, mahakama ya kimataifa ilipotaka kuchunguza makosa ya kivita ya askari wa Marekani, Marekani ilikataa na kuwatishia maafisa wa mahakama hiyo kuwawekea vikwazo.
Dunia si uwanja wa haki kabisa.
 
Dini no kitu kibaya sana!!

Imani siasa dini madaraka.

So sad!

Ni Bora ccm itawale TU tuwe na amani kuliko wavuruge mambo tuingie huko!

Hai wanaokufa walizaliwa baada ya miezi Tisa tumboni Kuna wanafamilia wanawategemea!!
Hasta hapa Bongo hatujui ni wangapi waliokufa gizani bila kamera kunasa matukio kisa!siasa,imani dini!

Siasa ni imani,Dini,madaraka n.k imani zimeua wengi sana!!
 
Dini no kitu kibaya sana!!

Imani siasa dini madaraka.

So sad!

Ni Bora ccm itawale TU tuwe na amani kuliko wavuruge mambo tuingie huko!

Hai wanaokufa walizaliwa baada ya miezi Tisa tumboni Kuna wanafamilia wanawategemea!!
Hasta hapa Bongo hatujui ni wangapi waliokufa gizani bila kamera kunasa matukio kisa!siasa,imani dini!

Siasa ni imani,Dini,madaraka n.k imani zimeua wengi sana!!
Una amani gani sasa wewe hapa bongo ? Unafikiri kuwa tahira na kondoo la CCM la kukubali kila kitu cha kipumbavu ndio amani au ushenzi ? Pumbavu
 
Hii dunia hakuna watu wa hovyo kama waarabu, huwa hawaelewi wanataka nn!
 
Hii clip iliniumiza, na sasa nimeumia zaidi kwa kufahamu kwamba waliouawa hawakuwa na hatia!

Amjad hastahili kuwa hai mpaka hivi sasa, na ingependeza zaidi endapo wangepatikana wote waliotekeleza ukatili huo katika clip.
Maumivu hayo ndio wanayoyapata mnaowazushia ushoga na ufiraji humu JF kwa kutumia fake ID. Nao wana mioyo ya nyama, pia wana ndugu na jamaa wanaowaamini na kuwafuatilia. Acheni kudharirisha watu.😁😆😀
 
Hivi hawa washkaji wana familia kweli huko nyumbani yaani watoto au mke aseee !! Watu huwa wanasema kufanya kazi mochwari ni kipengele ila hii kazi ni ya moto asee naona bora hata anayenyonga wafungwa ana nafuu ! Hii kazi hata ukiiacha lazima upate Post Traumatic Disorder.

Hiki kitengo hata kwetu hapa kipo kweli ?
Ungemuuliza Ben angekuambia. Duniani tunapita, haina maana ya kufanyiana ubaya. Sasa yupo wapi Jiwe? Atakuwa amekutana na Ben Sasa anamuuliza kuhusu Damu yake aliyoimwaga. Wanadamu tunajisahau Sana tukiwa na madaraka na uhai ila kuna siku ya kukutanika njia panda na siku ya hukumu ya Mungu.

Siku hiyo watu wataona aibu na kulia kilio cha hatari tokana na vitu vya hovyo wafanyavyo.
 
Maumivu hayo ndio wanayoyapata mnaowazushia ushoga na ufiraji humu JF kwa kutumia fake ID. Nao wana mioyo ya nyama, pia wana ndugu na jamaa wanaowaamini na kuwafuatilia. Acheni kudharirisha watu.😁😆😀
Nakujibu tu kwa staha... tumia akili.
Unataka kufananisha udaku na watu wanaouawa kikatili? Uko timamu kweli?
 
Nakujibu tu kwa staha... tumia akili.
Unataka kufananisha udaku na watu wanaouawa kikatili? Uko timamu kweli?
We hata ukitukana ni sawa ila Maumivu ni yale yale. Kwa nchi za kiafrika bora uuliwe kuliko kusingiziwa u shoga. Fedheha kubwa sana katika jamii. Ebu badilikeni sister. Hamtendei haki wenzenu.
 
Ungemuuliza Ben angekuambia. Duniani tunapita, haina maana ya kufanyiana ubaya. Sasa yupo wapi Jiwe? Atakuwa amekutana na Ben Sasa anamuuliza kuhusu Damu yake aliyoimwaga. Wanadamu tunajisahau Sana tukiwa na madaraka na uhai ila kuna siku ya kukutanika njia panda na siku ya hukumu ya Mungu.

Siku hiyo watu wataona aibu na kulia kilio cha hatari tokana na vitu vya hovyo wafanyavyo.
Ndo iwe kweli hicho tunachokiwaza kuhusu maisha baada ya kifo kiwe kweli na hakimu awepo kweli , isiwe mtu ukifa na biashara imeishia hapo !!
 
Ndo iwe kweli hicho tunachokiwaza kuhusu maisha baada ya kifo kiwe kweli na hakimu awepo kweli , isiwe mtu ukifa na biashara imeishia hapo !!
Kwa muda wangu wa kuishi Duniani, sina mashaka wala wasiwasi wa uwepo wa siku ya Hukumu na maisha baada ya kifo. Sasa mna potoshwa na kudanganywa na yule muovu na mawakala wake ili muamini hakuna hiko kitu. Ile siku ipo bro, ile jioni ipo kaka na ni dhahiri kabisa.
 
huu ni zaidi ya unyama ila huu ukatili unaendana na aliofanyiwa mtanzania mwezetu mollel inasikitisha sana
 
Back
Top Bottom