Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Nimesoma maelezo ya msichana aliekuwa nae alipouwawa, yana ukakasi sana. Kuna coincidence ambazo labda ni polisi wetu tu waliozoea kutunga kesi dhidi ya wapizani wataikubali.
Inaripotiwa kuwa huyu UVCCM, mwenye biashara ya kuchoma chama klabu moja, alipigiwa simu kuwa kuna mbuzi wanauzwa aende kukutana na wauzaji
Halafu hiyo namba iliyopiga simu kusema njoo ununue mbuzi polisi wakomae nayo. Na pia waangalie kama hiyo namba imewahi kuwasiliana na namba ya huyo msichana. Unaweza kukuta kabla au baada tu ya kupiga simu kusema njoo tuna mbuzi, waliwasiliana na huyu msichana
Na polisi waelewe kwamba inawezekana wauaji walimfuata huyu bwana nyuma, sio kwamba walikuwa wamejificha mahali. Kama ni mpango uliosukwa na msichana anahusika anaweza kuwa anadanganya kwamba walivamiwa na watu waliokuwa pale, akijua wazi wauaji walikuwa nyuma yao na waliwalazimisha kusimama, na anawajua. Simu ya msichana ichunguzwe, namba alizopiga na kupigiwa zichunguzwe, na zilinganishwe na namba alizopigiwa kijana alieuawa
Polisi acheni kuwa na akili ya kesi za kutunga za Chadema tu, fanyeni kazi za kipolisi kama hizi kwa umakini mkijua kuwa maisha ya huyo msichana yanaweza kuwa hatarini. Mshawishini aeleze ukweli kama namna ya kujilinda dhidi ya kupotezewa asije akatoa siri

- Aliamua kwenda kwa wauzaji na pikipiki yake akifuatana na huyu msichama - kwa nini? Na nani alipendekeza waende na huyo msichana? Je lilikuwa ni wazo la huyo msichana? Na je, huyo msichana ndio alisuka mpango watu wapige hiyo simu?
- Wakiwa njiani sehemu yenye pori huyo kijana alisikia kukojoa akapaki pikipiki ajisaidie ndio wakavamiwa - hapa ndio kuna coincidence ya ajabu. Kwamba out of the blue sehemu unapoamua kukojoa porini ndio kuna watu wanaouua wanakuwepo by coincidence. Inakubalika? Haya ni maelezo ya msichana na yanatia shaka sana. Ninaamini aliesema simama nikojoe ni huyo msichana, na alijua wapi atamwambia huyu kijana simama nikojoe kwa sababu alijua wapi hao wauaji wanasubiri. Na hao wauaji walikuwa wamevaa soksi za uso. Kwa nini? Itakuwa ni watu wanaofahamiana nao.
- Anasema yeye wauaji walimwachia baada ya kumfunga na akajifungua. Hii inatia shaka sana.