Maelezo ya alivyouawa mwenyekiti wa UVCCM huko Chunya yana ukakaksi sana, Polisi fanyeni kazi yenu kwa umakini

Maelezo ya alivyouawa mwenyekiti wa UVCCM huko Chunya yana ukakaksi sana, Polisi fanyeni kazi yenu kwa umakini

N
Nimesoma maelezo ya msichana aliekuwa nae alipouwawa, yana ukakasi sana. Kuna coincidence ambazo labda ni polisi wetu tu waliozoea kutunga kesi dhidi ya wapizani wataikubali.

Inaripotiwa kuwa huyu UVCCM, mwenye biashara ya kuchoma chama klabu moja, alipigiwa simu kuwa kuna mbuzi wanauzwa aende kukutana na wauzaji
  1. Aliamua kwenda kwa wauzaji na pikipiki yake akifuatana na huyu msichama - kwa nini? Na nani alipendekeza waende na huyo msichana? Je lilikuwa ni wazo la huyo msichana? Na je, huyo msichana ndio alisuka mpango watu wapige hiyo simu?
  2. Wakiwa njiani sehemu yenye pori huyo kijana alisikia kukojoa akapaki pikipiki ajisaidie ndio wakavamiwa - hapa ndio kuna coincidence ya ajabu. Kwamba out of the blue sehemu unapoamua kukojoa porini ndio kuna watu wanaouua wanakuwepo by coincidence. Inakubalika? Haya ni maelezo ya msichana na yanatia shaka sana. Ninaamini aliesema simama nikojoe ni huyo msichana, na alijua wapi atamwambia huyu kijana simama nikojoe kwa sababu alijua wapi hao wauaji wanasubiri. Na hao wauaji walikuwa wamevaa soksi za uso. Kwa nini? Itakuwa ni watu wanaofahamiana nao.
  3. Anasema yeye wauaji walimwachia baada ya kumfunga na akajifungua. Hii inatia shaka sana.
Kuna kila dalili kuwa huyu msichana anahusika. Polisi wakomae nae. Huenda ni hela za kununua mbuzi zimemponza huyu kijana. Mauaji haya hayahusiani kabisa na suala la utekaji linaloendelea wala siasa. CCM wasije wakathubutu hata kusema mbona watu wetu nao wanauwawa kama wapinzani wanavyouawa.

Halafu hiyo namba iliyopiga simu kusema njoo ununue mbuzi polisi wakomae nayo. Na pia waangalie kama hiyo namba imewahi kuwasiliana na namba ya huyo msichana. Unaweza kukuta kabla au baada tu ya kupiga simu kusema njoo tuna mbuzi, waliwasiliana na huyu msichana

Na polisi waelewe kwamba inawezekana wauaji walimfuata huyu bwana nyuma, sio kwamba walikuwa wamejificha mahali. Kama ni mpango uliosukwa na msichana anahusika anaweza kuwa anadanganya kwamba walivamiwa na watu waliokuwa pale, akijua wazi wauaji walikuwa nyuma yao na waliwalazimisha kusimama, na anawajua. Simu ya msichana ichunguzwe, namba alizopiga na kupiguiwa zichunguzwe, na zilinganishwe na namba alizopigiwa kijana alieuawa

Polisi acheni kuwa na akili ya kesi za kutunga za Chadema tu, fanyeni kazi za kipolisi kama hizi kwa umakini mkijua kuwa maisha ya huyo msichana yanaweza kuwa hatarini. Mshawishini aeleze ukweli kama namna ya kujilinda dhidi ya kupotezewa asije akatoa siri
Nimejaribu kufuatilia mabandiko yako mengine hujasema kabisa kuwa kibao na wengine wenye matukiio sawa na huyo acha u ccm kwenye maisha ya watu
 
Kwani taarifa za kifo cha Mzee Kibao zimeshatoka?

Au tupige kimya kwa hitimisho - kifo ni kifo.
 
Kuna kila dalili kuwa huyu msichana anahusika. Polisi wakomae nae. Huenda ni hela za kununua mbuzi zimemponza huyu kijana. Mauaji haya hayahusiani kabisa na suala la utekaji linaloendelea wala siasa. CCM wasije wakathubutu hata kusema mbona watu wetu nao wanauwawa kama wapinzani wanavyouawa.
Hii inafanana sana na ya wale waliokuwa wanawatumia wanawake kwenda kukodi bodaboda ili kufika mbele ya safari wawaue na kuwapora pikipiki
 
N

Nimejaribu kufuatilia mabandiko yako mengine hujasema kabisa kuwa kibao na wengine wenye matukiio sawa na huyo acha u ccm kwenye maisha ya watu
Sijakuelewa, ila nachoweza kukuambia ni kwamba mie nachukia utekaji wa watu bila kujali ni wa Chadema au ACT au CCM. Kama umeangalia post zangu utaona nawaponda polisi kwenye mambo ya utekaji na uuaji, na mtu anaweza kuhisi mie ni mpinzani. Si hivyo. Ni kwa kuwa tu wengi wanaotekwa ni watu wa upinzani. Sasa hapa kauawa mtu wa CCM. Sintashangilia bali nitawaonya Polisi wasifanye uzembe kwa kuwa wamezoea kufanya hivyo.

Kwangu kifo si kifo tu, bali mwanadamu ni mwanadamu
 
Hii inafanana sana na ya wale waliokuwa wanawatumia wanawake kwenda kukodi bodaboda ili kufika mbele ya safari wawaue na kuwapora pikipiki
Hili nalo jambo kubwa Mkuu. Sijasikia wakisema kama pikipiki ilichukuliwa au ilipatikana!
 
Wanatuhitaji ili wabadilike,
Binafsi Nina marafiki huko, wengi wamejaa manung'uniko ,wanafanya wasiyotaka kuyafanya, viapo vinawabana!
Usimwamini sana mtu anaesema nakula nyasi kwa sababu nalazimishwa. Kama ingekuwa wanasema kweli kipigo wanachotembeza kwa wananchi, kwa mfano wakiandamana, kingekuwa sio cha kuua mtu, na hata usingeona jeshi la Polisi mara zote likilalamikiwa kutumia nguvu kupita kiasi. Ungeona wakizuia watu kiungwana. Ingekuwa picha za victims wa Police Tanzania bado zinawekwa Google na kwingine ningekuonyesha hapa uniambie kuwa hao victims waliumizwa hivyo na watu wanaofanya wasiyotaka kuyafanya, hao rafiki zako.

Polisi wetu ni wanyama wabaya kuliko fisi wa mwituni. Kuna mwanamke alitumiwa video clip ya mumewe FFU akipiga mtu, alidai talaka! Alisema hawazii siku mume wake akiamua kumpiga itakuwaje kila akifikiria ile video. Na kosa la mtu huyo aliepigwa ilikuwa kuandamana tu.
 
Mleta mada umekuwa shallow kufanya scientific analysis, badala yake umemalizia kwa kuonesha chuki na dhihaka dhidi ya issues za mauji ya wafuasi wa CHADEMA.

Ulitakiwa kwanza ujue huyo msijana ni nani, je alikuwa na mahusiano gani na marehemu hadi waondoke wote, na isiwe mtu mwingine jinsia nyingine, na ukizingatia kuwa ulikuwa ni usiku, je km ulikuwa mchepuko wake! Wewe ulitakiwa uwe na maswali mengi juu ya huyo mdada siyo kwa nini marehemu alishikwa mkojo au mdada alijifunguaj.

Mwisho, acha kuhusisha tukio lililotokea na matokio mengine kwa kuona kuwa hili ndo lakufuatiliwa ila hayo mengine ni drama.
 
Najua ufupi wa akili yako. Niliposema CCM wasije wakadai Chadema wanahusika unatoa povu! Chuki ipi umeiona dhidi ya issue za mauaji ya wafuasi wa Chadema, uko sawa wewe?

Kwanza ulivyo shallow wa shule, scientific analysis inaingiaje hapa? Unajua maana ya scientific analysis? Nikufundishe shule kidogo? Hapa tunaongelea feasible scenarios.
 
IMG_2333.jpeg
 
Umeona eeh? Sasa hebu nishawishi kwamba kwenye hii dili huyu msichana hakuwamo! Simama nikojoe, kumbe ndio kifo chako.

Na sasa utajua Polisi wanafanya makusudi kutowakamata watekaji na wauaji wa wafuasi wa vyama vya upinzani, eidha kwa kuwa wao ndio wahusika kwa maelekezo toka juu, au wakijua ni mission ya watu wa kitengo. Uwezo wa kukamata hawa watu wanao,ila wanajitoa akili kwa sababu ya chama tawala

Na onyo kwa bodaboda na hata dereva, hata siku moja usiambiwe na kukumbali kuelekezwa wapi usimame ili mtu aliekukodo au umempa lift afanye kitu. Iwe kuchimba dawa, iwe kununua sijui nini nk. Mpleke sehemu nyingine sio usimame pale anapokuelekeza.
 
Najua ufupi wa akili yako. Niliposema CCM wasije wakadai Chadema wanahusika unatoa povu! Chuki ipi umeiona dhidi ya issue za mauaji ya wafuasi wa Chadema, uko sawa wewe?

Kwanza ulivyo shallow wa shule, scientific analysis inaingiaje hapa? Unajua maana ya scientific analysis? Nikufundishe shule kidogo? Hapa tunaongelea feasible scenarios.
Ha ha ha ha siku zote mtu asie na hoja hutoa vihoja. Hivi wewe kwa akili yako unadhani umesoma kunizidi au unaelewa kuliko mimi. Pole sn, mimi siyo mtu wa kuropka. Nikupe pole tu kuwa unaongea usichokijua na kujifanya mjuaji. Ungesoma majib yangu kwako, ungeona wapi hatukwenda sawa na wapi tumeenda sawa. Huwa sina muda wa kubishana na mtu kwenye mitandao, siyo wa type hiyo hata kidogo. Wewe endelea upate medali. Mimi nilijibu kutokana na nukuu yako hii "Polisi acheni kuwa na akili ya kesi za kutunga za Chadema tu, fanyeni kazi za kipolisi'. Pengine hapa ndo sikukuelewa na wewe hukunielewa ukanidhania vibaya.
 
Ha ha ha ha siku zote mtu asie na hoja hutoa vihoja. Hivi wewe kwa akili yako unadhani umesoma kunizidi au unaelewa kuliko mimi. Pole sana
Mtu yeyote ambae anasema unadhani umesoma kunizidi wakati hajui nimesoma kwa kiwango gani ni wazi hajasoma na anaonyesha dalili zote za kutokuwa na akili ya kufikiria mambo.
When you have one known value x, and one unknown value y, you can never assert x > y unless you are a damn idiot!
 
Back
Top Bottom