Maelezo ya kina kuhusu Uber. Usafiri salama na wa bei ya chini kwa mtanzania

Habari wanaJamiiforums, baada ya kuona watu wanasambaza tricks za uongo kuhusu usafiri wa Uber nimeshawishika kuelezea kwa kina kuhusu usafiri huu.

Uber ni nini?
Uber ni application inayokuwezesha kupata usafiri wa bei ya chini na salama katika sehemu nyingi za mkoa wa Dar-es-Salaam, kwa kupitia simu yako ya mkononi. Usafiri huu ni wa kutumia magari madogo yanayoweza kubeba kuanzia mtu mmoja hadi watu wanne.

Kujisajili na Uber
Nenda playstore, search 'Uber' utaiona ina icon nyeusi, download kisha ifungue.
Fanya usajili kwa kutumia namba yako ya simu, email na pia utachagua neno la siri.

Kupata punguzo la Tsh6200 katika trip yako ya kwanza
  • Nenda Menu kwa kubonyeza mistari mitatu iliyoko juu kushoto,Kisha bonyezaPayments,kisha bonyeza Add promo code , andika tzaba17
  • Utaona maandishi ya kijani yakionyesha kwamba utapata punguzo la tsh6200 katika trip yako ya kwanza.
  • Nitatoa mfano, safari yako ya kwanzi ni kutoka posta hadi magomeni,na gharama yake ni shilingi 7200,basi utalipa sh1000 tu kutokana na hilo punguzo,lakini katika safari ya pili utalipa nauli kamili.

Zingatia

Unaweza kujisajili mara moja tu kwa kutumia hiyo promotion code, ukirudia kujisajili kwa namba nyingine kama baadhi ya watu wanavyopotosha mitandaoni, akaunti yako ya uber itafungiwa na hutaweza tena kutumia huduma za uber

Jinsi ya kutumia Uber kuita usafiri.
  • Fungua app ya Uber, hakikisha umewasha GPS, itakuletea maandishi 'where to'.Hapo utajaza unapotaka kwenda,mfano 'Magomeni Mapipa'.
  • Itakuonyesha kiasi cha nauli inayokadiriwa, na utabonyeza 'Request uberX'
  • Hapo hapo,itakuonyesha jina na namba ya gari la dereva atakayekufata hapo hapo ulipo, na ndani ya dk5 atakuwa kashafika.
Malipo ya usafiri
  • Ukifika 'destination' yako dereva atabonyeza 'Stop trip' kwenye application iliyoko kwenye simu yake, na hapo hapo itaonyesha nauli kwenye simu yako na kwenye simu ya dereva
  • Unaweza kulipa kwa Cash(Taslimu) au kwa kutuma Kadi ya benki
Umuhimu wa kutumia Uber
  • Ni gharama nafuu zaidi ukilinganisha na taxi za kawaida, kwa sababu bei inahesabiwa na mashine yenyewe kulingana na umbali wa sehemu unayoenda, na sio derevaa kujipangia bei kubwa
  • Ni salama zaidi, hasahasa usiku, kwasababu dereva wa uber anakuwa amesajiliwa na endapo itatokea tatizo lolote mfano kusahau kitu kwenye gari, dereva anaweza kupatikana kwa haraka
  • Inakusaidia kuokoa muda; mfano upo sehemu ambapo hamna taxi,bajaji wala bodaboda, unaweza kuita usafiri na ukakufata hapohapo kwa kutumia app hii.
Nakaribisha maswali yoyote kuhusiana na huduma hii ya UBER
Je kama safari ya kwanza inagharimu elfu 5 hivi halafu nina hiyo promotion ina maana sitalipia chochote?
 
Yootee ya nn nna namba ya Dereva tax wanguu na boder boder huo wooote ni mlolongooo...
 
maelezo mazuri lakini rekebisha kua promo code si lazima iwe hyo ulioweka kwa kufanya hvo tunakupa na ww offer kua muwazi vinginevo ni kama unatumia ka trick kupata offers
 
umewaza mbali mkuu tena kwa punguzo la 6200 kwenye nauli ya 5000 unatakiwa upewe 1200 taslimu na dereva
Promotion code inafanya kazi kwenye safari moja tu, ile ya kwanza. Hivyo hata kama nauli ni 5000; 1200 itakayobaki hutarudishiwa na haitatumika kwenye safari zinazofuata
 
maelezo mazuri lakini rekebisha kua promo code si lazima iwe hyo ulioweka kwa kufanya hvo tunakupa na ww offer kua muwazi vinginevo ni kama unatumia ka trick kupata offers
Ni kweli kabisa mkuu unaweza kutumia promotion code nyingine,ila ukitumia promotion code nyingine utapata punguzo dogo zaidi la sh 4500 badala ya 6200
 
Asante kwa maelezo mazuri.nina swali kuhusu usalama wa dereva au mmiliki wa Taxi.mteja akiniita usiku lakini akawa ana mipango yake mibaya ya kuniteka na kuiba gari.usalama umekaaje hapo na pili kama nataka kuliingiza gari langu kwenye hii biashara ya UBER inakuwaje.kama nina gari na nina dereva
 
Kuhusu usalama wako;
Mkuu ili mteja atumie usafiri wa Uber lazima awe amejisajili kwa kutumia namba yake ya Simu, hivyo ni vigumu mtu kufanya uhalifu akijua namba yake ya simu imesajiliwa. Vilevile uber wana taarifa mbalimbali kama IMEI namba ya simu husika, hii inaweza kusaidia kumtrace mteja anapofanya uhalifu kama kuiba gari la dereva wa uber.

Kuhusu kujiunga na Uber kama una gari na dereva; hii unaweza ukafika ofisi za Uber, Viva towers Posta, ukapata maelezo zaidi
 
uber ni the best kwakweli madriver tax ni vichefuchefu wanakuangalia kwanza umevaaje unaenda wapi ndo anakupa bei
JITAHIDI MUWEKE BANGO KUBWA LA UBER UBUNGO TERMINAL
AIRPORT NA POSTA HATA KARIAKOO
 
Uber iko freshi, na magari karibia yote ya Uber niliyopanda yapo katika hali nzuri sana full kiyoyozi yani
 
Back
Top Bottom