Maelfu wamchangia Mbowe katika kampeni ya #MwambaTuvushe ya kumrejesha madarakani CHADEMA

Molemo

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
14,620
Reaction score
13,361
Vijana wa Chadema Mkoa wa Dar es Salaam wameanzisha kampeni kubwa ya kutaka Freeman Mbowe achukue fomu kwa mara nyingine ya kugombea Uenyekiti CHADEMA.

Kampeni hiyo yenye kauli mbiu #MwambaTuvushe imeungwa mkono na maelfu ya watu ambao wanachanga pesa zao kwa kiwango cha kuanzia mia tano ili kutimiza shilingi milioni 1 ya kuchukulia fomu ya uenyekiti.

Vijana hao wa CHADEMA wameapa kumchukulia fomu na kuzijaza kisha kwenda kumlazimisha kiongozi huyo kuzitia sahihi na baada ya hapo wazirejeshe.

Vijana hao wameamua kuanza kampeni hiyo kabambe baada ya Tetesi kuvuma kwamba Mwenyekiti huyo wa CHADEMA ameamua kutogombea tena nafasi hiyo.

Wafuasi hao wa CHADEMA wametishia kukesha nyumbani kwa Mwenyekiti huyo na kumzuia kwenda popote mpaka atakapokubali kusaini fomu hizo za kugombea Uenyekiti.

Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr Vincent Mashinji alipuliza rasmi kipenga cha uchaguzi mkuu juzi na kutangaza uchaguzi mkuu wa kumpata Mwenyekiti mpya wa chama hicho utakuwa December 18.

=====
Michango ya wadau

 
Ni jambo jema, lakini huyu ndugu ameumizwa sana na utawala kisa tu ni hicho cheo. Natamani angepumzika kupisha mwingine lakini huyu aliyetangaza nia nahisi harufu ya kijani. Hakuna jinsi, SISIEM waendelee kulala na viatu sharti Mbowe awe mwenyekiti, tena napendekeza hadi hapo atakapoona hawezi hata kutembea.
 
Hata mimi niko tayar! Mbowe amenifunza mengi sana kwenye maisha kupitia ukomavu wake kwenye siasa. ANASTAHILI HESHIMA KUBWA SANA,URAIS,UBUNGE WALA UWENYEKITI HAVIMTOSHI KUMPA HESHIMA ANAYOSTAHILI. MBOWE UNASTAHILI HESHIMA TUU MBINGU NA ARDHI VINAFAHAMU HILI HUJAVIKANYAGA BURE.
 
Hao vijana hawafai kupewa nchi, wao na chama chao
 
Watu Wana hofu na Mbowe... Mbona vyeo Ni majukumu mazito? Au Mbowe Ni kikwazo kwa wapinzani wake?...
 
Huu ni ubabe umetumika

Mbowe apunguze udkteta

Kwanini achangishe Wakati yeye ni bilionea?
2019 Imeisha

-Soko la Korosho limeharibiwa -Ajira Sekta rasmi na sekta binafsi zimeshuka

-Hali ngumu ya Maisha Maradufu

-Uchaguzi Serikali za Mitaa Umeharibiwa

-Kuna Hatari kutokea Janga la Njaa Kanda ya Kati

-Katiba Inavunjwa na kubakwa Mchana wa Jua Kali

Hiyo ndiyo 2019
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…