Maelfu wamchangia Mbowe katika kampeni ya #MwambaTuvushe ya kumrejesha madarakani CHADEMA

Maelfu wamchangia Mbowe katika kampeni ya #MwambaTuvushe ya kumrejesha madarakani CHADEMA

John Heche ndo dawa ya mtu fulani apewe wenyekiti
 
Huu ni ubabe umetumika

Mbowe apunguze udkteta

Kwanini achangishe Wakati yeye ni bilionea?
Dah! Una moyo mgumu kama wa kenge! Unapigwa vijembe kuhusu tabia yako ya kudandia kila hoja kwa kuchomeka maneno hata yasiyohusiana lakini wapi! Haukomi, lazima unakasoro maungoni na sio ya kuzaliwa nayo bali umesababishiwa!
 
Kama watamzuia kutoka nyumbani aombe tu msaada kwa polisi. Watatoka wenyewe na hawatamsumbua tena kama kweli hataki.
Hawamzuii kwa mabaya bali kwa imani waliyo nayo juu yake, iweje atumie polisi kupambana na watu wema?
 
Hata mie mwanachama wa CCMlwa miaka mingi sana, hata chadema haijazaliwa, wakinikubalia, nitachangia.

Ukweli ni kuwa kwa sasa hakuna anayeweza kukivusha chama kwa busara, zaidi yake.

Japokuwa anayo madosari mengi, but he is truly needed now.
Huu ni ubabe umetumika

Mbowe apunguze udkteta

Kwanini achangishe Wakati yeye ni bilionea?
 
Mbowe, mmoja kati ya 'principled leaders' tulionao sasa hivi Tanzania, lakini kaumizwa sana yeye kama kiongozi wa upinzani. Laiti hawa vijana wanaochangishana wangeonyesha moyo huo huo wa kuwa karibu na kiongozi wao wakati alipokuwa akiumizwa, pengine majaribu anayopitia sasa hivi yasingekuwa yanamkabili.

Ameharibiwa biashara, maksudi kabisa, mashamba na kubambikiwa kesi mbaya. Kawekwa ndani miezi kadhaa..., na kujionea uhalisia wa upweke unaoweza kumpata kiongozi. Katambua kwamba kuwa kiongozi unachukua dhamana ya watu unaowaongoza; lakini bila shaka hakujua kwamba watu hao hao wanaoonyesha mapenzi kwa kiongozi wao wakati wa raha, wanaweza kugeuka na kusahau kabisa kiongozi huyo anapopatwa na masaibu kutokana na juhudi za uongozi wake. Kiongozi anasahaulika na kutelekezwa. Bila shaka hili linamuuma sana hata kama hasemi.

Sasa anakabiliwa na kesi ya kupikwa, na pengine yeye kama kiongozi makini wa chama amekwishajua mitego iliyotegwa ili kukimaliza chama moja kwa moja.

Je, itasaidia kitu gani yeye kuchaguliwa kuendelea kuwa kiongozi wa chama kama amekwishaandaliwa kutokuwepo kwenye uwanja wa siasa? Huu ni udadisi, lakini hatuwezi kutotambua uwezekano wake.

Hao vijana wanaochangishana, wanaweza wakasema potelea mbali, bado wanataka kiongozi aongoze bila kujali yaliyopangwa na wenye mabavu. Kama hivyo ndivyo, basi wasiishie kuchangishana tu. Wawe tayari kusimama na kiongozi wao katika raha na katika majaribu yote yaliyoandaliwa juu yake. Hili litamtia nguvu yeye ya kuendelea kukitumikia chama akijua, kujitoa kwake kunatambuliwa na kuheshimiwa na anaowaongoza.
 
Upuuzi wa Tz bana!!

Upinzani Tanzania bado saaaaaaaana.
 
Kama wewe sio mkono wa mh.Mbowe nakupa pole sana.

Umetumia nguvu nyingi kuandika aina ya hekima.


ILA NAKUPA TAARIFA MH.MBOWE SIO MPINZANI KAMA WANYONGE WANAVYOZANI.

Washauri wanyonge watafute mtetezi mpya ambaye hana Chembechembe na CCM.
Kalamu1,
 
Siasa za Tanzania ati mtu lazima ionekane kaombwa ama kalazimushwa!!!
 
Mimi binafsi namshauri Mhe. Mbowe achukue fomu ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti. Mhe. Mbowe ni mtu jasiri sana na ameitetea sana CHADEMA pale panapohitajika.
 
Masikini Lumumba wamenunaje, Ikulu nako wanafyonya tu.. haaa haaa mhe,Mbowe ndio habari kwa sasa.
#MWAMBA TUVUSHE🙏🏾
 
Sio muda muafaka Mbowe kuendelea kugombea uwenyekiti wa cdm. Ni vyema akampisha mtu mwingine ili demokrasia ishamiri ndani ya chama. Miaka 15 tosha sana.
 
Natamani wagombea uenyekiti chadema wawe hata 40.mwisho Wa Siku kura zitaamua.Ila kwa nin wasimchukulie lissu?
 
ILA NAKUPA TAARIFA MH.MBOWE SIO MPINZANI KAMA WANYONGE WANAVYOZANI.

Washauri wanyonge watafute mtetezi mpya ambaye hana Chembechembe na CCM.
Michango kama hii haisaidii lolote.

Eleza unayoyajua kuhusu "Mh. Mbowe kutokuwa Mpinzani," na nitakusoma na kupima hayo unayoona kuwa yanamfanya kutokuwa mpinzani.
Vinginevyo, nakupuuza kabisa na kukuona kutokuwa tofauti na wapiga majungu wengine.
 
Back
Top Bottom