Nimeona manowari za jeshi la US zikiwa zimesheni ndege vita za kutosha. Siku ambayo US atakua mkweli, akasema Israel iheshimu mipaka, walowezi waondoke maeneo yasiyo ya kwao la sivyo hakuna support, kwa vyovyote Israel hataweza. Pamoja na shida za Hamas, mgogoro huu unachangiwa na mataifa ya Magharibi. Israel peke yake HANA UBAVU, ni jambo lililo wazi. Kujua hilo MOSSAD walikua wapi wakati HAMAS anapenya kwa magendo? Kwa hiyo roure cause ya huu mgogoro ni kupuuzia mipaka ya mataifa hayo mawili ambayo kihistoria ni ndugu kabisa.
Jambo moja ambalo wakristo wengi wanaingiza udini lakini hawalijui labda kwa makusudi au kutofuatilia ni kuwa;
1. Israel Waarabu ni asilimia karibu 20 hivi wakati Wayahudi ni asilimia 73. Dini zingine au race zingine ni asilimia 6 tu.
2. Wayahudi hawamtambui Yesu kabisa na siyo katika mleta dini kwao ingawa ni uzao wao kabisa. Wao Mussa ndiyo kila kitu
3.Wapalestina maana yake siyo Waislam bali ni Waislam na Wakristo.