Maelfu ya mateka ya majeshi ya Ethiopia yalitekwa na Tigray Defense forces yafikishwa mji mkuu wa Tigray

Maelfu ya mateka ya majeshi ya Ethiopia yalitekwa na Tigray Defense forces yafikishwa mji mkuu wa Tigray

Kuweka mambo sawa kidogo,

TPLF ni chama cha kisiasa nchini Ethiopia kilichochaguliwa na wananchi wa tigray kuongoza jimbo hilo

TDF ni jeshi la jimbo la tigray

TPLF wanaweza kuwa waasi kwa serikali kuu ya Ethiopia ila sio waasi wakutokea porini kama ilivyozoeleka ni Jeshi kamili lenye mgawanyiko wa vikosi sawa na TPDF hapa bongo maana wana Jeshi la anga, ardhi na hata navy kama sikosei japo hawana bahari, wana bajeti ya jeshi lao kama sisi tu, majenerali wa rank zote

Ethiopia haikushindwa vita na tigray ilivunja ngome ya TDF na kuchukua mji mkuu Makelle kwa muda usiozidi miezi miwili

Ethiopia ilishindwa kuongoza mji huo kwa sababu ya nidhamu mbovu ya wanajeshi ya Ethiopia, Ethiopia ilishindwa kuwaelekeza wana Tigray kuwa tatizo sio kabila lao bali tatizo viongozi na Ideology mbaya ya TPLF,

Wanajeshi waliishia kubaka, kuiba mabank na mali za watu hivyo kupoteza mvuto machoni mwa wana Tigray, kuuwa watu kwa makundi hasa vijana wanao hisiwa ni TDF, kushindwa kuruhusu huduma za kibinadamu licha ya kuumiliki mji kwa karibu miezi6 umeme, maji, mtandao hawakurudisha

Kifupi Ethiopia iliondoa majeshi yake yenyewe mjini Makele kwa sababu ilikosa support ya watu (wana tigray) hivyo kuogopa kuendelea kuvunja sheria za kimataifa na haki za kibinadamu na sio hofu ya TDF ambayo ilikuwa imeshajifia
 
Basi kwa hali ilivo utawala wa waziri mkuu wa Ethiopia Ahmed Abiay utakua na mwisho mbaya au hata miaka miwili ijayo atakua keshatolewa.
Sioni hili likitokea kijeshi.
Hawa wazee wa Tigray watachemsha kwa sababu ya kukosa supply. Moja ya vitu vimewapa nguvu ni cache kubwa ya silaha ambayo ilikuwa pale wakati wa vita ya Ethiopia na Eritrea.

Hawa jamaa haziwaki na Eritrea. So hawawezi tumia border yao kama supply line. Pia Sudan wana matatizo yao, very unlikely watataka mgogoro zaidi na Ethiopia kwa kuruhusu wawe supply line ya TPLF.

Kwa maana hiyo ni suala la muda tu kabla ya jamaa kulazimika kuweka silaha chini. Mbinu pekee itakayoweza angalau kufua dafu nikuleta silaha kwa mgongo wa humanitarian aid. Hii Ethiopia wakiidhibiti ni game over.

Jamaa wanapigana vita waliyopoteza ukiangalia kwa darubini! Nadhani ndio maana hata PM wao hatetemeki. Akishinda kisiasa tu kwenye uchaguzi atakuwa na kazi moja ya kuhakikisha wanakuwa vizuri na Sudan na mchezo unaishia hapo. Kumbuka alihusika sana na amani ya Sudan post Bashir!
 
Kuweka mambo sawa kidogo,

TPLF ni chama cha kisiasa nchini Ethiopia kilichochaguliwa na wananchi wa tigray kuongoza jimbo hilo

TDF ni jeshi la jimbo la tigray

TPLF wanaweza kuwa waasi kwa serikali kuu ya Ethiopia ila sio waasi wakutokea porini kama ilivyozoeleka ni Jeshi kamili lenye mgawanyiko wa vikosi sawa na TPDF hapa bongo maana wana Jeshi la anga, ardhi na hata navy kama sikosei japo hawana bahari, wana bajeti ya jeshi lao kama sisi tu, majenerali wa rank zote

Ethiopia haikushindwa vita na tigray ilivunja ngome ya TDF na kuchukua mji mkuu Makelle kwa muda usiozidi miezi miwili

Ethiopia ilishindwa kuongoza mji huo kwa sababu ya nidhamu mbovu ya wanajeshi ya Ethiopia, Ethiopia ilishindwa kuwaelekeza wana Tigray kuwa tatizo sio kabila lao bali tatizo viongozi na Ideology mbaya ya TPLF,

Wanajeshi waliishia kubaka, kuiba mabank na mali za watu hivyo kupoteza mvuto machoni mwa wana Tigray, kuuwa watu kwa makundi hasa vijana wanao hisiwa ni TDF, kushindwa kuruhusu huduma za kibinadamu licha ya kuumiliki mji kwa karibu miezi6 umeme, maji, mtandao hawakurudisha

Kifupi Ethiopia iliondoa majeshi yake yenyewe mjini Makele kwa sababu ilikosa support ya watu (wana tigray) hivyo kuogopa kuendelea kuvunja sheria za kimataifa na haki za kibinadamu na sio hofu ya TDF ambayo ilikuwa imeshajifia
Dawa ya hili ni kupata kiomgozi mzuri ambaye ataijenga tena Tigray na kuwaleta watu pamoja waTigray bila swaga za kudai uhuru. Yaani atasimamia maslahi yao kwa muktadha wa shirikisho. Hapa ndio mtihani kwa Abiy na serikali yake. Akifanikiwa hili kamaliza vita. Japo akipatikana TPLF watataka kumuua ili mgawanyiko uendelee.
 
Ethiopia hana ubavu wa kusimama na Egypt
hawafanani kabisaaaa
Hawa ni very unlikely kupigana. Kumbuka Tigray ni sehemu ya Ethiopia hivyo mashambulizi yalilenga ku assert authority ya Federal government kuliko kuua na kufanya uharibifu. Vita na taifa jingine i.e Misri itakuwa ni kusababisha maximum infliction in shortest time possible. Hii ni game nyingine kabisa.

Halafu haya mataifa yana washirika pia ambao watatoa support iwe ya wazi au kimya kimya.

Wote wanalijua hili na uzuri PM Abiy na Rais Al Sis wote ni wajeda na wanajua maana ya vita, acha hii ya keyboard 🤣
 
... inaanza kunipa shaka uwezo wa Ethiopia kijeshi; kama wanamgambo wa Tigray wanawatoa jasho kiasi hiki ndio watapambana na Egypt kugombea maji ya Blue Nile "roho" ya Egypt? Ethiopia wajipange kweli kweli kama wanataka kulinda legacy ya haki ya kutumia maji ya Blue Nile bila "kuingiliwa" na foreign powers.
Ethiopia issue ya Tigray waliitengeza kuwaingiza maboya mahasimu wao na kupunguza joto la ujenzi wa bwawa lao.
 
Hv Waafrika ni uzao wa nani? Kinachoendelea ni laana tupu. Kila mmoja na rafiki zake anataka waingie madarakani, waliopo wanakwiba, hawawajali wenzao na hawako tayari kushirikisha wengine, SHIDAAAH
 
Hizi nchi za kimaskini ni shida tupu.
Kinachogombewa haswaa ni nini?
Kuna haja gani kuwepo kwa vita nchini Ethiopia?
Kwanini wasikae chini tu na kukubaliana ili mambo yaishe, ili watu wao wapone, pesa za kupigana vita ziende kwenye maendeleo na wajenge nchi yao?
Umeongea point!
Angalia Sudan Kusini, ubinafsi na umimi!
Kuna watu wana uchu na madaraka, ili watukuzwe, wafisadi wala hawawazii maendeleo. Innocent people wanakufa.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Dawa ya hili ni kupata kiomgozi mzuri ambaye ataijenga tena Tigray na kuwaleta watu pamoja waTigray bila swaga za kudai uhuru. Yaani atasimamia maslahi yao kwa muktadha wa shirikisho. Hapa ndio mtihani kwa Abiy na serikali yake. Akifanikiwa hili kamaliza vita. Japo akipatikana TPLF watataka kumuua ili mgawanyiko uendelee.
Binafsi siioni Tigrey ikiendelea kuwa sehemu ya Ethiopia tena,

-Kitendo cha Abiy kupiga deal na maraisi wa nchi hasimu kihistoria (Elitrea na Somalia) kuunda mbinu za pamoja kuivamia Tigray (kuingiza foreign power kuthibiti migogoro ya ndani) kulimaliza kabisa uhusiano wa kindugu baina yao,

-Kitendo cha Abiy kutaka kuitudishia Elitrea miji ya mpakani mwa Tigrey na Elitrea ili tu kupata umaharufu duniani, ikumbukwe TPLF ndio walipigana vita kuichukua hiyo miji ambayo ni yao kiasili leo hii mtu hausiki nayo kuirudisha ki makaratasi tu kisa ilikuwa upande wa Italia kipindi cha ukoloni ni jambo la aibu kwa nchi kubwa kama Ethiopia

Stage itakayo fuata sasaivi ni kukubaliana mipaka mipya baina ya Ethiopia na Tigray, hii ndio sababu TPLF hawataki kuweka silaha chini kwa sasa sababu maeneo yao mengi ya mipakani bado yamekaliwa na serikali, mfano Sudan, Elitrea na Ethiopia upande wa south

Pia siioni Tigrey ikikubalika kama nchi hadi miaka 15-20 mbele, itakuwa kama Somaliland tu kwamba mnajiita nchi ila hatambuliki na duniani/UN, uzuri utakuwa na urafiki na baadhi ya nchi na watafungua embassy zao mfano Kenya wana embassy huko Somaliland
 
Inakuwaje WanaJF!

Tigray defense forces ni nouma. Serikali ya Ethiopia inaminya uhuru wa habari kuficha kinachoendelea Tigray lakini mkong'oto wanaoupokea huko ni wa Hatari. Hii imetokea jana. Hao ni washenajeshi wa Ethiopia walioshikwa mateka wakiwa paraded Mekelle mji mkuu wa Tigray
View attachment 1839522

mng'ato Jumbe Brown
Hivi Hawa ni mgambo au wajeshi?

Yaani hii nchi nimeidharau hatari,nchi kama hizi hazina stable politics zinapataje wawekezaji ?
 
Hizi video ndo ziliifanya serikali Addis Abeba ishtuke nakuchukua hatua haraka sana. Yani hawa wanaume wangefanikiwa kuchukua silaha sasa hivi Tigray ingekuwa nchi kamili. Na Tigray ingekuwa nchi kamili Oromia nao wangetaka taifa lao pia Amhara kwa iyo Ahmed Abiy ilibidi tu kuwa bomb marafiki zake wa muda mrefu kunusuru Ethiopia kuzidi kugawanyika. View attachment 1839251

dudus mng'ato
Hiyo Nchi kuna siku watagawana fito kwa staili hii
 
TDF , Tigray Defence Force , msisahau watigray ndio jamii ya watu ethiopia wanaojiita first class people kwa ufupi hao ndio wenye wasomi wengi na kwenye serikali kuu ndio wenye position nyingi lakini pia ndio watu walioshika uchumi yaani wanawafanyabiashara wakubwa na wenye ushawishi mkubwa pale ethiopia, hata mkurugenzi wa WHO nae ni mtigray hivo jamaa msiwachukulie poa
Wapumbavu tuu sijui hayo makabila zinashindwa nini kuwa nchi moja?
 
Kuweka mambo sawa kidogo,

TPLF ni chama cha kisiasa nchini Ethiopia kilichochaguliwa na wananchi wa tigray kuongoza jimbo hilo

TDF ni jeshi la jimbo la tigray

TPLF wanaweza kuwa waasi kwa serikali kuu ya Ethiopia ila sio waasi wakutokea porini kama ilivyozoeleka ni Jeshi kamili lenye mgawanyiko wa vikosi sawa na TPDF hapa bongo maana wana Jeshi la anga, ardhi na hata navy kama sikosei japo hawana bahari, wana bajeti ya jeshi lao kama sisi tu, majenerali wa rank zote

Ethiopia haikushindwa vita na tigray ilivunja ngome ya TDF na kuchukua mji mkuu Makelle kwa muda usiozidi miezi miwili

Ethiopia ilishindwa kuongoza mji huo kwa sababu ya nidhamu mbovu ya wanajeshi ya Ethiopia, Ethiopia ilishindwa kuwaelekeza wana Tigray kuwa tatizo sio kabila lao bali tatizo viongozi na Ideology mbaya ya TPLF,

Wanajeshi waliishia kubaka, kuiba mabank na mali za watu hivyo kupoteza mvuto machoni mwa wana Tigray, kuuwa watu kwa makundi hasa vijana wanao hisiwa ni TDF, kushindwa kuruhusu huduma za kibinadamu licha ya kuumiliki mji kwa karibu miezi6 umeme, maji, mtandao hawakurudisha

Kifupi Ethiopia iliondoa majeshi yake yenyewe mjini Makele kwa sababu ilikosa support ya watu (wana tigray) hivyo kuogopa kuendelea kuvunja sheria za kimataifa na haki za kibinadamu na sio hofu ya TDF ambayo ilikuwa imeshajifia
Tunajuaje hao ndo wanajeshi wa Ethiopia? Kwangu mimi Ethiopia ndo wanajeshi bora kuliko yote Africa
 
Back
Top Bottom