Huu mfano wako wa Burundi hauendani na kinachoendelea pale.....
Mfano unaokaribiana ni huu, chukulia Zanzibar leo wajiondoe kwenye muungano wenu, tena kwa kura nyingi za Wazenji ambao wapige kura ya kujiondoa.
Hao Zanzibar huko ni mkusanyiko wa makabila ya Watanganyika, maana huko kuna Wanyamwezi, Wazaramo n.k. Hivyo wana undugu kabisa na Watanganyika, ni kwamba tu kuna historia iliyohusu Mwarabu kuwagawa .
Sasa baada ya Zanzibar kujitenga na kuwa nchi kivyao, rais wa Tanganyika aanze chokochoko za kutaka kurejesha muungano walioukataa na ambao kuna Watanganyika wengi hawautaki pia, atume wanajeshi kufanya uvamizi na mauaji huko ambapo askari Mnyamwezi anakwenda kumuua Mnyamwezi mwenzake kule kisa vitu vya kipuzi.
Leo Mrusi anaacha ardhi yote ya Urusi, taifa kubwa duniani, mapori yote hayo anakwenda kujisumbua akili na kataifa kama Ukraine.
Tembelea mitandao kama Quora uone Warusi walivyochukia na wanatukana sana, hata waliokua wafuasi kindakindaki wa Putin.