Maelfu ya Warusi waanza kujitokeza na kuandamana kupinga kinachofanyika dhidi ya ndugu zao Ukraine

Maelfu ya Warusi waanza kujitokeza na kuandamana kupinga kinachofanyika dhidi ya ndugu zao Ukraine

Maelfu wapi Media za west wanajaribu kufanya kama kuna maelfu ya watu wakati ni kawaida tu kutokea vikundi vidogo kupinga kama huku wako watu watapinga tu haijalishi ni nini sera zao pinga kila kitu. Huu mziki mkubwa hauzimwi na vikaratasi barabarani. Hao CNN sijui BBC wanajitahidi kupaka rangi watu waamini lakini wapi ngoma imefika mji mkuu wa Ukraine.
Wananchi wa kawaida hawataki vita kwa haina faida kwao zaidi ya hasara. Maisha baada vita yasikie tu
 
Ifahamike Ukraine na Urusi ni watu wamoja, na lugha inayotumika sana Ukraine ni Kirusi, maelfu ya Warusi hawaungi mkono huu uvamizi dhidi ya ndugu zao, ukiingia kwenye mitandao ya kijamii wengi wanatukana sana maana hawaelewi nini sababu za mauaji yanayoendelea au tija yake kwa Urusi, pia kuna taarifa baadhi ya wanajeshi wa Urusi wamenza kujisalimisha Ukraine na kugoma kuendelea kuua ndugu zao bila kuelewa nini sababu kuu.

Putin kwenye hili kachemsha, ingekua vita dhidi ya watu wa tabaka tofauti, Warusi wengi wangemuelewa, lakini hapa ni mauaji kwa ndugu zao kabisa wanaochangia vinasaba, na hakutumia muda wake vizuri kuwaelewesha ulazima au umuhimu wa mauaji haya, kakurupuka tu na kutuma majeshi yaanze uvamizi.

Huu uvamizi umesababisha Warusi wengi walio ugenini waishi kwa aibu ya kutojitambulisha popote utaifa wao.

https://www.news10.com/news/ukraini...sian-platoon-surrendered-to-ukrainian-forces/

Uko very biased
 
Wananchi wa kawaida hawataki vita kwa haina faida kwao zaidi ya hasara. Maisha baada vita yasikie tu
Hakuna mtu anaomba vita sio jambo zuri kwa nchi yoyote lakini vita kama hii haikuwa ya lazima ila chokochoko za hawa hawa wanaojitapa kuongoza kwa amani ndio wanaleta mabalaa. ukitizama nchi zenye ma dikteta utakuwa wametulia ila usiwaingilie 18 zao hawa wengine wanataka kila mtu aishi kama wao.
 
Uko very biased

Biased kivipi, Ukraine ni taifa ambalo lilikua limetulia wakiwa wanajifanyia mambo yao na hawajamchokoza Urusi au hata kufadhili magaidi wala hata kujihusisha kwenye maugomvi ya kimataifa, leo unawakuta na kuwashushia mabomu....

fb_img_1645859801058-jpg.2131766
 
Kwa libya ilikuaje? Huko congo hao ngozi za nguruwe wanafanyaga nini? Kila mtu abebe msalaba wake
 
Biased kivipi, Ukraine ni taifa ambalo lilikua limetulia wakiwa wanajifanyia mambo yao na hawajamchokoza Urusi au hata kufadhili magaidi wala hata kujihusisha kwenye maugomvi ya kimataifa, leo unawakuta na kuwashushia mabomu....

fb_img_1645859801058-jpg.2131766
LIBYA IRAQ SYRIA waliteseka zaidi ya hv acha nawao waonje utamu wa vita
.hpa nashangaa kwanini hawa UK GERMAN nawengine hawaingilii huu mtanange ili wakapta kuonja ladha ya vita nawao kama wenziwao
 
LIBYA IRAQ SYRIA waliteseka zaidi ya hv acha nawao waonje utamu wa vita
.hpa nashangaa kwanini hawa UK GERMAN nawengine hawaingilii huu mtanange ili wakapta kuonja ladha ya vita nawao kama wenziwao

Hao uliowataja walikua na sifa za kufadhili yale makundi yenu ya kufia dini, ndio maana hata wakipigwa dunia ikapiga kimya.

Lakini huyu Ukraine hajishughulishi na mtu, yuko busy kwenye mambo yake halafu anashushiwa mabomu kisa hataki kujiunga kwenye muungano wa lazima wa USSR.
Leo hii wavaa makobazi mnashabikia Mrusi huyo huyo aliyewachinja wenzenu Chechnya.
 
Walikua wanafadhili makundi ya ugaidi eeehhh...
So watoto walokua wanauliwa na mabomu middle east nao walikua wanafadhili magaidi???
USA ni war criminal ka criminals wengine sema media zao ndio zinawasaidia kudanganya watu ka wewe mnaoamini kirahis rahisi...
Iraq walisema ana atomic bombs wakamuua sadam je waliyaona hayo mabomu walosema???
Au ndio mambo ya ukitaka kumdhuru mbwa mpe jina baya eeehhh...
 
Huu mfano wako wa Burundi hauendani na kinachoendelea pale.....
Mfano unaokaribiana ni huu, chukulia Zanzibar leo wajiondoe kwenye muungano wenu, tena kwa kura nyingi za Wazenji ambao wapige kura ya kujiondoa.
Hao Zanzibar huko ni mkusanyiko wa makabila ya Watanganyika, maana huko kuna Wanyamwezi, Wazaramo n.k. Hivyo wana undugu kabisa na Watanganyika, ni kwamba tu kuna historia iliyohusu Mwarabu kuwagawa .

Sasa baada ya Zanzibar kujitenga na kuwa nchi kivyao, rais wa Tanganyika aanze chokochoko za kutaka kurejesha muungano walioukataa na ambao kuna Watanganyika wengi hawautaki pia, atume wanajeshi kufanya uvamizi na mauaji huko ambapo askari Mnyamwezi anakwenda kumuua Mnyamwezi mwenzake kule kisa vitu vya kipuzi.
Leo Mrusi anaacha ardhi yote ya Urusi, taifa kubwa duniani, mapori yote hayo anakwenda kujisumbua akili na kataifa kama Ukraine.

Tembelea mitandao kama Quora uone Warusi walivyochukia na wanatukana sana, hata waliokua wafuasi kindakindaki wa Putin.
Umeelezea sababu inayokufurahisha wewe lakini Mrusi lengo lake ni usalama tu. Kwa Urusi USA na NATO ni maadui. So Ukraine kujiunga na NATO na kuruhusu kuwekwa Kwa kituo Cha kijeshi Cha NATO mpakani mwake anakichukulia kama ni hatari Kwa usalama wa nchi yake. Hiyo sababu nyingine ya kurudisha Soviet Union inaweza ikawa hidden agenda
 
Sababu unaitoa ndio sio kabisa, maana Ukraine na Urusi waliachika kwenye muungano wao, kila mmoja akachukua hamsini zake, hivyo wote hakuna anayetakiwa kumpangia mwenzke nani wa kuungana naye, Urusi akitaka aungane na Korea Kaskazini, China n.k. Huku Ukraine naye akiingia kwenye miungano yake.
Ukishaachika kwenye ndoa usimpangie mkeo nani wa kumuoa huko anakokwenda.
 
Back
Top Bottom