Rais Magufuli bado anatosha sana! Ila akubali kupokea ushauri kutoka kwa watu makini.
Akibadili mtazamo kuhusu Sera zake za Uchumi na kuruhusu Sekta Binafsi kuendesha uchumi.
Akizingatia Utawala wa Sheria (Rule of Law ) na akakubali pia kukosolewa.
Akikubali kukuza Demokrasia na kuzuia mambo haya ya hovyo ya kutekana na kuuana hovyo.
Akajitenga na wapambe nuksi wanaosaka Ugali kwa kivuli cha kumsifia na kumuabudu !
Basi Mhe.Rais Magufuli atakuwa na ata sasa ni Rais Bora kuliko anavyoweza kuwa Ndg.Bernard Kamillius Membe.
Nguvu kubwa (undisputed power ) ambayo Mhe.Rais Dr.Magufuli anayo kuliko akina Mhe. Membe ni hii ya kuamini kuwa maendeleo ya Watanzania yako mikononi mwa Watanzania na kwamba Tanzania ni Nchi Tajiri sana!
Hawa kina Mhe.Bernard Kamillius Membe walitudhalilisha sana na uombaomba na kuabudu Wazungu!
Kama ni Mhe.Membe ni bora mara 1000 kwa Taifa hili Mhe. Rais Magufuli aendelee tu kutuongoza na " udikteta" wake.
Watakao- survive wataona kitu huko mbele kuliko huu ("u- softness, u- diaspora, kuzurura duniani, uombaomba ) wa akina Mhe. Bernard Kamillius Membe.