SoC03 Maendeleo/ Furaha yako ni zao la unaotumia nao muda mwingi. Yajue haya na uchukue hatua

SoC03 Maendeleo/ Furaha yako ni zao la unaotumia nao muda mwingi. Yajue haya na uchukue hatua

Stories of Change - 2023 Competition

Infinite_Kiumeni

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2023
Posts
382
Reaction score
687
Haijalishi unajishawishi kichwani kiasi gani kwamba we ni wa tofauti.
Haijalishi unajiona we ni wa tofauti na unaotumia nao muda mwingi.
Lazima mwisho wa siku uwe kama wao, kama unavoendelea kuwa nao.
Sababu binadamu tumeumbwa kufanana na watu wetu wa karibu.
Ndo mana utasikia familia ile ipo hivi, au ukoo huu upo vile.

Ukijitenga kidogo tu utaanza kusemwa na utaonekana we ndo mkosi mpya kwenye familia/ ukoo au kwa marafiki zako.
Watakusema vibaya mpaka we mwenyewe utaamua kurudi ili kuepusha maneno, dharau au kejeli.

Usipuuze madhara ya, maneno mabovu (ya kukurudisha nyuma/ kukufanya ujione mjinga), kejeli, uchafu, kutokua na maadili, umasikini, ulalamishi, kutokua na mipango, kutokua na shukrani, ubaya, uchawi, kutokua na malengo na uzembe kutoka kwa watu unaotumia nao muda mwingi.

Hata ukisema hauwezi ukawa hivyo, huwezi ukakwepa wakati bado upo nao. Lazima ushawishi wao utakuzidi. Kumbuka we sio malaika. Ni binadamu na umeumbiwa kuendana na wanaokuzunguka muda mwingi.

Kama watu hawakusaidii kwenye kutimiza malengo yako ujue fika ya kuwa wanakurudisha nyuma kwenye malengo yako.

Japo unaweza usilione haraka haraka, lakini kadri muda unavyozidi kwenda utajihisi uchovu bila sababu, machungu, na woga kupita kiasi.
Sababu umejitenga mbali na maendeleo uliyokua unatamani na sasa roho inakusuta.

Dunaini hakuna kitu kama ambacho kipo kipo tu. Kuna vitu viwili tu, aitha kuna maendeleo au kuna kurudi nyuma. Hakuna kwamba upo sehemu moja utakaa apo milele. Narudia, aitha unaendelea katika malengo yako au unapotea na kurudi nyuma.
Unaposema upo upo tu ujue unajipooza tu kuliko kusema naangamia/ siendelei naona narudi nyuma.

Pia usijidanganye kwamba umwambie mbaya wako upo upo tu ili asione unaendelea, maneno yanaumba. Heri usimjibu au umuulize kuhusu yeye.
Na kwanini uhangaike naye?

Na unaotumia nao muda mwingi wanachangia hilo, aitha wanakusaidia kusonga mbele au wanakurudisha nyuma kimaendeleo yako. Hakuna vuguvugu. Ndo mana we mwenyewe ndani yako unajisikia uchungu/ kutoridhika usiposonga mbele.

Angalia mazungumzo mnayokua nayo muda mwingi, vitu mnavyofanya muda mwingi, sehemu mnazoenda, na kwanini mnafanya hayo mnayofanya, je yote hayo yatakusaidia kusonga mbele?

Utasema … lakini ni marafiki/ ndugu zangu ndo hao nilionao.
Ntakuuliza … upo tayari kwa mabadiliko na maendeleo chanya?
Utajibu … ndio (huku unawafikiria rafiki zako).
Ntakuambia … maendeleo yoyote yana machungu/ sadaka/ kafara yake na mazuri yake, pia huwezi kukosa watu wa kuendana na wewe ukiamua kutafuta na kuwa nao. Na huwezi kuwa na marafiki wabaya na wazuri kwa muda mmoja, chagua moja. Hivyo, kamwe huwezi kosa marafiki wapya wenye malengo sawa na wewe.

Utauliza … lakini naanzia wapi?
Ntakujibu … anza na kujiangalia wewe, hatua uliyopiga kimaisha tangu uwe nao, washukuru kwa kukusaidia kwa lolote, kisha angalia unatamani ufike wapi.

Ukishajua unatamani ufike wapi, jiulize kama kati ya hao ulionao karibu wamefika kwenye hayo maendeleo unayotamani. Kama jibu ni hakuna basi ujue ni muda wako wa kubadili watu wa karibu na kutafuta wengine.

Utasema … lakini ni ndugu zangu siwezi kuwaacha. Siwezi kujitenga nao.
Ntakuambia … kama huwezi kuachana nao, badilisha matumizi ya muda pamoja nao pia kuwa makini na vitu mnavyozungumza.

Kuna vitu watu wanajitakia wenyewe, sote tunafundishwa kwenye dini kwamba hata ardhi inaongea na inashika maneno na kila mguu wako unapokanyaga unaenda na hayo maneno, alafu bado mtu unajitamkia ‘mimi nitaendelea kuwa masikini’, kweli!!
Kwaiyo kuwa makini na mazungumzo unayozungumza nao.
Usiitikie tu kila kitu, na kukubali kila kitu unachoambiwa sababu tu ni baba ako.

Mwingine atainuka na
Kusema … lakini ni mume/ mke wangu, bado nampenda siwezi kumuacha/ kumpa muda kidogo japo ananirudisha nyuma kimaendeleo, nafanyaje?
Ntaguna ntamjibu … apo kweli ni pagumu, ndo mana nikasema maendeleo yana machungu yake. Pengine hadi sasa mmeishi kwa kuridhika na unaona inatosha basi endelea nae.
Lakini kama bado unataka maendeleo, kuna mawili aitha umshirikishe na muongee vizuri pengine muende hata kwa washauri wenu na mpate mafunzo zaidi na wote muendelee kwa pamoja (katika hili uwe mvumilivu SANA) au,
Uchague machungu ya kuyabeba kwa muda, machungu ya kuachana au machungu ya kuishi bila maendeleo. Ukiamua kuachana jitahidi huyo utakayempata tena awe anaendana na wewe sio ukae tena na mchawi anaekurudisha nyuma.

Sawa watakusema unajitenga skuizi/ umetususa skuizi (iyo ipo tu wala isikuumize), kiukweli wanamaanisha tunatamani tuwe kama wewe saivi. Wengine wanaweza wakaja kukuomba na ushauri kabisa, usisite kuwaonesha andiko hili.

Wengi wakiambiwa wamejitenga wanajisikia vibaya na kujikuta wanarudi walipotoka ili wasisemwe. Tafadhali, kuwa na msimamo katika ulichochagua na ujue ni asili ya binadamu kuongea.

Napenda ufanikiwe na uwe na maendeleo zaidi.
 
Upvote 2
Back
Top Bottom