Maendeleo hayana vyama, wapinzani mkubali CCM imebadilika na imefanya makubwa

Maendeleo hayana vyama, wapinzani mkubali CCM imebadilika na imefanya makubwa

Waswahili wanasema mnyonge myongeni ila haki yake mpeni. Vyama vyote vya kisiasa vilianzishwa kw nia moja kubwa ni kushinda uchaguzi na kukamata dola ili kuwatumikia wananchi.

kabla ya uchaguzi wa mwaka 2015 Ccm kilionekana kama chama ambacho kimechafuka na hii ni kwa sababu kulikuwa na ubadhirifu na ufisadi mkubwa hapa nchini. Mfano ni uchotwaji wa pesa nyingi kama bil 300 kwenye sakata la Escrow. Pesa ambazo zinaweza kutumika kujenga vituo vya afya kama mia tatu.

Lakini kila mtanzania anaona kwa macho yake tokea Rais Magufuli aingie madarakani mwaka 2015 kuna mabadiliko makubwa sana. Hasa kwenye udhibiti wa pesa za umma.

Hii imesababisha kuwepo kwa miradi mikubwa kuweza kutekelezwa na miradi hii itakuwa na manufaaa makubwa baada ya kukamilika. Mfano ni mradi wa kuzalisha umeme wa JNHPP huu utalinufaisha taifa kwa kuwa na umeme mwingi na kushusha gharama za umeme.

Mradi wa ukarabati wa gati za bandari ya Dar es salaam uanaelekea kukamilika. Hapa kutaweza kurahisisha meli nyingi zaidi ya nne kuhudumiwa kwa wakati mmoja. Na hivyo kuondoa msongamano na kuliongezea pato taifa letu.

Hii ni baadhi ya mifano tu ya yaliyofanyika kwa muda mfupi tangu JPM aingie madarakani. Na kwa mantiki hii iwe Chadema,Nccr mageuzi,Cuf,Chauma, Chausta na Cck wote mnatakiwa kuunga mkono haya yanayofanyika na kumpongeza rais JPM maana sio hisani bali utashi wake na nia njema ndio umeibadili Ccm kwa muda mfupi.

Kama ni hivyo kwanini kila leo mnaandaa mikakati ya kuua vyama vya upinzani? kwanini muna hofu ya uchaguzi? Kwanini watu wanabambikiwa kesi za ajabu ajabu? Ata leo ni dhahiri mnaogopa uchaguzi Mumeandaa sheria za maadili ili chama kikiuka hayo kifutiwe usajili kabisa kabisa kwanini yooote haya? kwanini yote haya.

Kama mumeleta maendeleo kwa kiwango hicho ni dhahiri wananchi watakuchagueni tena awamu zote zijazo kwanini mnatumia nguvu kubwa kudhoofisha upinzani
 
Wapinzani si wamejimaliza wenyewe baada ya kuona kazi nzuri ya JPM.Madiwani 300 na wabunge 15 wamehama sababu ya uroho na ubinafsi wa wenye vyama.
 
Back
Top Bottom