Maendeleo mapya: Mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Uzalendo

Maendeleo mapya: Mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Uzalendo

Huitaji kuwa msomi wa chuo kikuu kujua kwamba CCM ndio chanzo cha kila tatizo Tanzania. Lakini kama wewe ni msomi na hujagundua kwamba CCM ndio chimbuko la matatizo Tanzania, nakupa pole. Nchi masikini duniani haziongozwi na CCM, lakini Tanzania ilitokea kutawaliwa na CCM kwa zaidi ya miaka 45 na watanzania wana kila sababu ya kutaka CCM itoke kwenye maisha yao. Je itamaliza matatizo yao? Ndiyo. Wengine watafaidi matunda ya ukombozi, na kuna wale dhaifu ambao hawataishi kuonja matunda ya ukombozi. Lakini haitukatishi tamaa ya kujikomboa
 
Kutoa mahubiri marefu juu ya udhaifu wa tume ya uchaguzi kwetu wananchi hakutaleta tofauti yoyote kwani hatuna nafasi ya kusema A na E katika suala la katiba ila pengine kama tunaingia katika suala la rasimu ya katiba ambayo itahitaji maoni ya wananchi.
Jambo la msingi kabisa kwa sasa ni wabunge wetu kukaa chini kweli pale Dodoma na kuamka na utatuzi wa udhaifu unaojitokeza katika tume yetu ya uchaguzi.
Ndugu zetu wa Kenya wametuonyesha mwanzo mzuri sana katika harakati hizi ambazo ni muhimu kwetu. Ili kuondoa makundi ya wakosoaji katika jamii kuhitaji maoni ya wakosoaji hao ndio suala la msingi. Kenya wameepusha shari kwa kupitisha rasimu ya katiba mpya ambayo imepigiwa kura na wananchi.
Watanzania wote tuna nafasi japo kwa viwango tofauti katika ujenzi wa njia ya kuelekea katiba iliyojitosheleza na isiyokosolewa na wadau. Watanzania tuchague lipi? Kurekebisha katiba ili tulinde amani na ustawi wetu au kuhifadhi udhaifu ili baadaye tuwe kama Somalia na Congo –DRC?
 
WanaJF tume kwanza, tukiikamata mikononi mwa bunge hili la kizazi kipya, basi katiba itajipa kirahisi tu!!!!!
 
Kuna Wananchi Wengi Inchini Wanaona Umuhimu wa Katiba na Kama Kawaida Wale Wasiosoma na Kujua Mfumo wa Siasa Nyumbani Watasema Ooo Tumebadili Katiba Mara Kadhaa na Inatosha. Wewe Ulishona Mtu Hataki Kutetea Hoja Yake na Wanabaki Kurudia Maneno ya Wengine. Hii Nchi Sio ya Wanachama wa CCM Peke Yao na Uchaguzi Umedhihirisha Hivyo Kwamba Watanzania Wamechoka na Pipi na Maneno ya CCM. Mfano Gani Mzuri Hatuoni Huu Uchaguzi Ulivyoendeshwa na Kilicholeta na Kusababisha Chadema na International Community to Voice Their Opinions Ni Nini? Sijasikia Hata Msimamizi Hata Mmoja Aliesema CCM Wanaonewa na Hii Katiba. Katiba Kama Ingekuwa Inazungumzia Haki na Uchaguzi wa Ukweli, Kura Zote Zilizokuwa na Utata Zingerudiwa Kuhesabiwa na Atakaeshinda Katika Kuhesabiwa kwa Kura ni Mshindi. Kila Chama Kingeleta Wasimamizi Wao na Hakuna Msimizi Angeandika Ripoti ya Uongo. Chadema na Watanzania Wote Wanataka Mshindi wa Kweli Sio Masanduku ya Kura Kukusanywa na Usalama wa Taifa na Jeshi, ni Kwa Manufaa ya Nani? Ukiangalia Rushwa na Vipengele Vingi Katika Hii Katiba, Raisi wa Nchi na Chama Tawala Wanapewa Power na Hakuna Balance Yeyote ya Mwananchi Kuweza Kuchallenge Jambo Lolote Hasa Matumizi ya Serikali na Utendaji wa Serikali. Check and Balance System Inafanya Kazi Nchi Nyingi na Nchi Hizi Leo Zinamaendeleo kwa Ajili ya Katiba. Hili Sio Swala la CCM Peke Yake Hata Chadema au CUF Wangekuwa Madarakani au Wameshinda Tungeendelea Kuchallenges Hizi Issue Kwa Sababu Failures za Utendaji Tanzania na Maendeleo Yanakwamishwa na Hii Katiba. Sisi Kama Watanzania Tufanye Kampeni ya Nguvu ili Kila Mtanzania Aelewe Ni Nini Umuhimu wa Katiba Mpya na Maendeleo Yetu Kiujumla.
 
Itabidi bunge linalokuja lisimamie kidedea katiba mpya bila hivyo hatutafika popote hata mia 200 inayokuja. Kwa sababu ndio itakayo-dictate tume huru ya uchaguzi itawezesha upinzani kuchukua nchi
 
Haya sasa Bungeni Speaker wanamuweka mwanamke ili akiboronga tu wamtunishie misuli asalimu amri sasa hii ni nini? jamani Hawa jamaa vipi? mbona wana mbinu za kutunyonga kiasi hiki? ndo tuseme interest za chama?
 
Mbona unaanzisha thread zinazofanana kwa wakati mmoja?

Inasemekana Katika maswali ambayo humuudhi Muheshimiwa Jakaya mrisho kikwete, ni pamoja na Swala la Katiba ya Jamuhuli ya Muungano wa Tanzania...

Ameshasikika ,marachache akisema kubadili katiba si maendeleo ya nchi huku akijua kuwa Katiba ndiyo inayo Bana maendeleo ya nchi,,

Tazama Zambia, Tazama Rwanda,, Nchi hizi mbili zilikuwa na rushwa na ufisadi wa kutupwa,, lakini Maraisi wake wameamua kujikubali kuwa lazima Wananchi waumie kwa kuwabana na sheria ngumu zinazo leta maendeleo ya nchi ili baada ya maendeleo hayo kupatikana watafurahia maisha

Wananchi wengi tunaishi kwa kukosa besic needs kwa kiwango kile kinachotakiwa,,,

Katiba hii inatakiwa ibadilishe jamaniniiii
 
Watanzania Tuwaone CCM kama ukoma maanandio chanzo cha kuumia sisis
 
Maneno ya Kibaki yalikuwa mazito kuliko ya JK. Hajaona nguvu ya pipoooooooos wakifikia hatua ya kusema enough is enough!!!!!!!!!!!!!!!. Akumbuke Nyamagana-----pipooooos pawassssssssss
 
Hivi kwanini tusi washawishi Watanzania tuungane Tanzania Nzima Kudai Katiba mpya?
Tuungane kuidai Katiba mpya

Chadema ifanye hima kuungana na civil society ili kuwahamasisha wananchi tangia sasa ilil uwepo mchakato wa kupata katiba inayoendana na wakati huu wa vyama vingi vya siasa. Chadema wasikubali kungoja wakati unapita wa kupata katiba itakayomkomboa mwananchi kutokana na makucha ya hawa mafisadi!!
 
Kenya waliandamana sana kudai katiba mpya. Nakumbuka katika moja ya maandamano hayo, somebidy Prof. Ghai (mzungu au mhindi) alikuwa amevaa T-Shirt iliyoandikwa "Why hire a Lawyer if I can buy the Judge". Kwa maana nyingine, tunahitaji Wa-TZ kuanza kudai katiba kwa maandamano ya amani, migomo baridi hasa kususia mikutano ya wanasiasa wakubwa, na kupiga kampeni ya nguvu ili watu waelewe kwa nini tunataka katiba mpya na watuunge mkono.

Nafikiri hii ndiyo iwe strategy ya kwanza, tukiungwa mkono wa wabunge wote wa upinzani. Najua hamasa ipo. Tukumbuke Mawaziri walipozomewa baada ya bajeti ya pili ya serikali ya Kikwete! Slogan "KATIBA MPYA NA TUME HURU YA UCHAGUZI". Tuwaombe wananchi wawasusie wabunge wao ambao hawataunga mkono hii move.

Dr. Slaa anzia hapo. Tutakuunga mkono.
Sio slaa aanze anza wewe na mimi ndo tuna nguvu kuliko slaa...vipi bana slaa halali njaa, hashindwi kulipa school fees, wala halali mbavu za mbw'a wewe na mimi wazazi wetu wanaokula mizizi kijinini ndo tutaweza
 
Katiba itabadilishwa tu siku si nyingi sana. tena asipoangalia mabadiliko yatakuja kama ambavyo hakutarajia mabadiliko ya uchaguzi huu
Mpaka yesu arudi au ndo zile hadithi na njozi za alinacha...? anza sasa
 
Chadema ifanye hima kuungana na civil society ili kuwahamasisha wananchi tangia sasa ilil uwepo mchakato wa kupata katiba inayoendana na wakati huu wa vyama vingi vya siasa. Chadema wasikubali kungoja wakati unapita wa kupata katiba itakayomkomboa mwananchi kutokana na makucha ya hawa mafisadi!!
hapo sio chadema kaka ni mimi na wewe kushirikiana na civil for society vipi tena bana kumbe na wewe unahitaji kuelimishwa...?:A S angry:
 
Wakati umefika wa kudai katiba mpya mimi na wewe tushiriki kwa pamoja
 
Kama Tanzania hatuta Badili katiba katika miaka hii mitano,, nitawaona Hata hao wabunge tulio wachagua kwa |People powe ni wasaliti tuu,, kwasababu ni moja kati ya Sera za Peoples power kipindi cha Campaign,,
pia kwasababu wao walituahidi watafanya kazi kufuatana na maoni ya Wananchi wengi basi mmi ninamatumaini wao wataanzisha na sisi tuta maliza..
 
duh kanyaga twende tudai katiba mpya JK ni mwajiriwa wetu tumpangie kazi asitupangie!
 
Back
Top Bottom