katiba ni dira ama ramani inayotumiwa na nchi kuongoza watu wake kwa kufuata sheria,taratibu,mwongozo, kanuni zilizowekwa. nasikitika kusema kuwa tanzania imekoswa muongozo sahihi (katiba) hivyo nchi kuendeshwa na kundi dogo kulingana na wanavyo taka. kundi hili hutawala wanavyo taka bila hofu kwa kujua makusudi nchi ina mapungufu makubwa, wasafiri (wananchi) waliomo hawana ramani wala dira hawajui waendako, pamoja na hayo bado walio na dhamana ya kuongoza hawataki kushtuka kwamba abiria sasa wanafahamu kuwa wamepotezwa njia na wanaitaji mambo mawili; kwanza, dira au ramani sahihi ioneshayo waendako itolewe na isahihishwe maana tulishapotea; pili, safari ifuate mwongozo huo.
katiba ndio nguzo pekee itakayo saidia kutufikisha huko tunapo pafikiria kama sio sisi basi watoto wetu, nchi yoyote inapo kosa katiba madhubuti basi inakuwa vulnarable, tanzania tunaendelea kunyemelea hatari nyingi kama bado hatuta washurutisha viongozi wetu kufanya mabadiliko haraka ya katiba tena tusichelewe zaidi maana, viongozi wetu watatupa wakati mgumu sana kuirudisha nchi katika dira sahihi endapo hatutaungana kupinga udhalimu, wanaoutenda kwa wananchi ambao wengi wao bado hawajui wanapelekwa kwenye hatari ya kufa huku wakiimba nyimbo za viburudisho na mipasho. kweli inatia huruma na hasira kwa mtu aliye kwisha soma alama za nyakati.
ukweli tanzania haina amani tanzania haina utulivu, iko wapi amani kwa mtu mwenye njaa? ipo wapi amani kwa mwananchi aliyekosa mahali pa kupumzika? upo wapi utulivu kwa mtu aliyekosa tiba? je mwenye kiu ana furaha? la hasha! hivi ni vilio vya wanyonge walio kata tamaa wanasubiri shujaa kutoa sauti ya matumaini angalau kwamaba wataishi kwa masaa mengine yajayo kabla ushindi haujatangazwa.