Maendeleo mapya: Mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Uzalendo

Maendeleo mapya: Mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Uzalendo

Watanzania walio wengi sasa, hata wale wa ccm, tofauti na siku za nyuma wanaonekana kuwa na mwamko wa kutamani katiba iandikwe upya. Nasema IANDIKWE UPYA sio hii iliyopo itiwe viraka. Kwangu mimi hii ni dalili ya kukua kutoka kwenye hatua moja ya kidemokrasia na mwamko wa kisiasa hadi nyingine. Lakini pia nadhani ni dalili kubwa ya mabadiliko ya mazingira ya kisiasa, kiuchumi, na kila nyanja. Watu wameanza kugundua sasa kuwa shuka ambayo wamekuwa wakijifunika haiwatoshi tena, kwani wamerefuka zaidi, tena shuka hii imechakaa. Wanataka mpya.

Katika hali hii nadhani think tanks wa nchi hii ni wakati muafaka kuijuza jamii ni kwa nini tuwe na katiba mpya, kwa nini tunadhani hii ya sasa imepitwa na wakati, na katiba mpya tunadhani izingatie mambo gani tunayodhani yanahitajika sasa. Nawaita akina political analysts, wanamageuzi, na wadau wengine wote tuchangie hoja hii muhimu. Hebu tulikoke hili jiko la mabadiliko vichwani mwa watz. Badala ya kusema tu tuwe na katiba mpya, tupendekeze pia ni kwa nini tunaihitaji, na iweje. Hii itasaidia kusensitize umma.

Napendekeza tuanze na maeneo ambayo tunadhani katiba mpya itahitaji kucover. Kwa upande wangu nitaje machache:

1. Muundo wa muungano na mgawanyo wa madaraka

2. Ukubwa wa madaraka ya raisi, mf. asiteuwe baadhi ya watu katika nafasi inayotakiwa kuwa huru kama Mkurugenzi wa TAKUKURU, Tume ya taifa ya uchaguzi, Wakuu wa mikoa na wilaya nk.

3. Bunge liwe la uwakilishi wa wananchi kwa 100% pasiwepo viti maalum wala viti vya kuteuliwa na raisi, tena wabunge wasifungwe na vyama vyao katika kuibana serikali, wawe huru, kusiwepo na uwezo wa chama kilichoshika dola kuwashinikiza wabunge wao kukubaliana na matakwa ya serikali palipo na maslahi ya taifa.

4. Mfumo wa uwajibikaji kwenye utendaji wa mihimili mikuu ya dola

5. Mfumo huru wa kupata viongozi, yaani tume huru ya uchaguzi, uwezekano wa kupinga matokeo ya urasi, openness and transparency kwenye uchaguzi.

Tafadhali ongeza, kosoa jadili challenge, ali mradi tupanue hoja. Let's brainstorm friends.
 
Napenda kuwambia WaTanzania wenzangu kuwa ninaunga mkono moja kwa moja madai ya msingi ya Chama cha Chadema kuhusiana na ukarabati au utungwaji upya wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na pia uundwaji upya wa tume ya Uchaguzi ya Taifa ,Ninachowataka viongozi hawa wasitegemee Chama kingine wao kama Chama wasonge mbele na madai haya bila ya kurudi nyuma ,au kusimama kama ilikuwa mwendo mdundo wakati wa kampeni za Uchaguzi sasa ni wakati mwendo mruko juu ya kuwashawishi wananchi ili kuungwa mkono,na wasingojee au kusubiri kwani tabia iliyojengwa ndani ya utawala wa CCM ni wa kusema muda hautoshi, hivyo tuna kipindi cha miaka mitano katika kurekebisha na kuunda upya mambo haya nadhani tunahitaji kama mwaka mmoja au miezi sita tu ikiwa tutatumia wataalamu kutoka nje na kuipitisha Katiba.

Je wewe :angry:
 
hivi jamani kama si chadema haitaanzisha move hii ..... asasi gani au chama gani chenye nguvu ya kupush hii motion ya kupata katiba mpya kabisa wala si kukarabati kwa vile tuliyonayo hata watu wa nje wanasema ni "Obsolete" nani tena atathubutu.. wajameni ... tuwaunge mkono chadema...tukipata hii twaweza kuendelea na kazi nyingine

kwa maoni yangu ..... Death penalty is not friendly with the modern life and progressive life... scrap this Act... soon

Wewe unafikiri ipi haifai..??????
 
Maalim Mwiba kulikoni? Hongera kwa wazo zuri ambalo naona linaitakia mema Tanzania.

Uongozi wa CHADEMA wanatakiwa wakutane na Muungano wa Asasi za Kiraia ili kuona namna watakavyo-push agenda ya madai ya Katiba Mpya kwa kushirikiana. Ni rahisi sana kuzitumia AZAKI kupeleka agenda kwa wananchi kwa kuwa AZAKI zimesambaa nchi nzima na zinajihusisha na mambo tofauti japo common goal ni kuwasaidia wanyonge na kusimamia haki. Kwa kuwa swala hili linagusa vyama vyote vya siasa, siyo vibaya ku-reach out ili kupata support ya vyama vingine ambavyo vina nia ya kutaka mabadiliko.

Pili, Wabunge wa CHADEMA kwa kushirikiana na wabunge wa upinzani ambao wako tayari, waandae Hoja Binafsi ya kuitaka Serikali ianzishe mchakato wa mabadiliko ya katiba. Ili kuweka uzito, watumie hukumu ya Mahakama ya Rufani kuhusu mgombea binafsi, pia kasoro zote zilizojitokeza wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka huu na pia mapendekezo ya Tume ya Nyalali ya kufuta baadhi ya sheria kandamizi.

Iwapo, Mama Makinda na CCM yake watagoma, hapo ndipo watakuwa wametoa plat form nzuri ya mahali pa kuanzia ili kupeleka agenda ya madai ya Katiba Mpya kwa wananchi. Hili la hoja binafsi inabidi lianze mapema sana ikiwezekana Bunge la Januari au April mwakani. Lengo la kuanza mapema ni kuhakikisha kwamba within the first two yrs kiwe kimeeleweka. CCM ni wajanja sana, hoja ikichelewa kwenda wanaweza kuanza kujitetea kwamba mchakato wa mabadiliko ya Katiba unahitaji muda mrefu sana, so wanaweza kusema watabadilisha after 2015.

Wananchi wana kiu kubwa sana ya mabadiliko, iwapo mjadala utazimwa bungeni then ni rahisi sana kuupeleka kwa wananchi. Hoja za Buzwagi na EPA ziliwatesa sana na ziliwaweka CCM kwenye defensive mode miaka yote 3. Kwa hiyo wanaweza kuwa makini sana kwenye kujibu hoja binafsi, na sidhani kama wako tayari kuwa kwenye defensive mode tena kwa kuwa inawagharimu sana.

Wananchi wameishatuma salaam kupitia uchaguzi wa mwaka huu. Watu kukesha wakilinda kura ni dalili kwamba hawana imani na tume ya uchaguzi, ili kuepusha nguvu ya wananchi iliyoonyeshwa Ubungo, Arusha, Mwanza, Mbeya na kwingineko tunahitaji kuwa na tume huru.
 
nilichasema kwenye thread hoja itashindikana mjengoni kwa ajili ya collective responsibility... dawa ni push ya popular party pamoja na wananci kushinikiza serikali ...kubadili katiba
 
msaada sheli jamani,naomba wataalamu mnidadavulie kwa umakini kidogo,hivi katiba ya sasa,mapungufu yake ni nini hasa?
kwanza nijihami kidogo,si maanishi haina mapungufu,nadhani yapo,ila sijui hata moja.nipeni shule hapo wapendwa
 
msaada sheli jamani,naomba wataalamu mnidadavulie kwa umakini kidogo,hivi katiba ya sasa,mapungufu yake ni nini hasa?
kwanza nijihami kidogo,si maanishi haina mapungufu,nadhani yapo,ila sijui hata moja.nipeni shule hapo wapendwa

Ili watu wengine wadadvue nawe uelwe ni vema ukijipa Head Start kwa kuisoma kwanza.

http://www.tanzania.go.tz/images/katibamuungano.pdf

Baada ya kuisoma bila shaka utakuwa na maswali ya moja kwa moja.
 
Sitaki kuamini hivyo...lakini Makyembe na Sitta kuingizwa kwenye baraza la mawaziri haijakaa vizuri.....

Mara ya kwanza nilifikiria itakuwa pigo kwa mafisadi kwamba itakuwa message sent kwamba JK yupo pamoja na kundi la anti-mafisadi (Sitta, Makyembe na wengine) lakini on second thought ndio ni kawa na mawazo kama yako...any way let us wait and see....
 
Watanzania kama kweli tunahitaji mabadiliko lazima tusimamie kidete mabadiliko ya katiba. Tunatakiwa kufahamu kuwa kiburi kilichoko ndani wa viongozi wa chama tawala ni kwa sababu katiba inawalinda. Uhuru wa kuongea utulinde na ikiwezekana tuandamane nchi nzima ili vilio vya walalahoi visikike.
 
Naunga mkono hoja lazima ibadilishwe kwa gharama yeyote ile hata ikibidi kuingia barabarani tuingie tuu,watu wanaviburi kweli anadhani anaendesha nchi kama kampuni binafsi inaudhi kweli
 
Sitta abaki benchi kupambana na ufisadi na kusaidia kusukuma mbele wazo la kubadili katiba na kuwa na tume huru
 
Mkubwa uko sahihi kabisa! Mimi nashangaa kwa nini Vyama pinzani vinashangaa kushindwa kila uchaguzi!!.. Hivi kweli itoke siku Yanga waandae mechi na Simba, halafu uwanja uwe wa Yanga... Refa atafutwe na Yanga... Obvious washabiki watakuwa wa Yanga... Halafu Simba ipate nafasi ya kushinda!!!!!? No way!!!... Mazingira ya kisiasa kwa vyama pinzani ni mabaya zaidi ya mno!!! Na hii yote ni kwasababu ya KATIBA FEKI!!!
 
Katiba yetu ilikuwa nzuri sana miaka ya 70' ambapo mfumo wa demokrasia ulikuwa still low na hata watu walikuwa hawana upeo wa kuhoji na kuweka wazi msimamo wao... lakini imezeeka na haifai kuendelea kutumika kwa sababu bado inafunga na inakinzana na mapinduzi ya demokrasia nchini Tanzania bado ipo kwenye miaka ya 70'.Kitu ambacho tunakihitaji sasa kutokana na wale tuliowaamini na kuwakabidhi madaraka wametumia nyadhifa zao vibaya...mfano katiba yetu hairuhusu uchunguzi wa matokeo baada ya NEC kuyatangaza,ibara ya 41 ibara ndogo ya 7,..jamani hii si njia ya kuuziba mdomo ukuaji wa demokrasia nchini?
Mimi naunga mkono katiba ibadilishwe thats 1 man down out of 44milion...so wanajamii tunaunga au tunapinga?

Mimi nakuunga mkono mia kwa mia! Hapa kinachotakiwa ni kufanya kweli na sio kuendelea kurumbana. Strategies ziwepo...well organized plans then tunaingia uwanjani tukiwa full combat...!
 
kichwa chako cha thread hakiko sahihi, katika mdahalo siku mbili kabla ya uchaguzi mhe jakaya kikwete akijibu swali hilo alisema kuwa "kuwa katiba imeshafanyiwa mabadiliko mara nyingi tu haja inapojitokeza, na akaendelea kama itakuwepo haja ya kuifanya katiba mabadiliko serikali iko tayari kufanyia hivyo.

Kwa kauli hiyo ni wazi kuwa mlango wa majadiliano ya mabadiliko ya katiba uko wazi. Sipendi negativity ambayo wengi wetu tunayo kiasi cha kushindwa kutumia forum hii kubrain storm solutions za matatizo yanayoikabili tanzania hasa kuhusiana na katiba na tume ya uchaguzi mbovu.

Ni ukweli usiopingika kuwa katiba ya sasa ya inakipendelea chama tawala (ccm); na ni ukweli kwamba cccm kina wanachama kama milioni 3 mpaka 5 nchi nzima. Hivyo viongozi wa ccm wanabasis ya kudai kuwa katiba iliyopo haina tatizo wakitarajiwa kuungwa mkono na idadi hiyo wanachama.

Ni ukweli usiopingika kuwa tokea mfumo wa vyama vingi vya siasa kuanza mwaka 1992, vyama vya upinzani vimejitahidi sana kudai mabadiliko ya katiba kupitia njia mbali mbali ikwemo maandamano ya amani. Lakini kwa bahati mbaya watanzania waliokuwa wakijitokeza katika maandamano hayo ni wachache sana; sijui ni wangapi miongoni mwetu tulikuwa tukijitokeza wakati huo? Na sijui leo hii kama maandamano ya amani ya kudai mabadiliko ya katiba yataitishwa ni wangapi watajitokeza kuweza kupelekea ujumbe kwa watawala kuwa watanzania walio wengi wanataka mabadiliko ya katiba.

Hoja inayokuja hapo ni watanzania wangapi wasiokuwa wanajf wanafahamu kuwa mabadiliko yameshindikana kwa njia ya sanduku la kura kutokana na mapungufu makubwa ya katiba yeti na tume ya uchaguzi; na suluhisho ni kudai mabadiliko kwa njia za amani ama sivyo hadithi itakuwa ile ile mwaka 2015 kama ilivyokuwa 1995, 2000, 2005 na 2010.

Kama kweli tumekasirishwa na wizi wa kura unaolelewa na katiba mbovu na tume ya uchaguzi isiyokuwa huru, kila mmoja wetu anatakiwa kuanza kazi ya kuwaelimisha watanzania popote alipo mapungufu ya katiba tuliyonayo na kuwahamasisha kushiriki katika shughuli mbali mbali za kudai kmabadiliko ya katiba kwa njia za amani kama vile maandamano, makongamano, warsha semina n.k.

Shughuli hii inatakiwa kwenda sambamba kwa sisi tunaotaka mabadiliko ambao tunaona kuwa chadema ndio ngarawa yetu ya kutufikisha kwenye lengo hilo kukijenga chama cha chadema kutoka ngazi ya taifa kwenda ngazi ya mikoa, wilaya, tarafa, kata , vijiji, mitaa hadi kwenye mashina walipo watanzania. Hayo ndio mamabo mawili tunayotakiwa kuyafanya kati ya sasa hadi 2015 badala ya kuendelea kulia kulia pasipo kuchukua hatua zozote muafaka.

Kwa kuwa ccm wanatambua kuwa siasa ni watu, ni wazi katika kipindi cha 2010 -2015 watatumia mbinu mbali mbali kuhakikisha kuwa chadema inapungukiwa na uungwaji mkono wa wananchi. Endapo wapenda mabadiliko atutafanya mambo hayo mawili yaliyotajwa hapo juu, ni wazi kuwa 2015 si ajabu tukashuhudia ccm wakifanikiwa kusambaratisha vuguvugu la mabadiliko, ambapo itachukua muongo au miwili kujenga taena vuguvugu hilo.

Bahati ambayo tunayo ni kuwa penye riziki fitina hazikosi, kama alivyoanza chenge ccm ndio wameshaanza kugo,mbea madaraka na baada ya la uspika watafuata kugombea uwaziri, watagombea uchguzi kwenye chama na mwisho urais wa 2015. Huu ndio wakati tunaotakiwa kuutumia vyema kujijenga kwa wananchi ili ya 2010 yasiweze kujirudia.

Hapo mkuu umenena haswa!!!
Kwa hiyo umetangaza vita, mapambano ya kudai katiba mpya.
Basi kwa njia hiyo ebu tuige wenzetu Wakenya walifanyaje mpaka katiba mpya ikapatikana. Kwanza inahitajika taasisi zisizo za kiserikali (Km; Kama yule mama Ananilea Nkya na taasisi yake) Wanasheria (Tanzania Law Society) na wengineo pomoja na political parties. Wafanye kwa kushirikisha wananchi wenye nia njema na Watanzania, makongamano, midahalo na shughulizingine zenye mwelekeo wa kuelimisha jamii NA KUHAMASISHA juu ya kuwa na KATIBA bora ya kumkomboa Mtanzania toka lindi la umasikini. Uzuri wake ni kwamba Watanzania wa sasa wameanza kuamka, wataelewa ni kitu gani tunatakiwa kufanya.Midahalo mingi wakati wa uchaguzi mbona watu wengi tuu walihudhuria. Mbona hamasa za AIDS na Maralia zinaeleweka? Tusianze kukata tamaa kabla hatujaanza ebu wale ndugu walio mbele (politicians and non govmental org's na wanasheria) watoe dira.THINGS WILL FALL IN PLACE. (BOMAS OF KENYA)
 
Hapo mkuu umenena haswa!!!
Kwa hiyo umetangaza vita, mapambano ya kudai katiba mpya.
Basi kwa njia hiyo ebu tuige wenzetu Wakenya walifanyaje mpaka katiba mpya ikapatikana. Kwanza inahitajika taasisi zisizo za kiserikali (Km; Kama yule mama Ananilea Nkya na taasisi yake) Wanasheria (Tanzania Law Society) na wengineo pomoja na political parties. Wafanye kwa kushirikisha wananchi wenye nia njema na Watanzania, makongamano, midahalo na shughulizingine zenye mwelekeo wa kuelimisha jamii NA KUHAMASISHA juu ya kuwa na KATIBA bora ya kumkomboa Mtanzania toka lindi la umasikini. Uzuri wake ni kwamba Watanzania wa sasa wameanza kuamka, wataelewa ni kitu gani tunatakiwa kufanya.Midahalo mingi wakati wa uchaguzi mbona watu wengi tuu walihudhuria. Mbona hamasa za AIDS na Maralia zinaeleweka? Tusianze kukata tamaa kabla hatujaanza ebu wale ndugu walio mbele (politicians and non govmental org's na wanasheria) watoe dira.THINGS WILL FALL IN PLACE. (BOMAS OF KENYA)
Ndg zetu Wakenya wanaotutakia mema Watanzania hebu tupeni ushauri na maelekezo!!!
 
Tupatieni Katiba Yetu
Kelvin Kachingwe

LUSAKA, Okt 28 (IPS) - Shinikizo linazidi kupanda kwa ajili ya katiba mpya inayoainisha maoni ya wananchi wakati ucheleweshaji wa kuandaa rasimu hiyo bado unaendelea.

Pamoja na kwamba Kongamano la Taifa la Katiba (NCC) liliongezewa muda wa miezi minne kutoka ombi la kwanza la miezi 12, shinikizo inazidi kupanda kwa chombo hicho kukamilisha katika muda uliowekwa ili nchi ipate fursa ya kuendesha uchaguzi mwaka 2011 chini ya katiba mpya.

Zoezi la kuandika rasimu ya katiba mpya ambalo liliwashirikisha wananchi katika mijadala, lilianzishwa na rais aliyefariki Levy Mwanawasa. Lengo lilikuwa kuizuia serikali pekee kupitisha Katiba ya Jamhuri kinyume na demokrasi.

Chombo cha NCC, ambacho kilianzishwa mwaka 2007, kilitakiwa kuandika rasimu ya katiba ambayo ingesubiri maoni ya wananchi katika kipindi cha mwaka mzima.

Lakini ilipofika katikati ya mwaka 2009, NCC iliomba mwaka mmoja zaidi ili kufanikisha zoezi. Rais Rupiah Banda, ambae ana mamlaka ya kukubali ametoa miezi minne tu badala ya 12 iliyoombwa.

Akitangaza kuhusu kuiongezea muda dhamana ya NCC wakati wa uzinduzi rasmi wa bunge mwezi uliopita, Rais Banda amesema anasikitishwa na jinsi mambo yanavyoenda polepole.

Tilyenji Kaunda, mtoto wa rais wa kwanza, Dr Kenneth Kaunda na kiongozi wa chama cha upinzani cha United National Independence, anasema NCC haina budi kumaliza kwa haraka kazi yake katika muda uliowekwa ili uchaguzi mkuu ujao ufanyike chini ya katiba mpya.



"Katika vikao vyake vijavyo, NCC hazima ihakikishe inamaliza kazi kwa sababu wananchi wengi wa Zambia wana shauku kuona katiba mpya kabla ya uchaguzi mkuu ujao," amesema katika mkutano na vyombo vya habari mapema mwezi huu.

Chama cha upinzani cha United Party for National Development (UPND) kinasema kwamba kina wasiwasi kwamba muda ulioongezwa wa mchakato wa katiba mpya ni ishara kwamba nchi haitakuwa na katiba mpya wakati wa uchaguzi mwaka 2011.

"Iwapo tutaendelea kuongeza muda wa NCC, kuna uwezekano wa kutokuwa na katiba mpya mwaka 2011 kwa sababu bado kuna mazoezi mengine kadha ambayo yanatakiwa kufanyika hususan kuendesha kura ya maoni, ndio maana kuongezwa kwa muda sio dalili nzuri kwa taifa," Charles Kakoma, mwenyekiti wa habari na uhamasishaji wa UPND anasema.

Hata hivyo, msemaji wa NCC, Mwangala Zaloumis anasema kuongeza muda ni muhimu kwa sababu mbalimbali ambazo zimeifanya NCC kushindwa kufikiria ripoti za kamati sita kati ya 11 ambazo chombo kilistahili kuzipitia wakati wa kipindi cha mwaka mmoja wa mamlaka hayo.

"Kuongeza muda kulisababishwa na mambo mengi, baadhi ya hayo ni kifo cha Rais Mwanawasa mwaka uliopita, kufanyika kwa uchaguzi mdogo wa rais na vile vile mabadiliko ya hivi karibuni katika mzunguko wa bajeti. Wakati Bunge linaendesha kikao chake, NCC hairuhusiwi kufanya kazi," Zaloumis amesema.

Profesa Patrick Mvunga, mwanasheria wa katiba, anasema kwamba kuharakisha mchakato wa kutayarisha katiba mpya kwa sababu ya uchaguzi mkuu mwaka 2011 hakutaweza kuleta matokeo mazuri yaliyokusudiwa.

"Ni vizuri kila wakati kufanya kazi nzuri, na kazi nzuri lazima iende na wakati. Iwapo sababu kubwa ya kuwa na katiba ni kwa ajili ya uchaguzi, wale wote wanaotaka katiba ikamilishwe badala yake waiambie NCC wamalize kuzishughulikia sheria zote zinahohusu uchaguzi," Profesa Mvunga anasema.

" Kama ni muhimu hivyo, ingebidi vipitie vifungu vinavyohusiana na uchaguzi na ndio maana sielewi pale watu wanaposema kwamba lazima tuwe na katiba kabla ya uchaguzi mwaka 2011 kwa sababu sio vifungu vyote katika katiba vinahusu uchaguzi, sio mambo yote katika katiba ni uchaguzi."

George Kunda, makamu wa rais nchini alisema mwaka uliopita kwamba NCC itamaliza kazi yake ifikapo Desemba 2009 ili taifa liwe na katiba mpya kabla ya uchaguzi mwaka 2011 lakini aliongeza kwamba mchakato lazima uwe wenye uhalisi na sio wa kuharakisha.

"Hatuwezi kuhujumu mchakato kwa kupendekeza muda usio halisia. Tutamaliza kati kabla ya 2011, lakini tusipendekeze muda ambao hauendani na kazi yenyewe," amesema.

Mwezi Julai 2008, kikundi cha vyama vya vyama hiari, katika barua walioiandikia sekretarieti ya NCC na kunakili kwa Rais, Waziri wa Sheria na Mwanasheria Mkuu, ilidai kwamba kongamano limalize kazi yake ifikapo mwishoni mwa mwezi Julai 2009 na kutoa ripoti ya fedha ya kina kuhusu matumizi ya fedha za umma tangu ilipoanzishwa.

Mashirika yamesema kwamba NCC ilibidi kumaliza kazi yake mara moja ili kutoa fursa kwa zoezi jingine linalohusu ya kupitishwa kwa katiba, hususan Kura za Maoni, liweze kufanyika kabla ya uchaguzi mwaka 2011.

"Zoezi kubwa kama hilo haliwezi kuachiwa lifanye kazi bila kuwa na ratiba maalum…na ili kuonyesha uwajibikaji na uwazi, tunataka ripoti ya fedha kutoka NCC na matumizi yake," ilisomeka sehemu ya barua hiyo iliyoandikwa na baadhi ya wawakilishi kutoka Transparency International Zambia, Citizens Forum, Women in Law Southern Africa na Southern African Centre for Constructive Resolution of Disputes.

Kujibu hoja hiyo, mwenyekiti wa NCC Chifumu Banda alisema kwamba kongamano ni taasisi ya serikali ambayo hukaguliwa na Mkaguzi Mkuu.

"Katibu wa NCC ndie afisa mdhibiti pamoja na mafungu yote yanashughulikiwa na watumishi wa serikali. Matumizi yetu yatawekwa wazi kwa wananchi," amesema.

Lakini Michael Sata, kiongozi mkorofi wa upinzani kutoka chama cha Patriotic Front anapinga kuongezewa muda NCC na anatoa changamoto kwa chombo hicho kuonyesha maendeleo yaliyofikiwa hadi sasa.

"Kila mtu NCC, hawako pale kutayarisha katiba, wako pale kugawana dola milioni 80 zilizotengwa kwa ajili ya kazi hiyo. Watatumia kila sababu kuhakikisha kwamba ‘wanazimaliza’ dola milioni 80 kwa ajili ya vikao," Sata amesema.

Situmbeko Musokotwane, waziri wa fedha, katika hotuba yake ya bajeti mwezi uliopita, ametenga fungu jingine la dola milioni 1 kwa ajili ya NCC baada ya rais kuongeza muda wa mamlaka hiyo kwa miezi mingine minne.

Mapema mwaka uliopita, katibu wa NCC Russell Mulele alisema kwamba ingawaje rais ana mamlaka ya kuongeza mamlaka baada ya muda wa miezi 12 kumalizika, watahakikisha kwamba wanakamilisha kazi hiyo katika muda uliowekwa ili uchaguzi mkuu mwaka 2011 ufanyike chini ya katiba mpya.

Banda anasema ana imani kubwa kwamba katiba mpya itakuwa tayari kabla ya uchaguzi mkuu.

"Hatutarudi nyuma kwa sababu tumetoka mbali na tunakaribia ukingoni kukamilisha zoezi la katiba," Banda anasema.

"NCC ina muda maalum ukiondoa siku ambazo Bunge linafanya kikao, siku za mapumziko na siku za mwisho wa wiki, isingekuwa hivyo na maombolezo ya Rais Levy Mwanawasa, tungefika mbali."

Kupitishwa kwa Sheria ya NCC kunatokana na mapendekezo ya wananchi kwa Kamati ya Kupitia Katiba ya Wila Mung’omba kwamba katiba ipitishwe na Bunge, Kongamano la Katiba au chombo kingine chochote kinachoaminika ambacho kitawakilisha mawazo ya wananchi. (END/2009)


Someni kwa Wazambia jamani Wapo juu kutuzidi sisi kwanini tubaki nyuma jamani?

Hapo umenena Ndg Yangu Silver25. KATIBA MPYA NDILO JIBU LA UMASIKINI WETU. Tusiyumbishwe na siasa za kifisadi, malengo yetu yawe ni katiba mpya. Sio kuwa na baraza la mawaziri hamsini. Yaanai mtu anajipangia tu anataka wakubwa wenzie wangapi!
Jibu la yote hayo ni katiba definitive self explanatory on the size and type of goverment we should have. VIVA KATIBA MPYA.
 
Mi naona kuna haja ya Wananchi Watanzania Wazalendo na wenye uchu wa Maendeleo Tanzania, tunge andamana kila mtu Mkoani kwake kwa siku moja kwamfano Dar Jtatu, basi Tanzania nzima J3

MAANDAMANO NDO SULUHISHO LA KSTAKABALI WA KATIBA MPYA
 
...Bila ya kutaja matatizo ya katiba yetu, ningependa kueleza
sema ni nini tatizo la hiyo Katiba!

Hivi unawezaje kuwa na theme ya kudai kubadilisha Katiba lakini huwezi kusema jack squat about what's wrong with the Katiba????

Kila mtu katiba ibadilishwe katiba ibadilishwe katiba ibadilishwe... NINI KIBADILISHWE? MTU HAJUI, HAJAWAHI KATA KUISOMA
 
Mkakati wa kudai Katiba mpya ya nchi ya Tanzania.

Wadau, baada ya kipindi cha uchaguzi kumalizika, kila mtanzania mwenye nia njema na nchi hii, atakubaliana na mimi kuwa kwa sasa tunaanza kudai katiba ili yale yaliyo tusibu kwenye uchaguzi ulioisha, yasije tukuta tena, make bado nasikia kizungu-zungu cha tume ya uchaguzi kututajia madudu badala ya kutoa hali halisi na hatimaye kuwa na kiongozi aliye chomekwa na tume ya uchaguzi ya ccm.

Naomba tuchangie mapendekezo ya hatua za kuchukua ili tuwapelekee watu wetu ambao wamesha onja harufu ya mjengoni ili kwamba Bunge lijalo waanzishe mchakato.
  1. Maandamano ya amani ya kudai Katiba mpya, itakayo ainisha mambo muhimu likiwemo
  • Muundo wa muungano- Sio mtu kutoka Zanzibar anakuwa mbunge wa Jamhuri wakati mtu kutoka bara, haruhusiwi hata kutembelea Zanzibar.au kuwa mbunge huko Zanzibar.
  • Mzanzibar anakuwa waziri wakati mbara hawezi kuthubutu, kwanini kunakuhongana?
  • Idadi ya uwakilishi kwenye bunge, mfano jimbo la ubungo, mbunge ni mmoja anayewakilisha watu zaidi ya laki moja, wakati Zanzibar mbunge mmoja anawakilisha takribani watu 5,000. Huu uwiano unanipa kichefuchefu!!!!!!!!!!
  • Wanafunzi wanao lipiwa kutoka Zanzibar kusomea vyuo vya bara, wao wanalipiwa moja kwa moja na serikali, wakati wa bara wanashinda wanakimbizana na fomu za mikopo ya HESLB na wanakosa muda wa ku-concentrate na masomo.
  • Kodi ya kuagiza kama magari kupitia Zanzibar kuwa tofauti na ile ya bara, wakati wanadanganya kuwa tuliungana!!!!!


BILA KUANZA HUU MCHAKATO TUME ITAKUWA KILA MWAKA INATUTANGAZIA RAIS FEKI.
 
Back
Top Bottom