Maendeleo mapya: Mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Uzalendo

Maendeleo mapya: Mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Uzalendo

Dai lingine:
Mtu anayetokea Zanzibar kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuongoza hadi Tanzania bara wakati mtu wa bara hawezi kuwa rais wa Zanzibar
 
Maandamano kwa bongo ni ngumu labda ujaribu mapendekezo mengine ila kiukweli katiba mpya ni muhimu!
 
Kufanya hii issue ifanye kazi.... fanya yafuatayo
  • Maandamo ni magumu kufanya kwanza hautapewa kibali, ukipewa itakuwa ni issue ya siku moja media huenda hazitakupa enough coverage na baada ya siku utasahaulika. Cha muhimu ni kuandaa Petition... Watu wasaini kwenye majimbo yao na hata online na baadae kuwapa wabunge wao kama ammunition ili waende nayo bungeni ikajadiliwe.
  • Issue fanya iwe ni kubadilisha katiba na sio kuwe na nini ndani ya katiba (ukisema kuwe na nini ndani ya katiba unamaanisha kuiwekea viraka katiba)
Kwa haya yakifanyika strategically utafanikiwa bila shaka
 
Strategy Nyingine inayoweza kutumika ni kutoa namba ya simu; ili watu watume sms na majina yao uyakusanye yote kwenye Data Base yakifika kama milioni Tatu kutakuwa kuna Case ya kuweza kupeleka Bungeni...... ILA ISSUE IWE NI KUBADILISHA KATIBA WENGI THEY FEEL ABOUT THIS Jambo la muungano can come later wakati wa kubadilisha katiba
 
Kudai katiba mpya maana yake ni kuzungumzia issue za muungano tu? kwa taarifa yako mambo yanayotia kichefu chefu wala sio hao uliyoyaorodhesha, ungeongelea mamlaka aliyonayo rais wa Jamhuri, muungano wa vyama vya siasa kukubalika kikatiba, muundo wa tume ya uchaguzi, uteuzi wa mawaziri na kama hayo, muundo wa serikali tatu n.k
Punguza chuki zisizo na msingi ndugu yangu.
 
I agree ndugu yangu kupata response nzuri futa hizo point zote na uache heading peke yake
 
Dai lingine:
Mtu anayetokea Zanzibar kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuongoza hadi Tanzania bara wakati mtu wa bara hawezi kuwa rais wa Zanzibar

Hii inanipa shida sana. HIVI huu ni muungano au ni miradi ya wapemba na viongozi wasio tumia fikra, wao wanapokea tu bila ku-reason!

Naliorodhesha kwenye madai pia
 
Kufanya hii issue ifanye kazi.... fanya yafuatayo
  • Maandamo ni magumu kufanya kwanza hautapewa kibali, ukipewa itakuwa ni issue ya siku moja media huenda hazitakupa enough coverage na baada ya siku utasahaulika. Cha muhimu ni kuandaa Petition... Watu wasaini kwenye majimbo yao na hata online na baadae kuwapa wabunge wao kama ammunition ili waende nayo bungeni ikajadiliwe.
  • Issue fanya iwe ni kubadilisha katiba na sio kuwe na nini ndani ya katiba (ukisema kuwe na nini ndani ya katiba unamaanisha kuiwekea viraka katiba)
Kwa haya yakifanyika strategically utafanikiwa bila shaka

Mkuu nimekusoma. Thanx
 
Jamaa me nipo hapa Marekani navinjari kidogo lakini kuna Maprof wananiambia tatizo la Tz ni kuwa hamna wasomi wanaoichachafya serikali. Me nikabisha bwana. Wakaniambia kama wapo mbona mpaka sasa hatuoni wameweka forum yao wakiandamana kutaka katiba mpya
Kama kawaida yangu nikajipanga kwa hoja kidogo. Nikawapa mifano ya Prof Maina na Safari ambao tayari kwa nyakati tofauti wameshatoa mawazo ya kuwa na katiba mpya Tz
Lakni maprof wakaendelea kunibana. Wakanikandamiza na hoja kuwa ingekuwa kwao hoja ya msingi kama hiyo haihitaji mwanasheria ila msomi aliyeboboe kulipika na angenda hiyo na kuja kuwambia watu kuwa kinachotakiwa ni kujitolea na kuamsha ari ya watz kuwaunga mkono.

Nikaishiwa nguvu kidogo, lakini kama kawaida nikawapa mifano mengine ya akina Lwaitama.
But, rohoni nakumbuka jinsi gani hata palle UDASA maprof walivyogawanyika wakidai maslahi yao.

Lakni cha ajabu ni kuwa mpaka sasa maprof magwiji wengine hawajajitokeza kudai katiba. Wako wapi watunga sera za wanyama pori na zingine akina Prof Kabudi? Au wako kwa masuala ya hela na kuitetea kutokuwepo kwa mgombea binafsi?

Ninaonavyo mimi wenzetu wataendelea kudharua kwa sababu hata katika masuala ya msingi na mfano wasomi wa Tz wanabaki wanakaa kimya utafikiri jamii haina tatizo. Kutokuwepo katiba ni tatizo kubwa la kujamii (Its a social crisis which requires sociatal solution)

Maprof, tuungane na watz wote wenye dhamira njema ya kupigania katiba mpya. Si Agenda ya chadema tu ni hitakji la watz
 
Wanajamii na Wananchi Tujadili Katiba Yetu. Leo Tunaona CCM Wanakataa au Kukwepa Kuzungumzia "Mabadiliko ya Katiba" na "Sheria" za Sasa Inchini. Wananchi Tunaona Wazi Makosa na Uvunjwaji wa Demokrasia Kila Leo. Tukiangalia Jinsi Ofisi ya Raisi wa Tanzania Ilivyo na "Absolute Power" Kuliko Chombo Kingine Chochote Inchini Tutaona Makosa Mengi Ndio Yanapoanzia. Katiba Hii ya Sasa Inasema Raisi Ndie Kuteua Viongozi Kila Kona ya Inchi. Raisi wa Tanzania Anahusika Kuteua Waziri Mkuu, Mawaziri, Manaibu, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Mabalozi, Majaji, Wakuu wa Jeshi, Wakuu wa Polisi na Wakurugenzi wa Shughuli Zote Serikalini. Wananchi Wengi Tunajua Hii ni Hatari Katika Demokrasia. Hatuwezi Tukasema Tuna Uhuru na Demokrasia Safi Kama Inchi Zilinazotaka Kuendelea. Sehemu Zote Nilizozitaja Hapo Juu ni Muhimu Sana Katika Serikali Yetu na Hawezi Kufanya Kazi kwa Uhuru Wao au Bila Kuingiza Siasa. Wananchi Wengi Wana Lazimika Kujiunga CCM ili Wateuliwe Kufanya Kazi Serikalini. Uchanga wa Upeo Ndani ya CCM Hawajui Hatari ya Kuweka Mwanachama wa CCM Kuwa Jaji Mkuu Badala ya Jaji Ambaye Atakuwa Anaonyesha Si Mwanasiasa na Kutetea Haki ya Mwanachama wa Chama Chochote Kile. CCM Hawajui Hata Wenzao Wangekuwa Wawajibikaji Kama Wanajua Matokeo ya Kufanya Makosa Makubwa Kama ya Chenge na Lowasa Yasingetokea? Wafanyakazi Wengi Serikali Hawapo Huru Kufanya Kazi Zao na Hii Tunasikia Kila Leo Sio Kwa Sababu ya Utendaji Ila Wanapata Maelekezo Kutoka Viongozi Ndani ya CCM Badala ya Knowledge na Skills Walizosomea. Hili Jambo Limeiangusha Judicial System na Kufanya Kila Mtanzania Kufanya Kazi kwa Kuangalia Paycheck Sio Upenzi na Inchi Yake. Taratibu Zenyewe za Bunge Zinasema Mabadiliko ya Katiba na Sheria Lazima Yaletwe Bungeni na Mwanasheria na Ofisi ya Raisi, Sijui Bunge Lina Maana Gani hapa Tanzania? Je Tanzania Ikipata Idi Amin na Katiba Yenyewe ni Hii? Tutakuwa Tumejiingiza Shimoni Zaidi? Sasa Hivi Tunaona JK ni Kama Putin Vile.

Mpaka Sasa Hatujajadili Hatari ya Katiba Katika Uchaguzi Ambapo Watanzania Wengi Tumeona Kura Zilivyo Chakachuliwa na Tume ya CCM. Hii ni Katiba Kweli au ni Kichekesho Jamani? Katiba Hii Imetengenezwa kwa Malengo ya Kulinda Chama Kimoja Ambacho ni CCM. Sisi Watanzania Wataka Mapinduzi ya Kubadilisha Inchi Yetu Tuwafikie Wananchi Wote na Kuwaelimisha Juu ya Katiba Mpya Mapambano Ndio Yameanza Hivyo.
 
sasa rais atakuwa na kazi gani kama kazi zote zitafanywa na mwanainchi? Na atawamurisha vipi kwa sababu hajawachagua yeye? Lakini sasa hivi anaweza kuwafukuza kwakuwa wako chini yake!
 
Wa TZ ni Kondoo!
Labda tufanyiwe POLITICAL GENETIC MODIFICATION
 
KWELI KABISA!!!

Hii ndio ilipelekea PhD holder slaa kugombania urais akijua katiba ina matatizo na nec ina matatizo, PhD aliiweka mfukoni, sembuse wa hapo mlimani? tumbo baya yakhe!
 
Jamaa me nipo hapa Marekani navinjari kidogo lakini kuna Maprof wananiambia tatizo la Tz
profesa wa Marekani doesn't know jack squat about "tatizo la Tanzania" and if he knew he wouldn't solve it, that's why he fled in the first place
 
Wanajamvi, Wananchi, na Wadau wa vyama vyote....

Naomba msaada wenu wa kukusanya takriban saini 5,000,000 za wananchi wa Tanzania ili kuomba Katiba mpya, Nimeweka deadline ili tuwe tumepata sahihi hizi by February.

Attached kuna fomu yenye namba hadi 27 unaombwa uwape watu wajaze au utoe photocopy na kuwapa watu tofauti wajaze, pia unaweza kuzituma kwenye email za watu, facebook etc. Fomu ikikamilika naomba uiscan na kuituma katika email ya mpyakatiba@yahoo.com nitakuwa ninatoa update jamvini ya majina yamefika mangapi na kwa kila atayehitaji tampa file ya documents za majina hayo mpaka wakati huo.

Lengo ni baada ya kupata majina hayo ni kuyapeleka kwa wabunge wetu ili tuwaombe sisi tuliowachagua watupe tunachowaomba. Tafadhali wajaze watu wazima na kwa hiari yao na si kuwalazimisha
 
Attachments

Wanajamvi, Wananchi, na Wadau wa vyama vyote....

Naomba msaada wenu wa kukusanya takriban sahihi 5,000,000 za wananchi wa Tanzania ili kuomba Katiba mpya, Nimeweka deadline ili tuwe tumepata sahihi hizi by February.

Attached kuna fomu yenye namba hadi 27 unaombwa uwape watu wajaze au utoe photocopy na kuwapa watu tofauti wajaze, pia unaweza kuzituma kwenye email za watu, facebook etc. Fomu ikikamilika naomba uiscan na kuituma katika email ya mpyakatiba@yahoo.com nitakuwa ninatoa update jamvini ya majina yamefika mangapi na kwa kila atayehitaji tampa file ya documents za majina hayo mpaka wakati huo.

Lengo ni baada ya kupata majina hayo ni kuyapeleka kwa wabunge wetu ili tuwaombe sisi tuliowachagua watupe tunachowaomba. Tafadhali wajaze watu wazima na kwa hiari yao na si kuwalazimisha

Binafsi mimi sina tatizo na wewe ila nataka kufahamu wewe ni nani, maana mimi nawza kuwapata na kugharima vijana kama 100 na wazee kama 100 jumla mia mbili issue ni kwamba this has to come through a trusted source.

Peoples Power.
 
Ni kweli, ni vizuri tupate maelezo ya utangulizi. Nani anaecoordinate jambo hili. Ama ni taasisi ipi? Tafadhali tunaomba utambulisho. Kwani hata fomu yenyewe haina utambulisho wala nembo ya taasisi inayohusika. Najua kujitambulisha kunaweza kuleta shida hasa kiusalama, lakini hivi sasa ni ukweli ulio wazi kuwa suala la Katiba mpya imekuwa agenda ya kitaifa. Tafadhali tusaidie kulifahamu hili.
 
Binafsi mimi sina tatizo na wewe ila nataka kufahamu wewe ni nani, maana mimi nawza kuwapata na kugharima vijana kama 100 na wazee kama 100 jumla mia mbili issue ni kwamba this has to come through a trusted source.

Peoples Power.

Issue ni kufikisha ujumbe.... Kwahiyo mimi am just a normal person mlalahoi tu wakaida, nimefikilia kuhusu ili jambo, na nikaona kuna uwezekano wa watu kukusanya majina ambayo yatakuwa kwenye hiyo email; na nitaforward hapa jamvini. Hili sio suala langu ni la kila mtu.. Petition inatoka kwa wananchi wote sio kwangu tu. I am not important just a mediator au call me mtoa wazo tunaweza tukaboresha kama kuna mtu ana wazo zuri
 
Back
Top Bottom