Maendeleo mapya: Mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Uzalendo

Maendeleo mapya: Mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Uzalendo

Mh huyu anasema, hakuna hitaji la lazima la katiba mpya ambayo kupatikana kwake ni gharama, mbali ya changamoto nyingine za ujenzi wa taifa. Tunamuuliza kazi za ujenzi wa taifa kwake na serikali yake wananazo zionaz ni muhimu kuliko hii ya katiba ni kununua mashangingi ya billioni 9? Na wamesha sahau kuwa kabla ya uchaguzi walituambia magari ya gharama sasa basi wataelekeza matumizi ya serikali serikali katika kuwahudumia walalalahoi wa nchi hii na tukaona matrekta ya kilimo kwanza, wamerudi kulekule kwenye matumizi ya anasa kazi ipo.

Anasema serikali haiko tayari kuanzisha mchakato wa kupata katiba mpya kwani hawaja pokea maombi kwa kufuata utaratibu kwa wenye madai (wananchi). Hivi hii ni serikali ya aina gani ya wananchi au serikali ya watawala? kwa maana anatuambia kuwa hawaoni kilio cha wananchi wao.

Anasema serikali isilazimishwe kushuhulikia suala hili nyeti kwa kupitia magazeti(sina hakika kama vyombo vingine vya habari anavichukulia je hapa?). Kama serikali inajua kuwa ni suala nyeti. kwanini inachezea suala nyeti?

Anasema kwamba shauku ya mabadiliko ya jumla ya katiba hayako kwa maslahi ya wananch na serikali, ila hasemi ni wapi, lini na vipimo vipi wametumia kujua kutokuwepo kwa shauku hiyo. Sasa kwa hili tunamuabia Waziri huyu kuwa awe mkweli wa nafsi yake na serikali, asiwa semee wananchi. Atuambie hivi mabadiliko hayatakuwa na maslahi kwa watawala, mafisadi na wachakachuaji maslahi ya watanzani. Kwani kwao wao katiba mpya ni kujitengenezea anguko lao kwa mikono yao wenyewe.

Kwa kauli za aina hii za viongozi wa serikali kunakila sabaubu ya wananchi walio wengi ambao ndio watanufaika kwa kupatikana katiba mpya, kuamini kuwa katiba mpya haitakuja bila ya kutumika nguvu ya umma.
 
The more wanavyochelewesha japo kukubali mjadala the more wanajiweka kwenye loosing side. When time comes na wao kukubali watakuwa hawana cha kujivunia kwani itaonekana ni nguvu ya umma au upinzani

Jakaya and CCM wake up
 
Ogopa nchi ambayo number of graduates is greater than number of employments available in a given year....................
 
Shivji aponda Baraza la Mawaziri
• Aonya bila Katiba mpya, yatatokea ya Kenya

na Hellen Ngoromera


amka2.gif
MWANAZUONI na mwanaharakati mashuhuri nchini, Profesa Issa Shivji, ameibuka na kulikosoa Baraza jipya la Mawaziri kuwa ni kubwa na halikuwa na haja ya kuwa na Naibu Mawaziri. Shivji aliyasema hayo juzi usiku jijini Dar es Salaam wakati akizungumza katika kipindi cha ‘Channel Ten on Monday’ kuhusu uundwaji wa Baraza la Mawaziri.
“...Hakukuwa na haja ya Naibu Mawaziri, kazi yao ni nini? Tuwe na makatibu wakuu wenye msimamo wanaojua kazi yao na wanaoweza kusema hili haliwezekani mheshimiwa na huko nyuma walikuwepo,” alisema Profesa Shivji.
Shivji ambaye ni Profesa wa Kigoda cha Taaluma cha Mwalimu Nyerere katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), alisisitiza kuwa mawaziri wengi ni mzigo na idadi haiendani na hali halisi ya umaskini wa taifa.
Alisema mawaziri si watendaji bali hushughulika na sera na kilichotakiwa ni kuwa na mawaziri wachache ambao ni wachapa kazi.
Akijibu swali la mtazamaji wa kipindi hicho aliyetaka kujua ikiwa kuna uwezekano wa wasomi kumshauri rais kuhusu ukubwa wa baraza hilo, Profesa Shivji alisema kila mwananchi ana wajibu wa kuzungumza kutoa maoni yake na kumshauri rais.
“Huwezi kutoa ushauri kama hujaombwa na kuna wengine wanaombwa ushauri lakini kutokana na siasa zetu hutoa ushauri wa kujipendekeza, sasa...,” aliishia hapo Profesa Shivji kisha kucheka.
Kuhusu madai ya Katiba mpya Profesa huyo aliishauri serikali kutosubiri machafuko yatokee kama ilivyokuwa Kenya na kuitaka ianzishe mchakato wa Katiba sasa.
Alisema ili kushinikiza suala hilo kuna haja ya kuwepo kwa mjadala mkubwa wa kitaifa ambao utawashirikisha pia wananchi kwani suala hilo ni la jamii nzima.
Alisema suala la kudai Katiba mpya halikuanza leo bali tangu kuingia kwa mfumo wa vyama vingi lakini hadi leo hakuna kilichofanyika.
Pia aliikosoa serikali kwa kuwasahau wakulima na kushindwa kuwaundia wizara yao huku akisisitiza kuwa ‘wakulima ni watu muhimu’.
Alisema ikiwa nchi inataka kuendeleza kilimo lazima itilie mkazo kwanza umwagiliaji vinginevyo utachukuliwa na soko la uwekezaji.
Alizungumzia pia suala la huduma za mikopo na kuitaka serikali isimame kidete katika kuwapatia mikopo wananchi kuliko kuyaachia mabenki kufanya shughuli hiyo.
 
Wana JF ukiona bomu linatoa moshi jua kabisa sekunde chache litalipuka. Namaani fukuto la katiba mpya lililoanza kufukuta hapa kwetu lazima litazaa katiba mpya naamini. Lakini lazima tuendelee kujiuliza, hivi matatizo yetu kisiasa, kiuchumi na kijamii yatatatuliwa kwa kuwa na katiba mpya tu? Hata mi pia nahitaji katiba mpya hata kesho.
 
Kunatofauti kubwa ya kufuata sheria na kufuata Taratibu,, Kwasababu Taratibu huwekwa na watu wachache ambazo ukizifunja taratibu hizo unarekebishwa hapohapo bila kusubiri nani aje, kwamfano utaratibu wa kuvua viatu wakati wa kuingia Msikitini, ukiingia msikitini watu wengine wote watakushangaa na Mmoja wapo atainuka na kukueleza kwa ustaarabu kuvua na kwenda kutawadha ili uendelee na swala, kama watatumia nguvu basi wao hawana Elimu ya Dini ya kutosha.

Lakini Sheria ni tofauti na Taratibu hapa kwetu, Kwa nchi za wenzetu unaweza kuvunja sheria na hakuna mtu hata mmoja eneo lile lakini kesho unaletewa Barua unaitwa kituo cha polisi ukajibu shitaka na kupangiwa Fine palepale inayo kuhitaji ulipe kwa muda Maalumu..

Tanzania tunaingiza masihara hata kwenye Katiba ya Sheria yetu,, kwasababu hata wao wanaojua Sheria wanazivunja kwa makusudi wakati wao wanazifahamu,, Watanzania tumekuwa mambumbumbu kufuatili9a Sheria na Taratibu na Hata katika kudai haki
KATIBA INAHITAJIKA
 
ASASI za kiraia zimeitaka serikali kuyatilia maanani madai ya Katiba mpya na kuanzisha haraka mjadala wa kitaifa kufanikisha upatikanaji wa Katiba hiyo.
Madai hayo yanayozidi kushika kasi kila kukicha, jana yalichukua sura mpya baada ya kusisitizwa mbele ya wawakilishi wa nchi wafadhili wanaohudhuria mdahalo wa kitaifa kuhusu sera uliofunguliwa na Waziri wa Fedha, Mustapha Mkulo, katika Hoteli ya Blue Pearl, jijini Dar es Salaam.

Akiwasilisha msimamo na mapendekezo ya awali ya asasi za kiraia kwa maboresho ya sera za nchi, mwakilishi msemaji wa asasi hizo Moses Kulaba, alisema hitaji la katiba bora lililoanza kuibuliwa na wanaharakati kabla na baada ya kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi, sasa ni suala lisiloepukika kwa mustakabali wa taifa hili.

Kwa niaba ya asasi hizo, Kulaba alionya kuwa amani na usalama ambao Tanzania imekuwa ikijivunia inaweza kuwa hatarini ikiwa serikali haitasikia kilio cha mapungufu makubwa yaliyoko katika Katiba ya sasa.

Akiiponda Kataba ya sasa na kugusia jinsi inavyokwamisha utawala bora na maendeleo ya haraka, alisema, “Ni ukweli ulio dhahiri kwamba Katiba yetu ya sasa ni moja ya mambo yanayokwamisha utawala bora na wenye uwajibikaji. Kwa upande mmoja imebeba vifungu vinavyokwamisha uwepo wa mgawanyo mzuri wa kimadaraka baina ya mihimili mikuu mitatu ya dola na wakati huohuo vikikwamisha uwajibikaji kwa kusababisha kuwepo kwa mgongano wa kimaslahi baina ya viongozi.

“Kwa upande mwingine Katiba ya sasa inatoa mamlaka makubwa sana kwa wakuu wa nchi, hivyo inaathiri uhuru na wajibu wa idara na taasisi muhimu kama TAKUKURU katika kushughulikia masuala ya rushwa na ufisadi na kuikwamisha Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) katika kusimamia uchaguzi huru na wa haki.

“Mchango na wajibu wa kila mdau katika kufanikisha uwepo wa Katiba mpya ni muhimu mno kwa majaaliwa mema ya taifa na kuhakikisha hatua zilizopigwa katika MKUKUTA na MKUZA zinafanikiwa na kuwa endelevu.”

Kisha, aliongeza, “Zanzibar imeonyesha njia ni wakati wa Tanzania sasa kwa ujumla wake kufanya hivyo. Hatuwezi kuliacha suala hili lionekane kama ajenda ya kisiasa tu au vita baridi ya kisiasa baina ya vyama vya siasa, hapana. Hili ni suala lenye maslahi kwa taifa zima na linahitaji wajibu wa kikamilifu wa raia kulifanikisha.”

Awali Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, akitoa hotuba yake ya ufunguzi, aliwataka wadau kutekeleza changamoto zilizopo katika kuweza kutekeleza Mpango wa Pili wa Kupambana na Umaskini na Kukuza Uchumi (MKUKUTA), ili kuweza kuinua uchumi wa taifa kutoka asilimia 7 kwa mwaka na kuweza kufikia asilimia 10.
 
Well said: na kwa mtaji huu endapo mtu yeyote, kikundi au taasisi yoyote ile ITAKAYODIRIKI kusimama mbele au kuonekana kikwazo kwa 'UMMA WA TANZANIA' kutaka kutekeleza WAJIBU wao wa msingi katika KUANDIKA UPYA mkataba wa kiutawala (KATIBA) kati yao na WATAWALA wa leo na wa siku zijazo, basi itakua ni juu yao kujilaumu milele endapo watakubwa na dhoruba isiyokifani toka kwa wananchi kwani swala la MABADILIKO YA KWELI kutokomesha UFISADI wa kitusha nchini mwetu NI SASA na wa sio KESHO!!!
 
Ndugu zanguni wanaJF na watanzania wenzangu popote pale mlipo; ingawa nimejawa na hofu kubwa, bado kisima changu cha matumaini hakijaanza kukauka. Bado nimejawa na matumaini kuwa-tukiiunganisha nguvu zetu, kwa pamoja tunaweza kabisa tukaepusha "inevitable death" ya nchi yetu.

Maana, Tanzania ikifa, maiti yake itanuka vibaya sana (na nisingependa hilo litokee)!

And so, badala ya kupiga porojo hapa jukwaani na kupeana matumaini ya uongo kuwa ipo siku CCM (kwa hiari yake yenyewe), itashika adabu na kuanza kujiheshimu hata kutupatia Katiba Mpya, sasa ni wakati muafaka wa kuanza rasmi mchakato wa kudai Katiba Mpya!

Sasa ni wakati wa kufikiria na kufanya mambo makubwa ambayo hayajawahi kujaribiwa au kufanyika nchini mwetu. Mambo kama vile-kuishinikiza Serikali dhalimu ya CCM iruhusu na ikubali madai yetu ya Katiba Mpya.

Nashauri kwanza tuanze na njia ambayo ni rahisi kushinda njia zote.

Njia ya Petition.

Hilo likishindikana, then tutaruka kwenda hatua nyingine-hatua kali zaidi kuliko hii ya petition (naomba nisiizungumze hapa kwasasa-maana najua makachero wa-CCM watairukia na kuanza kuifanyia kazi/kubuni mbinu za kutukabili).

Katiba ya sasa ina mapungufu mengi mno, na yafuatayo ni mambo ambayo ningependa kuona yanafanyiwa mabadiliko:

(1). Mawaziri na manaibu waziri wateuliwe toka nje ya Bunge
(2). Wakuu wa mikoa wapigiwe kura moja kwa moja na wananchi wa mikoa yao
(3). Serikali iruhusu wagombea binafsi (Independent candidates)
(4). Madaraka ya Rais yapunguzwe (kuna mjadala mrefu hapa)
(5). Katiba iruhusu matokeo ya Rais kupingwa mahakamani
(6). Kila mkoa uwe na mwanasheria mkuu wake
(7). Mkuu wa Tume ya Uchaguzi (NEC) asiteuliwe na Rais
(8). Cheo cha mkuu wa wilaya kifutwe (badala yake Mkungenzi wa maendeleo, apewe madaraka hayo)
(9). Kuwe na idadi kamili ya Wizara katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mfano 20, na itamkwe bayana kwenye Katiba. Rais asiruhusiwe kuongeza ama kubadilisha miundo ya Wizara hizo.
(10). Idadi ya Mikoa, Wilaya na Majimbo itamkwe rasmi kwenye katiba (utaratibu wa sasa wa kuongeza wilaya/mikoa ovyoovyo usitishwe mara moja).
(11). Wawakilishi wa wananchi (Wabunge) wasiwe na uwezo wa kukaa na kujipangia malipo wanayotaka walipwe. Kadhalika wanasiasa wote walipe kodi kama wananchi wengine.
(12). Kwenye Sheria ya Uchaguzi, kila kituo kitangaze matokeo ya kura za mgombea baada ya kuthibitishwa na mawakala wa vyama vilivyoshiriki pamoja na msimamizi au msimamizi msaidizi. Matokeo hayo yakishatangazwa, basi yahesabike kuwa matokeo rasmi.
(13). Rais atangazwe mshindi endapo tu kama atapata kura zaidi ya asilimia hamsini (50%). Vinginevyo, runoff election iitishwe within 90 days.
(14). Uteuzi muhimu kama vile majaji na Mkurugenzi wa PCCB uthibitishwe na Bunge
(15). Suala la kupita bila kupingwa liondolewe
(16) Mikataba yote inayohusu maliasili za nchi yetu (Madini, gas, ardhi, mafuta); ijadiliwe na kupitishwa na Bunge
P.S. Unaweza ukaongezea mambo mengine ambayo ungependa kuona yanafanyiwa mabadiliko kwenye hii Katiba Mpya tunayodai (ukisha sign petition, weka comment ya jambo unalotaka kuona linafanyiwa marekebisho).

Ushirikiano wenu nyote unahitajika. Saini petition hapa: TUNAHIHITAJI KATIBA MPYA Petition
 
waziri wa sheria amesema kuwasilisha mapendekezo ambayo tunataka iwe katiba mpya,na iwapo tume haitakuwa chini ya serikali itaripwa na nani? Alihoji.na amesema walishajaribu kufanya hivyo watu wakawa wanakimbia na masanduku ya kura na hamna wa kuwachukulia hatua za kisheria kwa sababu hawako chini ya serikali,kwahiyo tume huru tunataka iwe ya namna gani?
 
(9). Kuwe na idadi kamili ya Wizara katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mfano ziwe 20, na itamkwe kwenye Katiba. Rais asiwe ma mamlaka ya kubadilisha idadi ya Wizara. Pia hakuna haja ya manaibu waziri. Ateue tu watu kuwa mawaziri katika Wizara hizo zilizotamkwa kwenye Katiba. Kila waziri mteule ajadiliwe na kuhojiwa na Bunge (au Kamati ya Bunge), na Bunge liwe linapokea habari kutoka kwa watu kuhusu kila waziri mteule (namaanisha kufanya 'vetting') kabla ya kumpigia kura ya kumkubali au kumkataa kila Waziri mteule mmoja baada ya mwingine.

(10). Idadi ya Mikoa, Wilaya na Majimbo itamkwe rasmi, na pasiwe na usanii wa kuyaongeza ili kuwapatia 'washkaji' nafasi za kutawala. Sanasana inaongeza administrative costs na kumbebesha mzigo mlipa kodi.

(11). Wawakilishi wa wananchi (Wabunge) wasiwe na uwezo wa kukaa na kujipangia malipo wanayotaka walipwe. Hivi sasa wanaweza kukaa na kubuni VIKAO VYA KAMATI (vinafanyika vingi tu) na kuanzisha MIFUKO YA BUNGE ili kuongeza kipato chao ambacho tayari ni kikubwa sana.

(12). Kwenye Sheria ya Uchaguzi, kila kituo kitangaze matokeo ya kura za mgombea baada ya kuthibitishwa na mawakala wa vyama vilivyoshiriki pamoja na msimamizi au msimamizi msaidizi. Matokeo hayo yatangazwe na yahesabike kuwa ni rasmi, kwani yatakuwa ndiyo rasmi.
 
(9). Kuwe na idadi kamili ya Wizara katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mfano ziwe 20, na itamkwe kwenye Katiba. Rais asiwe ma mamlaka ya kubadilisha idadi ya Wizara. Pia hakuna haja ya manaibu waziri. Ateue tu watu kuwa mawaziri katika Wizara hizo zilizotamkwa kwenye Katiba. Kila waziri mteule ajadiliwe na kuhojiwa na Bunge (au Kamati ya Bunge), na Bunge liwe linapokea habari kutoka kwa watu kuhusu kila waziri mteule (namaanisha kufanya 'vetting') kabla ya kumpigia kura ya kumkubali au kumkataa kila Waziri mteule mmoja baada ya mwingine.

(10). Idadi ya Mikoa, Wilaya na Majimbo itamkwe rasmi, na pasiwe na usanii wa kuyaongeza ili kuwapatia 'washkaji' nafasi za kutawala. Sanasana inaongeza administrative costs na kumbebesha mzigo mlipa kodi.

(11). Wawakilishi wa wananchi (Wabunge) wasiwe na uwezo wa kukaa na kujipangia malipo wanayotaka walipwe. Hivi sasa wanaweza kukaa na kubuni VIKAO VYA KAMATI (vinafanyika vingi tu) na kuanzisha MIFUKO YA BUNGE ili kuongeza kipato chao ambacho tayari ni kikubwa sana.

(12). Kwenye Sheria ya Uchaguzi, kila kituo kitangaze matokeo ya kura za mgombea baada ya kuthibitishwa na mawakala wa vyama vilivyoshiriki pamoja na msimamizi au msimamizi msaidizi. Matokeo hayo yatangazwe na yahesabike kuwa ni rasmi, kwani yatakuwa ndiyo rasmi.
Mkuu Guevara, those are some great points. Nitaziongeza wenye hard copy ya petition (kwa ruhusa yako lakini)
 
Mkuu(Bongo TZ) hivi kuna Petition mbili? hebu check again niliyoiona jana watu karibu 90 walikua wamesha sign hii ya leo naona 3 tu vp??
 
Back
Top Bottom