Maendeleo mapya: Mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Uzalendo

Maendeleo mapya: Mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Uzalendo

MJADALA wa kuwepo kwa mabadiliko ya Katiba umeibuka tena. Mjadala huu umekuwa ukiibuka na kuzimwa na Serikali mara kwa mara. Lakini hivi karibuni baada ya Rais Jakaya Kikwete kumteua Celina Kombani kuwa Waziri wa Katiba na Sheria, swali kubwa kwake limekuwa ni kuhusu mabadiliko hayo.

Hata hivyo, Kombani ameonyesha kutokuwa na dhamira ya kusimamia mabadiliko hayo. Hivi karibuni alikaririwa akisema kuwa kama kuna watu wanataka mabadiliko hayo wapeleke mapendekezo hayo ofisini kwake lakini akasema mabadiliko hayo yatagharimu fedha nyingi ambazo kwa sasa serikali za kutosha kuyafanikisha.

Kutoka na majibu hayo, wanasheria kadhaa wamejitokeza na kueleza haya ya serikali kusimamia mabadiliko hayo. Mhadhiri wa Sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Chris Maina anasema mabadiliko ya Katiba hayahitaji mapendekezo wala shinikizo bali, ni jukumu la serikali kuyafanya.

“Mabadiliko ya Katiba siyo lazima yaletwe mapendekezo, Serikali yenyewe inapaswa kufanya. Mbona mabadiliko ya 14 yalifanywa na serikali yenyewe. Kulikuwa na mabadiliko mwaka 2005 ambapo serikali iliingiza vipengele vya haki za binadamu bila kushinikizwa na mtu yoyote, kwa hiyo Serikali isisubiri mapendekezo” anasema Profesa Maina.

Profesa Maina anasema kuwa vuguvugu la sasa la kutaka kuwepo kwa Katiba mpya ni sehemu ya madai ya siku nyingi ambayo huibuka mara kwa mara na kuzimwa bila ya kuangaliwa kwa undani na kupewa majibu ya kuridhisha. Kwa sababu hiyo anasema madai hayo yataendelea kuibuka kwa namna moja au nyingine.

“Kwa kukumbushia tu wakati wa Tume ya Mheshimiwa Jaji Mkuu Nyalali ya mwaka 1991 kuhusu mfumo wa vyama vingi na ambayo ilipendekeza kuanzishwa kwa mfumo wa utawala wa vyama vingi vya siasa kulikuwa na hoja nzito tu kwamba mfumo huo mpya wa vyama vingi ulihitaji Katiba mpya na siyo kurithi hiyo Katiba ya chama kimoja ambayo mihimili yake ilikuwa tofauti kabisa. Hoja hizi hazikupewa majibu na vyama vingi vya siasa viliingizwa ndani ya Katiba ya mwaka 1977 kupitia Mabadiliko ya Nane ya mwaka 1992. Mabadiliko haya ya Katiba yalitungiwa pia Sheria ya utekelezaji – Sheria ya Vyama vya Siasa Namba 5 ya 1992.”

Anakumbushia pia Kamati ya 'White Paper' iliyoundwa chini ya Jaji Dk Robert Kisanga mwaka 1998, akisema wananchi waliibua tena suala la Katiba mpya... “Kamati ilipowasilisha Ripoti yake ilikemewa eti imevuka mipaka yake kwa sababu ilikuwa Kamati na siyo Tume. Hapa tena suala la Katiba mpya likawekwa chini ya mkeka.”

Akizungumzia madai ya sasa, Profesa Maina anasema kuwa suala hilo limechukua sura ya mikakati ya vyama vya siasa huku baadhi yao vikilichukua kama sehemu ya ilani zao za uchanguzi na kuahidi wananchi kuunda Katiba mpya. Anakumbushia hotuba ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa aliyoitoa katika Mkutano wa Mwaka wa chama cha Mawakili wa Afrika Mashariki (EALS) uliofanyika Bujumbura, Burundi Novemba19 na 20, mwaka huu... “Aliifananisha Katiba ya nchi na roho katika mwili wa binadamu na kusisitiza haja ya kuwa na Katiba bora.

Profesa Maina anasema ni vizuri kuona viongozi waliotoka madarakani wanatafakari na kuona vizuri baadhi ya vitu ambavyo hawakuvipa umuhimu wakati wakiwa bado ofisini.

“Vilevile inafaa iwe funzo kwa viongozi walio madarakani kushughulikia matatizo yanayowakera wananchi kama vile kuwa na Katiba isiyoridhisha. Haitoshi kukaa ofisini kusubiri malalamiko ya vikundi vya kiraia au vyama vya upinzani ili uyafanyie kazi. Wizara husika inatakiwa iwe msitari wa mbele (pro-active) katika kutoa mapendekezo ya kuboresha Katiba na ndiyo maana inaitwa Wizara ya Katiba na Sheria,” anasema Profesa Maina.

Mwanasheria Mkuu wa zamani wakati wa Serikali ya Awamu ya Kwanza, Jaji Mark Bomani naye anasisitiza kuwepo na mabadiliko ya Katiba. Anasema Katiba iliyopo sasa ina umri wa miaka 50 hivyo imepitwa na wakati.

“Ni kweli, Katiba yetu sasa inatakiwa ifanyiwe marekebisho ya jumla. Ni Katiba yenye umri wa karibu miaka 50 na chimbuko lake ni tangu uhuru. Ilifanyiwa marekebisho mwaka 1979 na mwaka 1992 wakati tunaingia kwenye mfumo wa vyama vingi.
Lakini sasa mazingira yamebadilika watu wamejifunza mengi kutoka sehemu tofauti.

"Umefika wakati sasa wa kuibadilisha yote na kazi hiyo ishirikishe wadau wote. Serikali ikae kitako na wadau wote ili kujadiliana kuhusu mabadiliko hayo. Hii ndiyo njia pekee ya kujibu malalamiko ya vikundi mbalimbli. Serikali inapaswa kuunda jopo litakaloratibu mchakato mzima wa kuundwa kwa Katiba mpya. Ningependekeza kuwe na ‘comprehensive review’. Siyo kila mtu alete mapendekezo yake, itakuwa ni vurugu tupu,” anasema Jaji Bomani.

Bomani anaeleza chanzo cha serikali kusuasua kukubali mabadiliko ya Katiba akisema kuwa ni woga wa viongozi waliopo madarakani...
“Ni woga tu, wanaona woga kwa sababu hawajui kitakachojadiliwa na kupitishwa kitakuwa nini kama wakiwapa watu uhuru wa kujadili. Lakini nadhani njia bora ni serikali kukaa kitako na wadau ili kupata maendekezo yao kuhusu mabadiliko hayo.”

Mwanasheria na wakili wa Mahamama Kuu ya Tanzania, Profesa Abdallah Safari anasema madai hayo ni ya muda mrefu lakini serikali imekuwa ikiyapuuza. Anakumbushia rasimu ya Katiba iliyokuwa ikiandaliwa na vyama vya upinzani vikiongozwa na CUF akisema kuwa hayo yalikuwa ni mapendekezo mengine ya mabadiliko ya Katiba ambayo yameshafika serikalini.

Profesa safari aliyewahi kutoa kitabu kinachoeleza haja ya Tanzania kuwa na tume huru ya uchaguzi anasema kuwa Serikali inaogopa mabadiliko ya Katiba kwa sababu yataleta tume huru ya uchaguzi na hapo ndiyo utakuwa mwisho wa ushinndi wa CCM... “Hao wanaogopa Katiba mpya kwa sababu wanajua kuwa italeta tume huru ya uchaguzi na hapo hawatashinda tena. Watashindaje wakati hawakubaliki?”

Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) Felix Kibodya anasema kuwa pamoja na madai hayo kuwa ya muda mrefu bado wanampa nafasi Waziri Kombani kujipanga kwani ndiyo kwanza ameingia ofisini. Hata hivyo, anasisitiza kuwa madai hayo ni ya msingi na kwamba wanaandaa mapendekezo mengine ambayo watayapeleka kwa Waziri ili yafanyiwe.

“Kama tulivyotoa taarifa yetu kuhusu uchaguzi, tutaandaa mapendekezo yetu na tutayapeleka kwa waziri. Kwa kweli hata sisi tunahitaji mabadiliko ya Katiba” anasema Kibodya.
 
Kweli bwana Nkapa.Maana bila katiba mpya hata Mahakama ya Qadhi haitapatikana
 
Hivi itakua sawa kila kikundi kwenda kukutana na Mzee Tyson Stephen Wassira kisirisiri kila kimoja kwa wakati wake au iweje kiuhakika kuhusiana na madai ya wananchi kutaka mabadiliko???

Je, kwa mtindo huo tutapona kwa kuhaha kwao mafisadi kujaribu kupenyeza vijisent kila kuna kuyumbisha jitihada za mabadiliko nchini??
 
Katiba mpya itafungua Pandora's box ya muungano.

Watanganyika(watanzania bara) tumechichipaa, tunajitutumua, tumepandisha sauti zetu kwa ghafla baada ya uchaguzi mkuu na hasa baada ya kuona au kuhisi kuwa tumefanyiwa hujuma katika matokeo ya ngazi mbali mbali kwa nafasi tulizokuwa tukigombania, kuanzia, udiwani, ubunge na urais.

Kama hatukuwa tunajidanganya nafsi zetu, roho zetu, kuna aliyeamini kwa dhati kabisa kuwa chini ya katiba iliyopo na tume ya uchaguzi iliyopo kuwa zingelitutendea haki na usawa?

Baada ya kila uchaguzi mkuu, suala la kudai mabadiliko ya katiba hujitokeza, sasa tumelenga zaidi, tunaelekeza nguvu zetu katika kuiandika katiba upya na sio kuitia viraka. Hii ni hatua nzuri.

Kwa mijadala ninayoifuatilia, ninayoisikia sioni kama tumejiuliza tutaipataje katiba mpya. Baada ya Wazanzibar kuwa pamoja(sio wamoja) na kuunda GNU kule Zanzibar.Vugu vugu lote la kudai katiba mpya limehamia Tanzania bara(Tanganyika). Kule Zenj wanajaribu kuekana sawa katika GNU yao. Sasa mechi inachezwa upande wa pili wa TZ.

Tuliipataje hii katiba inayotumika sasa?
Nani aliipitisha kuwa katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania?
Kuna atakaesoma hapa na kusema "kwenda zako huko! Sisi tunataka katiba mpya tu"

Ni sawa, hata mimi naitaka katiba mpya leo kabla ya kesho. Lakini ninataka tu tuipate katiba hii mpya kama Katiba ya Tan-Zan-ia na sio ya Tan-ia pekee. Sasa hivi, tunadai katiba mpya kama Tanzania bara(Tanganyika) na sio kama Tanzania. Hili tulione mapema vyenginevyo hiyo katiba yetu mpya itatuletea mambo mengine ambayo kwa sasa tunayafumbia macho. Tuwashirikishe na wenzetu wa Zenj ili tuweze kupata katiba imara,inayolinda na inayowapa haki zao katika muungano wetu. Tusiwe na mawazo ya kutaka haki kwetu tu pale tunapoona haki yetu imedhulumiwa lakini kuwa tayari kuzikanyaga haki za wengine. That is morally wrong.


CCM na Serikali zake zisingepata kigugumizi sana katika kukubaliana na upinzani na wadau wengine kuandika katiba mpya, hasa baada ya uchaguzi uliomalizika, kwani CCM imetambua kuwa nguvu za upinzani zimekitikisa, mara hii hakukuwa na Tsunami wala ushindi wa kishindo. Na hata baada ya kutangazwa washindi, wapinzani walipotaka kufanya mikutano yao, polisi walisema kuwa hali bado si shwari.

La pili ambalo linaipa CCM na serikali zake kigugumizi katika hili la katiba mpya(brand new, man! sio viraka)ni kuwa ile sera yao ya kutoka serikali mbili kuelekea serikali moja. Tafsiri sahihi hapa ni kuwa kazi ya kuimeza Zanzibar haijakamilika. Ingekuwa imekamilika basi sura ya mjadala wa katiba mpya leo usingekuwa mgumu sana kama ulivyo leo. Ndio maana wao wanataka waendelee kutia viraka na tuendelee kutumia hii iliyopo sasa.

Huko juu nimeuliza suali; Jee kuna mtu anajua vipi hii katiba tuliyonayo tuliipata? Kama huna jawabu, do your home-work Mkuu!Kwani tutakapokuwa tunaandika hiyo mpya tunahitaji kuyazingatia hayo.

CCM hawako tayari kuifungua Pandora's box ya muungano. Na hili nafikiri vyama vya upinzani vilivyojikita zaidi huku Tanzania bara hawajaliona au wanalijua lakini wanajifanya "vipofu". Kwa nini nasema hivi?

CHADEMA chama mahiri kabisa baada ya uchaguzi uliomalizika wanahoji kama mabadiliko waliyofanya Wazenj kuwa yanakiuka katiba ya Muungano. Inawezekana wana hoja ya msingi hapa. Lakini watu hawa walikuwa wapi katiba ya muungano ilipofanyiwa mabadiliko,kumuondoa,kumuengua rais wa zenj kuwa makamu wa rais wa TZ ili kuwa waziri asiye na wizara katika baraza la mawaziri la TZ? Hatukulipinga hili na kusema tunaudhoofisha muungano na pia tunaichakachua katiba na "the articles of Union".


Sio CHADEMA tu, bali sisi sote huku Tanzania bara tuliona CCM wamefanya sawa tu, jambo zuri tu. Wenzetu wa Visiwani walipiga kelele sana, including CCM Zenj, kelele zao zikawa ni kelele za mlango...
Hii project ya kui-annex Zanzibar haijakamilika na sisi sasa tunapiga kelele lazima tupate katiba mpya. Ninawaambia,Katiba mpya itafungua pandora box.Tutakayoyakuta humo tukae tayari.

La kushangaza mara hii, hakuna katika CCM aliyekuja na madai kuwa Wazanzibar wamekiuka katiba ya muungano kwa mabadiliko waliyofanya katika katiba ya Zanzibar. In fact, waliojitikeza kutoa ufafanuzi ,wametetea kuwa hakuna kosa kwa waliyofanya wazenj, tofauti na ilipotokea « saga » ya OIC.

Ugumu wa kuipata katiba mpya kwa TZ ,hasa kwa kuifanya CCM mmoja wa wadau, umeongezeka, kwa sababu CUF sasa wamo ndani ya Serikali kule Zanzibar, kwa hiyo wanasauti isiyoweza kupuuzika kama zamani.

Well, nisikuchoshe sana kusoma makala refu, jee uko tayari kuifungua Pandora's box ?Tumeshajitayarisha kumuona na kumsikia mama yetu , Tanganyika humo ndani ya Pandora's box akilia, akitulalamikia kwa nini tulimfungia humo, tulimsahau humo kwa muda mrefu? Atatupigia magoti na kutusujudia,kutuomba tumtoe humo, Tutafanya nini hapo wakati leo, hata uhuru tunasherehekea uhuru wa Tanzania na siyo uhuru wa mama yetu, Tanganyika? Tunaona haya kusema « mimi ni Mtanzania, mtanganyika. »

Katiba Mpya hiyo !! Mimi nataka tuidai katiba mpya lakini pia nataka tusimamie haki ya « kajisehemu kadogo » kanakotupa ufahari wa utaifa wetu. Wakiamua kuiondoa Zan, yao tutabaki na jina « Tania ».

Watawala wetu wametumia umbumbumbu wetu, uchovu wetu wa kufikiri kutufikisha hapa tulipo. Wametuzuga ili tuwaone Wazenj kuwa ni « toto tundu » na hivyo kuwaona ndio sababu ya matatizo yetu, na mashaka tunayokumbana nayo. Tumeondoa focus yetu kutizama m-baya wetu, na kumtambua « mchawi » halisi.

Amka mkuu, uko katika usingizi wa pono bila kujitambua.

Wachina wana msemo wao kuwa « safari ya maili elfu ni lazima ianzie kwa kupiga hatua ya kwanza. »

Tujipongeze leo kwa kusherehekea uhuru wa Tanganyika yetu !!na itakapofika april tusherehekee Muungano wa Jamhuri ya Tanzania. Tuondoe confusion hii katika bongo zetu.


PS, MwanaFalsafa1, ukiisoma hii na kuifahamu utajuwa kwa nini mimi napendelea mfumo wa Muungano wa serikali tatu au mfumo wa one country, two systems (Hong kong-China).
 
Nilikuwepo newsroom prof shivji amezidi kuiua serikali ya jk kwa kusema katiba mpya ndio msingi wa mambo yote na kwamba kilio cha kudai katiba mpya ya wananchi hakijaanza leo kilianza siku nyingi wakati wa mchakato wa vyama vingi. Amesema katiba ya sasa ni ya kulinda maslahi ya vigogo wachache sio katiba ya kumkomboa mtanzania na kwamba katiba hii haikuundwa na watanzania bali kikundi cha watu wachache. Alisisitiza kwamba bila katiba mpya hakutakuwa na maendeleo yoyote. Ameweka bayana kuwa nchi ya tanzania haihitaji manaibu mawaziri na pia haihitaji wizara zaidi ya 20. Huyu ni mwiba kwa mafisadi na ccm ni mtu safi na anaongea ukweli bila woga
 
Nilikuwepo newsroom prof shivji amezidi kuiua serikali ya jk kwa kusema katiba mpya ndio msingi wa mambo yote na kwamba kilio cha kudai katiba mpya ya wananchi hakijaanza leo kilianza siku nyingi wakati wa mchakato wa vyama vingi. Amesema katiba ya sasa ni ya kulinda maslahi ya vigogo wachache sio katiba ya kumkomboa mtanzania na kwamba katiba hii haikuundwa na watanzania bali kikundi cha watu wachache. Alisisitiza kwamba bila katiba mpya hakutakuwa na maendeleo yoyote. Ameweka bayana kuwa nchi ya tanzania haihitaji manaibu mawaziri na pia haihitaji wizara zaidi ya 20. Huyu ni mwiba kwa mafisadi na ccm ni mtu safi na anaongea ukweli bila woga

Spot on. Wizara mpaka nyingine sidhani kama zina idara 2. Mfano wizara ya jumuiya ya Afr mashariki ya nini wakati ya mambo ya nnje tunayo. Ujenzi na miundo mbinu haviendi pamoja?
Wizara zapaswa kuundwa kikatiba na kukiwa na haja ya kufuta au kuongeza zijengwe na kuamuliwa bungeni. Ipo haja ya mawaziri kuhojiwa na kuthibitishwa bungeni. Hatupaswi kuwalea mawaziri wenye kashfa za wazi kisa tu wameteuliwa na raisi. Bado twawalipa mishahara.
 
Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Bukoba, Methodius Kilaini, amewataka wanasiasa kuorodhesha mahitaji muhimu yanayotakiwa kwenye mabadiliko hayo, kisha wayapeleke kwao ili nao waongeze nguvu ya mabadiliko.

"Sisi tunawategemea sana wanasiasa watwambie maeneo ambayo yana upungufu, waorodheshe walete kwetu, tutawasaidia kuchochea hili kwani haliepukiki hata kidogo," alisema Askofu Kilaini.
Akitoa mfano alisema, nchi kama Zambia, Malawi Kenya wapinzani waliingia madarakani kisha kubadilisha Katiba, hivyo hata Tanzania inawezekana.

My take: Moto wa katiba unazidi kupanda tusidanganyane mahitaji ya katiba hayaepukiki, kama hatutaongea sasa wakati wa amani tutaongea kubadilisha katiba wakati tukipigana kiasi ambacho kitaharibu hata mtiririko mzuri wa mawazo.

MABADILIKO YA KATIBA: Maaskofu waonya

• Wadai Katiba iliyopo inabeba chama tawala



WAKATI jana taifa lilikuwa linaadhimisha miaka 49 ya uhuru, viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini, wameendelea kuikaba koo serikali kuwa kuna haja ya kufanya haraka marekebisho ya Katiba mpya ili inaendana na mazingira ya sasa.

Viongozi hao, wamesema Katiba iliyopo imepitwa na wakati, ndiyo maana wananchi, wasomi na wanasiasa kila kukicha wamekuwa wakipiga kelele za kutaka mabadiliko baada ya kubaini upungufu mara baada ya kumalizika uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani.

Wakizungumza na Tanzania Daima mjini Dar es Salaam jana kwa nyakati tofauti, viongozi walisema serikali haina budi kukubali matakwa ya wananchi kama ilivyokuwa wakati wa kuanzishwa mfumo wa vyama mwaka 1992.

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Dk. Steven Munga, alisema umefika sasa wa serikali kuona mabadiliko ya Katiba ni sehemu ya maisha ya wananchi.

"Jamii imebadilika, mfumo wa maisha umebadilika… sasa ni wazi kwamba Katiba iliyopo nayo lazima ibadilike, serikali ifikie hatua ikubali jambo," alisema Askofu Munga.

Alisema watu wasiposikilizwa kilio chao kukiwa na amani, wanaweza kuleta mabadiliko ya lazima ambayo yanaweza kuchochea ghasia zisizokuwa na msingi wowote.

"Nakwambia mwandishi kama watu hawakusikilizwa katika mazingira ya amani… wanaweza wakasikilizwa ndani ya mazingira machafuko ambapo hakutakuwa na maelewano kabisa, tunasema hatutaki vita sisi, suala hili haliepukiki hata kidogo," alisema Askofu Munga.

Alisema mabadiliko yaliyofanyika Zanzibar na kuiweka serikali ya umoja wa kitaifa, yanaonyesha wazi kwamba Katiba ya Jamhuri ya Muungano lazima ifanyiwe marekebisho.

"Mtakumbuka kule Zanzibar kumefanyika mabadiliko ambayo yameondoa vyeo kama vile Waziri Kiongozi ambaye alikuwa anatambulika vyema ndani ya Katiba, sasa iweje Katiba ya Jamhuri isifanyiwe marekebisho? Alihoji Askofu Munga.

Naye Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Bukoba, Methodius Kilaini, aliwataka wanasiasa kuorodhesha mahitaji muhimu yanayotakiwa kwenye mabadiliko hayo, kisha wayapeleke kwao ili nao waongeze nguvu ya mabadiliko.

"Sisi tunawategemea sana wanasiasa watwambie maeneo ambayo yana upungufu, waorodheshe walete kwetu, tutawasaidia kuchochea hili kwani haliepukiki hata kidogo," alisema Askofu Kilaini.

Akitoa mfano alisema, nchi kama Zambia, Malawi Kenya wapinzani waliingia madarakani kisha kubadilisha Katiba, hivyo hata Tanzania inawezekana.

Naye Askofu wa Kanisa la GRC la Ubungo Kibangu, Antony Anthony Lusekelo, alisema Katiba mpya lazima ipatikane kwa serikali kuhakikisha inafuata utaratibu wa kushirikisha wananchi kutoa mapendekezo yao.

Alisema kipindi hiki ni muhimu kuwa na Katiba itakayokuwa na mawazo ya kila mdau, kama ilivyokuwa kipindi cha kuanzishwa mfumo wa vyama vingi, ambapo hakuna madhara yaliyojitokeza kwani kila mwananchi alishirikishwa.

"Lazima tuone mbali na serikali ione hilo… ni muhimu katika hili kuhakikisha kunakuwa na mjadala mpana utakaoshirikisha watu wote kama ilivyotokea kipindi cha vyama vingi ambapo kila mwananchi alishirikishwa," alisema Askofu Lusekelo.

Alisema kama Katiba ikipatikana kwa amani, hakutakuwa na madhara, lakini iwapo serikali itapuuza matakwa ya wengi kuna uwezekano wa Katiba kuleta maafa jambo ambalo halipendezi hata kidogo.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (PCT), David Mwasota, alisema suala hilo hivi sasa halina mjadala hasa kwa jamii yenye akili timamu.

Alisema Katiba iliyopo haikuweka ili idumu milele, bali ilitungwa kipindi ambacho hakukuwa na uanzishwaji wa vyama vingi."Hao wanaokataa mabadiliko ya Katiba, wana maslahi yao binafsi, lakini kwa watu walio na maono ya mbali ni lazima ibadilike maana hii iliyopo inakipa nguvu chama kimoja, wakati tuko ndani ya mfumo wa vyama vingi," alisema Mwasota.

Naye Mtume Prosper Ntepa, alisema Katiba si mama wa chama tawala pekee, bali ni kwa ajili ya kusaidia jamii nzima hivyo ni muhimu serikali ikasikiliza kilio hicho ili kuhakikisha kinakidhi mahitaji.
"Serikali isipuuze kilio cha wananchi maana ni kilio halali na kimekuja kipindi husika; ni lazima Katiba ibadilishwe bila kuhofu hasa kwa wale wote wanaoitakia mema nchi na wapenda demokrasia," alisisitiza Ntepa.

Hivi karibuni viongozi mbalimbali walijitokeza kueleza msimamo wao kuhusu kubadilishwa kwa Katiba, akiwemo Mwanazuoni na mwanaharakati mashuhuri nchini, Profesa Issa Shivji, Jaji Mkuu mstaafu Mark Bomani na Rais mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa.

Mkapa ambaye alivunja ukimya na kusema ili kuzuia mifarakano ya kisiasa kwa nchi wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki, zinahitaji kuwa na Katiba mpya, ikiwemo Tanzania. Wakati viongozi mbalimbali wakionyesha nia ya kuhitaji mabadiliko ya Katiba, hivi karibuni Waziri wa Sheria na Mambo ya Katiba, Celina Kombani, alisema hakuna haja ya kuwa na Katiba mpya, kitendo kilichopingwa na watu wengi.

Waziri Kombani alisema Katiba iliyopo itaendelea kutumika kwa vile serikali haina fedha za kufanya maandalizi ya kubadilisha Katiba hiyo.
 
Bahati mbaya maprofesa wengi kama yeye wanakimbilia kwenye siasa, vp na yeye agombee ubunge kwa tiketi ya ccm.
 
Nilikuwepo newsroom prof shivji amezidi kuiua serikali ya jk kwa kusema katiba mpya ndio msingi wa mambo yote na kwamba kilio cha kudai katiba mpya ya wananchi hakijaanza leo kilianza siku nyingi wakati wa mchakato wa vyama vingi. Amesema katiba ya sasa ni ya kulinda maslahi ya vigogo wachache sio katiba ya kumkomboa mtanzania na kwamba katiba hii haikuundwa na watanzania bali kikundi cha watu wachache. Alisisitiza kwamba bila katiba mpya hakutakuwa na maendeleo yoyote. Ameweka bayana kuwa nchi ya tanzania haihitaji manaibu mawaziri na pia haihitaji wizara zaidi ya 20. Huyu ni mwiba kwa mafisadi na ccm ni mtu safi na anaongea ukweli bila woga

Pointi yako nzuri... lakini Profesa Shivji ni Shree Rajneesh Hindu Mandal (= 0% in every single way.) He may not have been born with the genetics of a big-time NBA baller kama Thabeet whoever, lakini trust me, kama angesilimu na kujiita Profesa Shivji-Islam-dunk, bila shaka watu wangemchukulia "serious"...
 
Prof Karim Hirji nae kasema hana imani na JK na Serikali yake...........These guys (Proffs) wamekuwa wakipaza sauti sana recently....There is something wrong somewhere.........
 
Balozi Mbita ataka mabadiliko ya Katiba Thursday, 09 December 2010 20:54

0diggsdigg
BALOZI Hashim Mbita ambaye alikuwa Katibu wa Kamati ya Ukombozi ya uliyokuwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU) amewashangaa wanasiasa wanaoogopa kuifanyia mabadiliko katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akizungumza katika Televisheni ya Taifa jana asubuhi, Balozi Mbita alisema: "Katiba yetu ina ukakasi, hivyo inahitaji kufanyiwa mabadiliko ili iweze kwenda na wakati na mfumo wa kisiasa ulipo sasa na kudumisha umoja wa kitaifa".

Alifafanua kuwa katiba iliyopo inaweka sera za maendeleo mikononi mwa wahisani ambao huamua hatima ya nchi, hivyo kuzorotesha juhudi za maendeleo.


Balozi Mbita alitoa mfano kuwa wafadhili walishawahi kukataa utekelezaji wa Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria mpaka mkoani Shinyanga kwa kuwa haukuwa katika vipaumbele vyao.


Kauli hiyo ya Mbita inakuja wakati kumeibuka mjadala mkali katika jamii kwa wanaharakati na vyama vya upinzani vitaka mabadiliko ya katiba huku viongozi wa chama tawala wakiwemo wabunge na mawaziri wakipinga hatua hiyo.

Hivi karibuni, Waziri wa Sheria na Mambo ya Katiba, Celina Kombani alisema katiba haiwezi kubadilishwa na kwamba hajui madai ya wapinzani kuhusu yanahusu nini na kwamba hawezi kushghulikia kwa vile hajapelekewa rasmi maelezo ya mambi yanayotakiwa kubadilishwa.

Wabunge wa Chadema walisimama na kutoka nje ya ukumbi wa Bunge mara baada ya Rais Jakaya Kikwete kusima ili kutoa hotuba ya kufunga rasmi Bunge la kumi la Jamhuri ya Mungano wa Tanzania wakidai kuwa hawakubaliani na katiba iliyomweka madarakani kwa kuwa ina kasoro nyingi.


Kitendo hicho kiliamsha changamoto mpya katika jamii ya Watanzania wakiwemo vijana na wasomi ambao wanasema sasa umefika wakati wa kuifanyia mabadiliko Katiba kwa manufaa ustawi taifa.


Naye Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Gaudence Mpangala, ambaye alishiriki katika kipindi hicho cha TBC alisema katiba mpya italinufaisha taifa kwa kuboresha misingi ya uongozi bora na siasa safi nchini kwa sababa iliyopo sasa haiendi na wakati, mfumo wa siasa na sera za taifa.

"Tatizo ni kwamba katiba inayotumika sasa ilitungwa mwaka 1977 ambayo ni ya mfumo wa chama kimoja. Katiba hii imeelekezwa katika mfumo chama kimoja, wakati nchi ni ya vyama vingi," alifafanua Profesa Mpangala.


Profesa Mpangala aliongeza kuwa katiba mpya itasadia kuufanya uamuzi wa kidemokrasia wa wananchi kuheshimiwe na kutochakachuliwa.


Hivi karibuni waziri Kombani alikaririwa na vyombo vya habari akisema suala la kuunda katiba mpya haliwezekani kwa kuwa serikali haina fedha na kwamba itaendelea na utaratibu uliozoeleka wa kufanya marekebisho ya katiba pale inapohitajika.

Naye Jaji Mark Bomani alisema kinachotakiwa sasa ni kufanyika kwa mapitio ya kina ya katiba iliyopo na kuainisha upungufu wote, kisha kufanya mabadiliko kwa mujibu wa mahitaji. "Nadhani ni woga ambao hauna msingi wowote, wanahofia kile ambacho watu watapendekeza katika katiba mpya, lakini mimi naamini watu wakikaa chini na kutulia, hawawezi kuja na vitu vya ajabu," alisema Jaji Bomani.

Madai ya serikali ya CCM kuhofia kitakachofuata baada ya kupatikana kwa katiba mpya, pia yalitolewa na Mhadhiri wa Sheria wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Profesa Mujwahuzi Njunwa, ambaye aliongeza kuwa hata CCM kama wakija kushindwa katika uchaguzi mkuu, watakuwa mstari wa mbele kudai mabadiliko ya katiba.


"Hii ni tabia ya watawala wengi, kuwa na woga na kutokukubali mabadiliko, jambo hili linatoa picha kuwa serikali haipo kwa maslahi ya wananchi na taifa," alisema Profesa Njunwa.

Hata hivyo, akizungumzia hoja ya matumizi ya nguvu ya umma iliyotolewa na Chadema hivi karibuni, iwapo CCM watagoma kusikiliza hoja za mabadiliko ya katiba, Profesa Njunwa alisema serikali haiwezi kungojea hali hiyo itokee.


Jaji Bomani ambaye aliwahi kuwa Mwanasheria wa serikali, aliishauri serikali kuunda jopo la wataalam kutoka sekta mbalimbali watakao pitia sheria iliyopo na kuja na mapendekezo ya kuwa na katiba mpya, jambo ambalo alisema litamaliza mvutano uliopo.

Kwa upande wake, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Vunjo kwa tiketi ya CCM katika Bunge lililopita, Aloyce Kimaro alisema ni vema serikali ikapewa muda wa kujipanga, lakini alisema kuna ulazima wa kuwa na mabadiliko kwa katiba. "Hakuna nafasi kwa serikali kutosikia, na kama wataziba masikio, wananchi watawalazimisha kusikia. Lazima kuwe na mfumo unaoleweka, hizi si zama za watu wachache kuamua juu ya mambo ya nchi," alisema Kimaro.

Naye Mhadhiri wa Kitivo cha sheria, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Chris Maina alipozungumza na Mwananchi Jumapili wiki iliyopita alisema Tanzania ni Jamhuri ya Muungano wa nchi mbili, serikali mbili na katiba mbili, katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 na Katiba ya Zanzibar ya 1984. Alisema kwamba hivi sasa kuna kero nyingi za Muungano.


SOURCE: 'Mwananchi' Newspaper.
 
Katiba inamahusiano gani na kanisa!? Au kwasabab zote zina anza na "k" wastake kutufanya si wajinga,kilaini abaki na kondoo wake na politicians waendelee na strugle zao, isije ikawa kama 1992 ishu za MoU....!
 
My Independent Take:

Mabadiliko ya KWELI YA KATIBA kamwe yasifuate mkondo wa KUTOKA JUU KWA WATAWALA kuja kwetu chini WATAWALIWA.

Tunapozungumzia MABADILIKO YA KWELI ya KUANDIKA UPYA KATIBA hapa Umma wa Tanzania tunamaanisha ya kwamba katika vikundi vyetu mbali mbali katika jamii ya Tanzania TUNAJUA FIKA TUNACHOKITAKA KIWEMO ndani ya Katiba hiyo Mpya ikiwakilisha vipaumbele vyetu tofauti tofauti, changamoto, Ndoto Zetu ambazo tunataka ziingizwe katika MKATABA MPYA KATI YETU NA WATAWALA watakaofuatia hapo baadaye, ambao watalazimika kuyatii, kuyazingatia na kuyasimamia KIKAMILIFU bila unafiki wala kuathiri Umoja wetu wa Kitaifa.

Hebu tuacheni kukajiandikia KATIBA MPYA ibebe yale mambo tunayotaka sisi na wala si yale mnayotaka watawala. Katiba mpya tunayotaka itaandikwa na sisi katika makundi yetu tunamojishughulisha kimaisha ili kweli ipate kuakisi matakwa YETU MAPYA. Hivyo tunatarajia kuona TAASISI MBALIMBALI zikishirikishwa MOJA KWA MOJA bila Ujanja Ujanja wa kutumia WATAALAMU ambao tangu huko nyuma hawakua tayari kudai tunachodai kwa nguvu zote leo hii.

Katka kuandika tunatarajia kuwa na halaiki ya watu pale uwanja mpya ya taifa kila mmoja akisema kwa UWAZI KABISA anachotaka kiwemo mle ndani. Hivo sote tujiandae katika vikundi vyetu kama vile NGOs, Academicians, Wachimbaji, Wakulima, Wafanyabiashara, Wavuvi, Wanafunzi, Wawekezaji wa Nyumbani, Washikadau wa Serikali ya Muungano, Dini, Wasanii, Wachezajii, Akina Mama, na SIsi Hapa Vijana... na kadhalika)

Kwa mantiki hii, kinachozungumziwa hapa ni sawa na kusema kwamba (i) Kuna Kampuni moja inaitwa JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, (ii) na kwamba kuna wamiliki wake ambao ni sisi wananchi wa Tanzania, na kwa upande mwingine (iii) kuna wafanyakazi wetu wanaoitwa Rais na Baraza lake, Bunge na Mahakama.

Sasa baada ya kampuni kufanya kazi takriba kwa miaka 50 sasa, wenye mali tumepitia vitabu vya mahesabu na kuona HAKUNA TIJA inayopatikana isipokua hali inayoendelea kwa sasa ni WAAJIRIWA KUJISAHAU NA KULA HADI MTAJI (UFISADI WAKUTISHA KILA KONA) WAKIDHANI kampuni hii ni mali yao binafsi. Ndipo Umma wa Tanzania TUKAJIAMULIA KUANDIKA UPYA MKATABA NA WAO (KATIBA MPYA) ili tukapate (a) kuweka DIRA MPYA ya miaka mingi ijayo kwa kampuni ambayo ni mali yetu halali,

(b) kuweka KINGA ya kulinda rasilmali zetu tulizowekeza mle, na (c) kupata kutiliana sahihi upya kuhusu mwenendo mpya ya kazi na kuwajibika zaidi kwetu; SASA HILI LA JAJI (RTD) BOMANI LA WATANZANIA KUWAACHIA WASOMI watakaoteuliwa na WAAJIRIWA WETU wakatazame jinsi gani bora zaidi ya kulinda Maslahi yetu sisi wenye mali -- HAYA NI MATUSI YA WAPI HAYA???

HIVI, NI NANI ATAKUA MWENDAWAZIMU KIASI CHA KUMUACHIA MWAJIRIWA WAKE AMBAYE AMEKUA AKIMKATISHA TAMAA KILA SIKU KWA UDOKOZI WAKE, KAZI YA KUTEUA WATU WA KUMUANDIKIA MKATABA MPYA KULINDA MASLAHI YAKE.

JAJI BOMANI, TUNAKUHESHIMU SANA LAKINI HATUKO HAPA KWA AJILI YA UTANI, hatusemi Mabadiliko ya kweli kwa ajili ya kufurahisha midomo yetu, ni pia itakua ni makosa makubwa mnoo endapo mtu yeyote atakua anatu-UNDERRATE sisi VIJANA juu ya ufahamu ya nini TUNAKITAKA katika katiba mpya. Kukaa kwetu kimya baada ya uchakachuaji wa kura kusije kukatafsiriwa kivinginevyo hapa.

Wana-JF, Katiba MPYA ipatikane kwa njia ya

KATIBA MPYA YA WATAWALA MAFISADI
(TOP-DOWN APPROACH = Mafisadi Kujitungi Mbinu Mpia ya Kula)

(a) Maamuzi ya Watawala kuja kwetu chini (TOP-DOWN APPROACH au
KATIBA MPYA WA UMMA WA TANZANIA
(BOTTOM-UP APPROACH = MABADILIKO YA KWELI ya Umma wa Tanzania kutawala)


(b) tukaiandike KUTOKA HUKU HUKU CHINI hiyo katiba MPYA kwa elimu zetu za ngumbaru ndio ipate kupewa UFUNDI wa lugha ya kisheria inapopelekwa kwa watawala HUKO JUU yaani (BOTTOM-UP APPROACH) ????

Nawashilisha hoja kwenu ijadiliwe kwa kina hapa

(mkumbuke One Mistake A Thousand Goals by MV UFISADI hapo nje).
 
Katiba inamahusiano gani na kanisa!? Au kwasabab zote zina anza na "k" wastake kutufanya si wajinga,kilaini abaki na kondoo wake na politicians waendelee na strugle zao, isije ikawa kama 1992 ishu za MoU....!
Wewe unafikiri katiba inatungwa na nani makundi ya jamii mbalimbali yakiwemo ya dini, katiba haitungwi kwa kujifungia ofisini kama bajeti.
 
CCM ni vilaza wa daraja la kwanza. Ila sidhani kama ni vilaza in the strictest sense. Wanatambua uzuri na madhara ya katiba mpya na ndiyo maana kwao hilo si kipaumbele.

Na kama wameyaweka mbele manufaa ya mustakabali wa taifa basi wataonesha juhudi za kuongoza mchakato wa kuandika hiyo katiba mpya ambayo kwa kweli iko long overdue!!!!
 
Nasikia JK alilalamikia sana kwa pengo kuhusu huyu mwanatheolojia kujihusiha na siasa ndo wakamtupa bukoba.

Lakini anachoooongea ni kweli
 
This is the RIGHT WAY to go.

Katiba MPYA itungwe katika vikundi vyetu mbali mbali TUNAVYOPENDEZEWA kisha baada kwenye Mkutano Mkuu pale Uwaja Mpya wa Taifa tutakaa na kuoanisha mawazo yetu yanayoendana kwa pamoja na yale yanayopingana tutayapeleka kwenye REFERENDUM.

Vijana na sisi tuanze kazi si kuongea tu tusije tukaachwa na basi la mabadiliko ya kweli nchini mwetu tena kuja kujilaumu hapo baadaye. Mzee Mgaya wa Vyama Vya Wafanyakazi Tanzania, nanyi kazi ianze mara moja, hata ndugu zetu MNAOISHI KWA MATUMAINI lakini bado mnaporwa hata misaada kidogo mlioletewa na pia kunyimwa fursa ya ajira kutokana tu na mabadiliko ya hali ya afya, ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi, makuli, wachimbaji wadogo wadogo, akinamama mnaotengwa kupata mali shauri ya tofauti tu za jinsia ... kazi sasa ni kwetu!!!!
 
Back
Top Bottom