kilimasera
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 3,068
- 277
MJADALA wa kuwepo kwa mabadiliko ya Katiba umeibuka tena. Mjadala huu umekuwa ukiibuka na kuzimwa na Serikali mara kwa mara. Lakini hivi karibuni baada ya Rais Jakaya Kikwete kumteua Celina Kombani kuwa Waziri wa Katiba na Sheria, swali kubwa kwake limekuwa ni kuhusu mabadiliko hayo.
Hata hivyo, Kombani ameonyesha kutokuwa na dhamira ya kusimamia mabadiliko hayo. Hivi karibuni alikaririwa akisema kuwa kama kuna watu wanataka mabadiliko hayo wapeleke mapendekezo hayo ofisini kwake lakini akasema mabadiliko hayo yatagharimu fedha nyingi ambazo kwa sasa serikali za kutosha kuyafanikisha.
Kutoka na majibu hayo, wanasheria kadhaa wamejitokeza na kueleza haya ya serikali kusimamia mabadiliko hayo. Mhadhiri wa Sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Chris Maina anasema mabadiliko ya Katiba hayahitaji mapendekezo wala shinikizo bali, ni jukumu la serikali kuyafanya.
Mabadiliko ya Katiba siyo lazima yaletwe mapendekezo, Serikali yenyewe inapaswa kufanya. Mbona mabadiliko ya 14 yalifanywa na serikali yenyewe. Kulikuwa na mabadiliko mwaka 2005 ambapo serikali iliingiza vipengele vya haki za binadamu bila kushinikizwa na mtu yoyote, kwa hiyo Serikali isisubiri mapendekezo anasema Profesa Maina.
Profesa Maina anasema kuwa vuguvugu la sasa la kutaka kuwepo kwa Katiba mpya ni sehemu ya madai ya siku nyingi ambayo huibuka mara kwa mara na kuzimwa bila ya kuangaliwa kwa undani na kupewa majibu ya kuridhisha. Kwa sababu hiyo anasema madai hayo yataendelea kuibuka kwa namna moja au nyingine.
Kwa kukumbushia tu wakati wa Tume ya Mheshimiwa Jaji Mkuu Nyalali ya mwaka 1991 kuhusu mfumo wa vyama vingi na ambayo ilipendekeza kuanzishwa kwa mfumo wa utawala wa vyama vingi vya siasa kulikuwa na hoja nzito tu kwamba mfumo huo mpya wa vyama vingi ulihitaji Katiba mpya na siyo kurithi hiyo Katiba ya chama kimoja ambayo mihimili yake ilikuwa tofauti kabisa. Hoja hizi hazikupewa majibu na vyama vingi vya siasa viliingizwa ndani ya Katiba ya mwaka 1977 kupitia Mabadiliko ya Nane ya mwaka 1992. Mabadiliko haya ya Katiba yalitungiwa pia Sheria ya utekelezaji Sheria ya Vyama vya Siasa Namba 5 ya 1992.
Anakumbushia pia Kamati ya 'White Paper' iliyoundwa chini ya Jaji Dk Robert Kisanga mwaka 1998, akisema wananchi waliibua tena suala la Katiba mpya... Kamati ilipowasilisha Ripoti yake ilikemewa eti imevuka mipaka yake kwa sababu ilikuwa Kamati na siyo Tume. Hapa tena suala la Katiba mpya likawekwa chini ya mkeka.
Akizungumzia madai ya sasa, Profesa Maina anasema kuwa suala hilo limechukua sura ya mikakati ya vyama vya siasa huku baadhi yao vikilichukua kama sehemu ya ilani zao za uchanguzi na kuahidi wananchi kuunda Katiba mpya. Anakumbushia hotuba ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa aliyoitoa katika Mkutano wa Mwaka wa chama cha Mawakili wa Afrika Mashariki (EALS) uliofanyika Bujumbura, Burundi Novemba19 na 20, mwaka huu... Aliifananisha Katiba ya nchi na roho katika mwili wa binadamu na kusisitiza haja ya kuwa na Katiba bora.
Profesa Maina anasema ni vizuri kuona viongozi waliotoka madarakani wanatafakari na kuona vizuri baadhi ya vitu ambavyo hawakuvipa umuhimu wakati wakiwa bado ofisini.
Vilevile inafaa iwe funzo kwa viongozi walio madarakani kushughulikia matatizo yanayowakera wananchi kama vile kuwa na Katiba isiyoridhisha. Haitoshi kukaa ofisini kusubiri malalamiko ya vikundi vya kiraia au vyama vya upinzani ili uyafanyie kazi. Wizara husika inatakiwa iwe msitari wa mbele (pro-active) katika kutoa mapendekezo ya kuboresha Katiba na ndiyo maana inaitwa Wizara ya Katiba na Sheria, anasema Profesa Maina.
Mwanasheria Mkuu wa zamani wakati wa Serikali ya Awamu ya Kwanza, Jaji Mark Bomani naye anasisitiza kuwepo na mabadiliko ya Katiba. Anasema Katiba iliyopo sasa ina umri wa miaka 50 hivyo imepitwa na wakati.
Ni kweli, Katiba yetu sasa inatakiwa ifanyiwe marekebisho ya jumla. Ni Katiba yenye umri wa karibu miaka 50 na chimbuko lake ni tangu uhuru. Ilifanyiwa marekebisho mwaka 1979 na mwaka 1992 wakati tunaingia kwenye mfumo wa vyama vingi.
Lakini sasa mazingira yamebadilika watu wamejifunza mengi kutoka sehemu tofauti.
"Umefika wakati sasa wa kuibadilisha yote na kazi hiyo ishirikishe wadau wote. Serikali ikae kitako na wadau wote ili kujadiliana kuhusu mabadiliko hayo. Hii ndiyo njia pekee ya kujibu malalamiko ya vikundi mbalimbli. Serikali inapaswa kuunda jopo litakaloratibu mchakato mzima wa kuundwa kwa Katiba mpya. Ningependekeza kuwe na comprehensive review. Siyo kila mtu alete mapendekezo yake, itakuwa ni vurugu tupu, anasema Jaji Bomani.
Bomani anaeleza chanzo cha serikali kusuasua kukubali mabadiliko ya Katiba akisema kuwa ni woga wa viongozi waliopo madarakani...
Ni woga tu, wanaona woga kwa sababu hawajui kitakachojadiliwa na kupitishwa kitakuwa nini kama wakiwapa watu uhuru wa kujadili. Lakini nadhani njia bora ni serikali kukaa kitako na wadau ili kupata maendekezo yao kuhusu mabadiliko hayo.
Mwanasheria na wakili wa Mahamama Kuu ya Tanzania, Profesa Abdallah Safari anasema madai hayo ni ya muda mrefu lakini serikali imekuwa ikiyapuuza. Anakumbushia rasimu ya Katiba iliyokuwa ikiandaliwa na vyama vya upinzani vikiongozwa na CUF akisema kuwa hayo yalikuwa ni mapendekezo mengine ya mabadiliko ya Katiba ambayo yameshafika serikalini.
Profesa safari aliyewahi kutoa kitabu kinachoeleza haja ya Tanzania kuwa na tume huru ya uchaguzi anasema kuwa Serikali inaogopa mabadiliko ya Katiba kwa sababu yataleta tume huru ya uchaguzi na hapo ndiyo utakuwa mwisho wa ushinndi wa CCM... Hao wanaogopa Katiba mpya kwa sababu wanajua kuwa italeta tume huru ya uchaguzi na hapo hawatashinda tena. Watashindaje wakati hawakubaliki?
Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) Felix Kibodya anasema kuwa pamoja na madai hayo kuwa ya muda mrefu bado wanampa nafasi Waziri Kombani kujipanga kwani ndiyo kwanza ameingia ofisini. Hata hivyo, anasisitiza kuwa madai hayo ni ya msingi na kwamba wanaandaa mapendekezo mengine ambayo watayapeleka kwa Waziri ili yafanyiwe.
Kama tulivyotoa taarifa yetu kuhusu uchaguzi, tutaandaa mapendekezo yetu na tutayapeleka kwa waziri. Kwa kweli hata sisi tunahitaji mabadiliko ya Katiba anasema Kibodya.