Riviera aika
New Member
- Aug 4, 2021
- 2
- 0
Ni Vema tungeanza kwa kutambua maana halisi ya neno MAENDELEO.
"Maendeleo ni mabadiliko yanayo onekana kuboresha hali ya binadamu na mazingira kwa ujumla".Kuna ngazi tatu za kimaendeleo; Maendeleo
Binafsi,Maendeleo ndani ya Jamii na Maendeleo ya Nchi kiujumla.Aina zote hizi za maendeleo huleta MCHANGO KATIKA UCHUMI WA NCHI.
Kabla ya kuendelea kufafanua namna ambavyo maendeleo ya kijamii huleta chachu katika kuinua uchumi wa nchi ningependa nikufafanulie maana ya neno Jamii,neno Uchumi,neno Nchi na Neno Maendeleo ya Jamii;
Jamii ni Istilahi inayoeleza uwepo wa pamoja wa mwanadamu,ni mkusanyiko wa watu wanaoishi pamoja katika eneo moja la kijiographia.
Uchumi ni jumla ya shughuli zote za binadamu zinazolenga kutosheleza mahitaji yao hasa za uzalishaji,usambazaji na utumiaji.
Nchi ni kitengo cha kisiasa katika eneo maalumu,huwa imegawanyika katika mikoa mbalimbali.
Maendeleo ya Jamii ni mchakato wa wanajamii kukusanyika pamoja kwaajili ya kupata suluhisho la changamoto zinazowakabili.hii ni dhana pana inayotumika kwa viongozi,wanajamii,wanaharakatii pia ikiwahusisha wataalamu ili kuboresha maisha ya wanajamii pamoja ili kutengeneza jamii iliyo bora.
MABADILIKO MABALIMBALI YANAYOPASWA KULETA MAENDELEO NDANI YA JAMII ILI KULETA CHACHU KATIKA UCHUMI WA NCHI
1.) UTOAJI WA ELIMU YA STADI ZA KAZI NDANI YA JAMII BILA KUJALI JINSIA,RIKA NA UWEZO WA MWANADAMU; Itapendeza Sana kukiwa na utaratibu maalumu wa kutoa Elimu ya stadi za kazi ndani ya jamii.Elimu hii iwe kwa NJIA YA VITENDO na MKUFUNZI ATOKE NDANI YA JAMII HUSIKA ili aweze kujibu Maswali na kufuatilia kwa ukaribu uwelewa wa somo husika.Elimu inaweza kutolewa kwa njia za kimakundi.Stadi hizi za kazi ni kama
●Upishi
●Kilimo cha mbogamboga
●Ushonaji
●Kutengeneza Sabani
●Kutngeneza Vikapu na Shanga.
Huku kutapelekea wengi kujiajiri na kukuza Uchumi wa Nchi.
2.) UTOAJI WA ELIMU JUU YA MAGONJWA MBALIMBALI PAMOJA UTUNZAJI WA AFYA ZETU; Ni Muhimu kila mmoja ndani ya jamii husika apate nafasi ya kutambua magonjwa mbalimbali yanayoibuka kutokana na hali ya hewa,Maji Machafu na kujaamiana.Mfano elimu juu ya UKIMWI, UVIKO19, KIPINDUPINDU na mengineyo. Elimu hii itapelekea wanajamii kutunza afya zao na kuongezeka kwa nguvu kazi hivyo kupelekea kukuza Uchumi wa Nchi.
3.) ELIMU YA MATUMIZI MAZURI YA FEDHA PAMOJA NA UWEKEZAJI; Wengi Wetu ndani ya jamii hatuna elimu juu ya matumizi mazuri ya kifedha kupelekea ukosefu wa maendeleo vilevile elimu ya uwekezaji na matumizi ya mifuko ya hifadhi kama NSSSF,UTT AMIS kupitia elimu hii Jamii itahamasika juu ya matumizi mazuri ya kifedha hivyo kupelekea ukuaji wa uchumi.
4.) ELIMU YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA; Dunia yetu kwa sasa inamatumizi makubwa ya teknolojia katika nyanja mbalimbali hivyo kila jamii inapaswa kupata mwanga wa elimu ya sayansi na teknolojia ili kusonga mbele kwa kasi inayotakiwa tukijifunza kutoka kwa mabara mengine. Ni muhimu kujifunza namna ya kutumia vifaa janja mbalimbali mfano simu janja,tarakilishi mpakato na vingine ambapo mtu anaweza kujiajiri kupitia hivi vifaa kwani uchumi wetu utakua kwa uharaka sana tukizingatia matumizi bora ya elimu ya sayansi na tecknologia.
Kwa kuhitimisha ni vema tukizingatia sana katika maendeleo ndani ya jamii zetu kwakua ndicho kinacholeta chachu ya ukuaji wa Uchumi wa Nchi.

Upvote
0