funaku
JF-Expert Member
- Oct 12, 2011
- 39,468
- 31,952
Katika kipindi hiki cha maamuzi na uwekwaji wa mustakabali wa Taifa ni muhimu tukarudi kwenye chambuzi na definitions mbalimbali zinazoelezea maana mtambuka (complex) ya maendeleo.
maendeleo ni nini...?
Itoshe kusema maendeleo ni jumuiko la mambo kadhaa endelevu yawe ya zamani au hata mapya yatakayokuwa yanajitokeza.
Maendeleo kwa muktadha wa kimataifa hadi sasa yana elements kadhaa ambazo sio lazima au rahisi zifikiwe kwa wakati mmoja...ndio maana tumekuwa na mihula ya kujatathmini katika hali zote...hii inamaanisha huwezi kumhukumu mtu au Serikali kwa kutumia kigezo(element) moja ya maendeleo...unatakiwa umchambue mtu au Serikali katika elements zote au vigezo vyote vinavyoelezea maendeleo.
Vipo vigezo ambavyo nitavitaja vinavyoonesha nchi au Taifa linaendelea
1-Hali ya kukua kwa ujumla
2-Hali ya kuendelea katika kukua
3-mabadiliko chanya na makubwa
4-Mabadiliko ya miundombinu
5-Mabadiliko chanya ya mazingira
6-Mabadiliko ya kiuchumi
7-Mabadiliko ya hali ya kijamii
Sasa nitaangazia vipengele hivyo hapo juu katika muktadha wa toka tupate uhuru na katika kipindi cha miaka mitano tunayoimalizia.
1-HALI YA KUKUA KWA UJUMLA WAKE
ni wazi kuwa Tanzania ya miaka ya 60 sio ya Tanzania ya miaka hii katika aspects zote za kuchambua maendeleo.miaka ya 60 au kurudi nyuma Tanzania imebadilika kama nchi nyingine zilivyobadilika.hili halina ubishi.
2-HAlI YA KUENDELEA KUKUA
Ni wazi kuwa Tanzania imeendelea kukua latika pase nzuri kwa kuitazama ilipotoka.tubaweza kusema tulipata shida baada ya vita vya Kagera lakini kwa ujumla yale yaliyopangwa kutekelezwa ili tuendelee yaliendelea kutekelezwa kadiri ya awamu mbalimbali.sekta ambayo naweza kusema haijakuwa kwa muendelezo unaotakiwa ni kilimo ingawa haijabaki kama ilivyokuwa.
3-MABADILIKO CHANYA NA MAKUBWA
Hakuna ubishi kuwa miaka ya hivi karibuni(chukua 95 hadi sasa) ambayo wengi wetu tumezaliwa kumekuwa na mabadiliko chanya na ya haraka.
kipekee ndani ya miaka mitano tunayoenda kuimalizia tumeshuhudia mabadiliko chanya na ya haraka.mfano uendeshaji wa serikali,uwajibikaji,matokeo makubwa yanayoendana na resources tulizo nazo ,uwezo wetu kuargain na majirani n.k
4-MABADILIKO YA MIUNDO MBINU
Hapa nikiyataja yote lazima andiko liwe refu haswa katika awamu hii.
fikiria shule,vituo vya huduma za afya,barabara,umeme,nyumba za kuishi ,viwanja vya ndege,madaraja,ofisi za umma n.k
5-MABADILIKO YA MAZINGIRA
Hapa unaweza kuangazia utunzaji wa vyanzo vya maji,uharamia dhidi ya wanyama(leo hii Tembo wanaingia mjini) ,uondishaji wa plastic ,usafi wa miji yetu n.k
mengi ya haya yamefanyika ndani ya miaka hii mitano.
6-MABADILIKO YA KIUCHUMI
Je yupo anayepinga hali ya ukusanyaji wa kodi?Je kuna anayepinga uwezo wa Taifa kujiendesha bila misaada?
Je yupo anayekataa Tanzania kuingia uchumi wa kati.?
7-MABADILIKO YA KIDEMOGRAFIA
Ni ukweli usiopingwa kuwa magonjwa ya kimasikini yamepungua na yale ya kitajiri yanaongezeka.
Ni ukweli usiopingika kuwa uwazi na uwajibikaji wa Serikali umeongezeka.
Nani anayekataa kuwa wenye elimu,afya bora wameongezeka?
Nani anayedanganya kuwa ndani ya miaka mitano vifo vya albino au vikongwe vimepungua?
Nani atakayebisha kuwa ujambazi umepungua?
Nani atakayebisha kuwa watu wengi wamepata fursa ya kugombea?
Kwa ufupi niseme kwa asilimia kubwa Tanzania imeendelea katika nyanja zote na hakuna namna ya kubeza iwapo unafikiria kwa kina.
KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!!!