Maendeleo ni nini? Ukweli kuhusu maendeleo ya vitu na maendeleo ya watu

Amani Msumari

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2016
Posts
1,833
Reaction score
979
Waungwana,

Kwanza nikiri kuwa mimi sio mtaalamu wa uchumi Ila ninafahamu kuhusu maendeleo. Suala la maendeleo linatafsirika tofauti kutokana na mitazamo tofauti.

Hapa karibuni pamekuwa na kelele sana kuwa watanzania wanataka maendeleo yao (maendeleo ya watu) na siyo maendeleo.ya vitu.

Uzi huu uwe ni kujadili kati ya vitu hivyo viwili na mimi nitashiriki kama mchangiaji muongozaji.

Nini Kifanyike?

Amani Msumari
Tanga
 
SWALI FIKIRISHI 1

Je, inawezekana kuwa na Maendeleo ya watu bila kuwa na maendeleo ya vitu?
 
SWALI FIKIRISHI 2

Upi ulikuwa mtazamo wa Mwl. Nyerere alipoongelea maendeleo ya watu?
 
SWALI FIKIRISHI 3

Je, ipo mifano ya nchi zenye maendeleo ya watu bila kuwa na maendeleo ya vitu?
 
Maendeleo ni perception tu

Ndio maana katika jamii fulani unaweza kuonekana unaendelea ila ukienda jamii nyingine unaonekana 'useless

Ni kwa sababu kama hizi unakuja kuona Maendeleo hayawagusi watu wote sawa sawa kama 'mahusiano'

Sisi wakristo tunaamini Yesu alikuja kutafuta kile kilichopotea yaan Ibada ambayo ni 'mahusiano' yetu na Mungu

Ukichemka kwenye mahusiano umechemka kwenye kila kitu hadi hayo Maendeleo kwiyoo🐤🐤🐤🐤 unachemka tu.
 
watu wakipata maendeleo wataleta vitu hata mandege kama fastjest walivyofanyaga.
vitu bila kuwawezesha watu ni kazi bure.
Asante ndugu Jabulani kwa kuwa mchangiaji wa kwanza.

Unaweza kufafanua kidogo mchango wako? Uliposema watu wakipata maendeleo wataleta vitu, umemaanisha nini?
 
Umesema vyema ndugu Balimar.

Kwahiyo unamaanisha hata Kama Maendeleo yapo lakini Kama hakuna uhusiano mzuri basi maendeleo hayo hayaonekani.

Maswali

Je, kwa kusema hivyo unakiri kuwa Tanzania Kuna maendeleo?
Je, hakuna uhusiano mzuri?
Uhusiano huo ni Kati ya Nani na Nani?
 
Ninaomba niweke wazi kuwa mimi kwenye mjadala huu nipo upande wa kutetea kilichofanywa na kinachoendelea kufanywa na serikali katika kuwaletea watanzania maendeleo
 
Maendeleo ya vitu Kama hayagusi kuboresha maisha ya watu hio ni matumizi mabaya ya Kodi za wananchi.
Mfano kujenga ikulu mpya dodoma Hali iliyopo Ni toshelevu, kujenga airport Chato Hali Chato nzima wenye kumudu kupanda ndege awafiki kumi haya ni maendeleo ya vitu, kujenga majengo makubwa ambayo sio hitaji la ulazima kiuchumi.
 

Attachments

  • 2452889_VID-20200711-WA0010.mp4
    10.7 MB
Yes mfano nchi nyingi za kidikteta kwao Ni fahari kurundika vitu kwa ajili ya ufahari wa watawala na sio vipaumbele vya wananchi
Sawa. Mfano wa nchi hizo na vitu vilivyorundikwa
 
Ninaomba niweke wazi kuwa mimi kwenye mjadala huu nipo upande wa kutetea kilichofanywa na kinachoendelea kufanywa na serikali katika kuwaletea watanzania maendeleo
But kwnn yaliyofanywa yameshindwa boresha maisha ya watu.Watz wengi walishasahau Ni lini walikunywa chai ula maramoja kwa siku saa kumi Hadi kesho Tena.Kama umebahatika kula Milo 3 shukuru.
 
Jo Mose,

Serikali ya CCM katika awamu zote zimekuwa zikileta maendeleo. Awamu ya tano imekuwa na kasi zaidi katika hilo hasa katika awamu hii ya miaka 5 ya kwanza ya Rais Magufuli.
Barabara, madaraja, ndege na miradi ya kimkakati, yote yanalenga kumsadia mwananchi wa kawaida.

Ujenzi wa ndege Chato sioni shida. Chato ni sehemu ya Tanzania. Isitoshe, tunahitaji viwanja vya kisasa zaidi sio tuu Chato bali na sehemu nyingine za nchi yetu. Hizo sio zama za kujenga "air strips". Tunahitaji vitu bora. Je, shida iko wapi? Ni uwanja wa kisasa au Chato?
 
But kwnn yaliyofanywa yameshindwa boresha maisha ya watu.Watz wengi walishasahau Ni lini walikunywa chai ula maramoja kwa siku saa kumi Hadi kesho Tena.Kama umebahatika kula Milo 3 shukuru.
Jo Mose,

Wakati unaandika kumbuka na sisi wasomaji humu wengi ni watanzania na ukweli unajulikana.
 
Handeni,manyoni,karagwe wanataka nao uwanja.
Je huo uwanja ndio vipaumbele vya wananchi wa chato,hofu Ni baada ya kumaliza mda uwanja utabakia wa kuanikia mazao,na kujifunzia kuendesha bodaboda.
Na usimnufaishe mwananchi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…