Maendeleo ni stress tupu

Una nyumba nzuri, gari nzuri, bima ya afya, unaweza kwenda sehemu ya starehe ukafurahia maisha, ndugu ENJOY. Ukianza tu kuutafuta utajiri zaidi ya huo utaishi maisha ya stress mno.
Watu wengine ni Roho tu za korosho hawana shukrani.

Yaani unamkuta mtu kanyaukaaaa! Na huku pesa anazo eti anatafuta utajiri.
 
100% true..!! Hasa kwenye ku-maintain status, FULL STRESS
 
Watu wengine ni Roho tu za korosho hawana shukrani.

Yaani unamkuta mtu kanyaukaaaa! Na huku pesa anazo eti anatafuta utajiri.
Kwangu, mtu yeyote anayeishi tofauti na kipato chake, huyo ni mchawi..!! Huwezi kuwa na utajili mkubwa halafu utembee na ndala zilizotoboka..!! 'Ukinga' huo sina..!!
 
Sio maendeleo, bali utajiri ni stress sana.

Mda mwingine unakua na mawazo vipi wasifu ukishuka ntaonekanaje, huwezi zurura barabarani kindezindezi,

Pia ni watu wanaongoza kwa kukosa usingizi na kuishi kwa mashaka kuhofia usalama wao.
 
tatizo unavotumia utahitaji mazuri zaidi.
Hakuna mazuri zaidi, ni stress zaidi.

Ninavyojua, fomula ni nyepesi tu, kadri unavyojulikana kuwa wewe ni tajiri ndivyo watu wanavyoumiza kichwa kuchukua fedha zako na ndivyo unavyoumiza kichwa kuzikusanya zinazochukuliwa.

Unakuwa kwenye trap ya utafutaji na hutoona kuwa ulichonacho kinatosha kukupa furaha, ndo pale unashangaa mtu ana Fixed deposit ambazo zinampa riba nzuri tu, ana appartment sehemu nzuri tu zinazompa kodi nzuri, ana biashara sehemu nzuri ila hana raha sababu anafungua kiwanda chake na watu wa serikali wanakiandama na ukaguzi sababu mshindani wake anawahonga wamkwamishe.
 
kweli mzee
 
Watu wamekariri kuwa maendeleo ni utajiri wa kiuchumi.

Inabidi wamsikilize LKJ katika "More Time".


View: https://youtu.be/_0abSDI9E-s?si=6OoAtmpd_yo14ut9
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…