SoC03 Maendeleo ni zao la mabadiliko

SoC03 Maendeleo ni zao la mabadiliko

Stories of Change - 2023 Competition

Musa Mkwanda

New Member
Joined
Jun 20, 2023
Posts
2
Reaction score
2
Mabadiliko ndio kila kitu.

Tanzania na Afrika kwa ujumla Ina matatizo yanayofanana kwenye kila nyanja elimu,uchumi,utawala,kilimo,afya sayansi na teknolojia.

Elimu tunayowapa watoto wetu mashuleni na vyuoni ni lazima wapewe elimu kulingana na mustakabali wa nchi yao kwa mfano Tanzania uchumi wetu wetu umejikita Sana kwenye kilimo, uchimbaji wa gesi, uchimbaji wa madini, utalii na vinginevyo Kama taifa tunatakiwa elimu yetu ijikite kwenye kufundishia watoto namna ya kuendesha hizo sekta na so vinginevyo, pia kukweli lengo la elimu ni kuelewa na utambuzi sio kuiga sioni haja ya kutumia kingereza mashuleni Kama Kuna uwezekano wa matumizi ya kiswahili na ni rahisi kwa mwanafunzi kuelewa serikali zetu iliangalie hili.

Uchumi wetu Kama taifa bado haujafikiwa kiwango cha kutajwa duniani miongoni mwa vinavyochangia kushuka kwa uchumi wetu ni rushwa,utegemezi,kutowajibika ipasavyo, rushwa ina upana wake sana nadhani sheria za kudhibiti ziwe thabiti sana kutokomeza na pia ajira zenye malipo mazuri ziwe nyingi ili kuepusha ulaji wa rushwa kwenye sekta mbalimbali, Kama taifa linatakiwa lisiwe tegemezi tuna ardhi tuna gesi tuna madini na kila kitu kwanini tutegemee kutoka nje ina maana tumeshindwa kuziendesha?

Sekta yetu ya kilimo bado iko nyuma Kama kilimo ndio nyanja yetu kuu watanzania kwanini tusiifanye yenye nguvu?

Kwanini Kama nchi tuagize chakula toka nje wakati tuna ardhi na rasilimali watu, wataalamu wa kilimo na kila kiihitajikacho kwenye sekta mama ni wakati wa mabadiliko sasa.

Utawala wetu unajitahidi kwa upande fulani Ila Kuna mambo yanatakiwa yarekebishwe kufikia nchi ya ahadi utawala Bora ni ule ambao unaweka wananchi na taifa mbele kila nyanja utawala ambao unaepukana na rushwa,matumizi mabaya ya madaraka na unajinyima pia Tanzania inaweza.

Afya ni sekta nambari moja tunatakiwa kuimarisha Mana bila Afya hakuna kazi itaenda taifa litazorota tu,tujifunze Kama watanzania kufanya Mambo yetu wenyewe tuna wanakemia na wansayansi wa kutosha sana kuweza kuendesha miradi yetu ya kiafya sioni haja ya kusibiri mpaka misaada ya dawa na vifaa vya Afya toka nje ni wakati wetu sasa kutumia elimu yetu kutufikisha tunapokwenda.

Sayansi na teknelojia ni nyanja adhimu sana tunatakiwa kuimarisha vipaji vyetu mashuleni na mitaani tuvikuze Mana sayansi na teknolojia hutoka kwao nadhani elimu ya vitendo ingesaidia Sana kukuza sayans na teknelojia hapa nchini kwetu sayansi ambayo mwanafunzi anaweza kuilewa tuwafundishe wanafunzi umuhimu na ubora wa sayansi hakika tutafika.

@JamiiForums,@storiesofchange Tanzania Mpya
 
Upvote 1
Back
Top Bottom