Na Fadhili Mpunji
Ripoti iliyotolewa kwa pamoja na Idara ya takwimu ya taifa ya China, Wizara ya sayansi na teknolojia, na wizara ya fedha ya China, inaonyesha kuwa mwaka 2020 fedha zilizotumiwa na China kwenye mambo ya utafiti na maendeleo zilikuwa ni zaidi ya dola bilioni 378 ambalo ni ongezeko la asilimia 10.2 ikilinganishwa na mwaka 2019, fedha hizo ni asilimia 2.4 ya GDP ya China kwa mwaka 2020. Uwekezaji huo uliwezekana, licha ya kuwepo kwa changamoto za janga la COVID-19.
Licha ya kuwa ongezeko la asilimia 10.2 ni kubwa kuliko malengo yaliyowekwa kwenye mpango wa 14 wa maendeleo ya miaka mitano, bado China iko nyuma ikilinganishwa na nchi wanachama wa Shirika la Ushirikiano wa uchumi na Maendeleo (OECD). Marekani kwa mfano inatenga asilimia 3 ya bajeti yake kwa ajili ya utafiti na maendeleo, wakati Israel na Korea Kusini zinatenga asilimia 5 ya bajeti zao.
Serikali ya China imekuwa ikihimiza ongezeko la bajeti ya fedha kwenye utafiti na uvumbuzi, wakati ikiendelea na mpango wa kujitegemea kiteknolojia. Hali hasa inatokana na ukweli kwamba China inaendelea kukabiliana na kitu kama ubaguzi wa kisayansi kutoka kwa baadhi ya nchi za magharibi, na inatakiwa kufanya utafiti na kuwekeza sana ili kujaribu kuzifikia nchi nyingine. Mfano mzuri uko kwenye sekta ya anga ya juu, ambako baada ya Marekani kuiwekea China vikwazo vya aina mbalimbali, China imekuwa haina chaguo ila kufanya juhudi kufanya utafiti ili iende sambamba na nchi nyingine. Na sasa imefanikiwa na kituo chake cha anga ya juu, ilichokitengeneza toka hatua ya mwanzo hadi hatua ya sasa kwa kujitegemea.
Lakini pia kwa sasa sehemu kubwa ya uchumi wa China ni uchumi wa kisasa, maendeleo ya karibu sekta zote za uchumi, iwe ni kilimo, usafiri na usafirishaji, huduma na hata biashara yanategemea sayansi. Tukiangalia sekta ya kilimo, tunaweza kuona kuwa China ililazimika kuwekeza fedha nyingi kwenye sekta hiyo, ili kuweza kuondokana na tatizo la upungufu wa chakula. Ikumbukwe kubwa Mzee Yuan Longping aliongoza utafiti ambao matokeo yake yalileta mbegu chotara ya mpunga inayotoa mazao mengi, na vile vile aliongoza utafiti uliosaidia kupatikana kwa mbegu ya mpunga inayoweza kuota kwenye ardhi yenye chumvi na alkali.
Jambo la kufurahisha ni kuwa maendeleo ya kisayansi ya China, sio kama tu yana manufaa kwa China, bali pia yana manufaa kwa dunia nzima. Tunaweza kuona mifano michache ya maendeleo ya kisayansi ya China kuzisaidia nchi nyingine. Kwa mfano, mbegu ya mpunga chotara sasa inalimwa katika nchi mbalimbali za Afrika na Asia. Nchi mbalimbali za Afrika sasa zimeanza kujiingiza kwenye sekta ya anga ya juu kutokana na msaada wa China kwenye kutengeneza satellite na kuzirusha kwenye anga ya juu. Mfano mwingine ni msaada wa chanjo ya COVID-19, ambayo baada ya China kutafiti na kutengeneza chanjo hiyo, sasa imekuwa ni bidhaa ya umma kwa dunia, tofauti na baadhi ya nchi za magharibi ambazo zimeamua kuhodhi chanjo hiyo.