Maendeleo ya sayansi na teknolojia yamebadili tabia zetu kama binadamu

Maendeleo ya sayansi na teknolojia yamebadili tabia zetu kama binadamu

Teknolojia imefanya mwanamke asithaminiwe tena kingono. Wanaume wanaona tupu za wanawake mitandaoni kwa hiyo hata ukikutana nayo mubashara abadan hamu imeshaisha.
Pia imepunguza ubakaji. Kuna tafiti niliona inasema wigo wa internet ukiongezeka kwa 10% ubakaji unapungua kwa 7%.
 
Nitasoma kwa utulivu hilo andiko na hicho kitabu na nitakupa inputs zangu.

Jambo moja tu aliloligusia ni uhalibifu wa mazingira kuwa utamfuta mwanadamu. Tunakubali uharibifu wa mazingira unatokana na hewa ukaa na ukataji miti. Nitagusia ukataji miti. Ukichunguza afrika ukataji miti unatokana na matumizi ya mkaa na kilimo. Yote hayo mawili yanatatuliwa na teknolojia. Wewe ni shahidi matumizi ya Gas yamepunguza matumizi ya mikaa mijini. Pili teknolojia ya majiko yakisasa ya mkaa yamepunguza matumizi ya mkaa. Hoja yangu ni kuwa teknojia bado inaendelea kupambana ili kutatua tatizo la uharibifu wa mazingira.
 
Siku hizi hata kula pamoja nyumbani hakuna. Huyu kaenda kuangalia mpira, huyu anaCHAT jikoni mwingine anacheza GAME chumbani. Chakula kipo kwenye hotpot kikipoa mtu anapasha kwa MICROWAVE.
Hahhaa kweli asee kukaa mezani kula kama familia hamna siku hizi kila mtu ana mda wake.
 
Tutaendelea kusalimiana vizuri sana ila tutakuwa tunakutana kwa mambo ya muhimu zaidi.
Kwa kweli mfumo wa maisha umebadilika sana, nakumbuka miaka ya nyuma sikukuu ya Wakristo basi tunafungasha mapilau kupeleka kwa majirani zetu waislamu lakini hivi sasa mambo yamekuwa kinyume kabisa. Kwa kweli tunapoenda itafika mahala tutakuwa hatusalimiani kabisa.
 
Sio kweli,kizazi cha sasa kina upendo mwingi zaidi kuliko hao ancestors wetu walioishi karne zilizopita. Hapo karne ya 18 tu isingekuwa rahisi Mkuria kuchanganyikana pamoja na Mhaya ila leo hii hadi wanaweza kuona kabisa,haya ni maendeleo makubwa sana.
Kizazi cha sasa tumekuwa wabinafsi sana, tusio na upendo.
 
Hapo ni wazazi wameshindwa kuwaweka pamoja watoto wao muda wa kula.
Siku hizi hata kula pamoja nyumbani hakuna. Huyu kaenda kuangalia mpira, huyu anaCHAT jikoni mwingine anacheza GAME chumbani. Chakula kipo kwenye hotpot kikipoa mtu anapasha kwa MICROWAVE.
 
Ukishindwa kuwafundisha watoto table manners umeshindwa wewe kama mzazi, hata katika jamii zilizoendelea sana katika sayansi na teknolojia kama Magharibi,Japan na China table manners ziko kwa kiwango cha juu sana.
Hata kuwafundisha watoto table manners hatuwezi baba anakula chakula akiwa kwenye sofa anaangalia Man United inacheza.
 
Teknoljia inaweza kutuangamiza kwa sababu inaharibu mazingira ya dunia,ila pia inaweza kutuendeleza zaidi kama binadamu tutaitumia ipasavyo kama vile kufanya umeme wa sola uwe wa bei rahisi na kuachana na mafuta, mkaa na gesi.
Tunachokitafuta tutakipata muda si mrefu! Tecnolojia itakuja kutuangamiza
 
Maendeleo ya sayansi na tekinolojia yameua mahusiano ya kijamii. Leo hii kila mtu anatembea na simu. Akiwa anasubiri huduma iwe mahakamani au hospitali anaingia Instagram au Facebook. Hakuna muda wa kumsalimia aliyekaa pembeni yako.

Miaka ya nyuma ilikua ni kawaida kugonga mlango katika nyumba iliyo karibu na kuomba maji ya kunywa ukiwa na kiu. Siku hizi kugonga nyumba ya mtu kuomba maji au kuomba kutumia simu umepatwa na dharura ni jambo la ajabu. Enzi za simu za mezani nyumba zenye simu zilijulikana na kukiwa na dharura mnagonga mlango hata usiku wa manane.

Binadamu ni wanyama wanao tegemeana na hupenda kushirikiana. Kadiri maendeleo yanavyoongezeka binadamu tunazidi kujitenga. Usishangae ukawaeza kusherehekea siku yako ya kuzaliwa ukiwa peke yako.

Huko tuendako itafikia wakati unafunga ndoa ukiwa na mashahidi wenu tu na baada ya hapo mnakwenda kupata chakula nyumbani au hotelini. Muda wa kualikana kwenye sherehe hautakuwepo.
Ndio mbele wanavyoishi.... Ndoa inahudhuriwa na watu kumi tu.......
 
Back
Top Bottom