Distant Relatives
JF-Expert Member
- Nov 21, 2020
- 415
- 731
Pia imepunguza ubakaji. Kuna tafiti niliona inasema wigo wa internet ukiongezeka kwa 10% ubakaji unapungua kwa 7%.Teknolojia imefanya mwanamke asithaminiwe tena kingono. Wanaume wanaona tupu za wanawake mitandaoni kwa hiyo hata ukikutana nayo mubashara abadan hamu imeshaisha.
Mbeleni giza lakini... Nini kitatokea endapo wanadamu wote tutaangamia?Teknolojia imeyaboresha sana maisha ya mwanadamu. Hii haimaanishi kuwa haina mapungufu.
Kweli maisha yamebadilika watu siku hizi hawana subira kwenye mawasiliano. Unakuta mchumba asipopokea simu tu basi mnaachana wakati zamani barua inakaa miezi hata miwili ndio upate jibu lini mtaonana.Maisha lazima yabadilike,
Kila zama na Kitabu chake.
Nitasoma kwa utulivu hilo andiko na hicho kitabu na nitakupa inputs zangu.Mbeleni giza lakini... Nini kitatokea endapo wanadamu wote tutaangamia?
Hahhaa kweli asee kukaa mezani kula kama familia hamna siku hizi kila mtu ana mda wake.Siku hizi hata kula pamoja nyumbani hakuna. Huyu kaenda kuangalia mpira, huyu anaCHAT jikoni mwingine anacheza GAME chumbani. Chakula kipo kwenye hotpot kikipoa mtu anapasha kwa MICROWAVE.
Kwa kweli mfumo wa maisha umebadilika sana, nakumbuka miaka ya nyuma sikukuu ya Wakristo basi tunafungasha mapilau kupeleka kwa majirani zetu waislamu lakini hivi sasa mambo yamekuwa kinyume kabisa. Kwa kweli tunapoenda itafika mahala tutakuwa hatusalimiani kabisa.
Kizazi cha sasa tumekuwa wabinafsi sana, tusio na upendo.
Siku hizi hata kula pamoja nyumbani hakuna. Huyu kaenda kuangalia mpira, huyu anaCHAT jikoni mwingine anacheza GAME chumbani. Chakula kipo kwenye hotpot kikipoa mtu anapasha kwa MICROWAVE.
Hata kuwafundisha watoto table manners hatuwezi baba anakula chakula akiwa kwenye sofa anaangalia Man United inacheza.
Tunachokitafuta tutakipata muda si mrefu! Tecnolojia itakuja kutuangamiza
Ndio mbele wanavyoishi.... Ndoa inahudhuriwa na watu kumi tu.......Maendeleo ya sayansi na tekinolojia yameua mahusiano ya kijamii. Leo hii kila mtu anatembea na simu. Akiwa anasubiri huduma iwe mahakamani au hospitali anaingia Instagram au Facebook. Hakuna muda wa kumsalimia aliyekaa pembeni yako.
Miaka ya nyuma ilikua ni kawaida kugonga mlango katika nyumba iliyo karibu na kuomba maji ya kunywa ukiwa na kiu. Siku hizi kugonga nyumba ya mtu kuomba maji au kuomba kutumia simu umepatwa na dharura ni jambo la ajabu. Enzi za simu za mezani nyumba zenye simu zilijulikana na kukiwa na dharura mnagonga mlango hata usiku wa manane.
Binadamu ni wanyama wanao tegemeana na hupenda kushirikiana. Kadiri maendeleo yanavyoongezeka binadamu tunazidi kujitenga. Usishangae ukawaeza kusherehekea siku yako ya kuzaliwa ukiwa peke yako.
Huko tuendako itafikia wakati unafunga ndoa ukiwa na mashahidi wenu tu na baada ya hapo mnakwenda kupata chakula nyumbani au hotelini. Muda wa kualikana kwenye sherehe hautakuwepo.