Maendeleo yanaendana na mahitaji ambayo pia huwafanya Wazungu na Wachina kuja Afrika

Maendeleo yanaendana na mahitaji ambayo pia huwafanya Wazungu na Wachina kuja Afrika

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2021
Posts
1,117
Reaction score
3,153
MAENDELEO YANAENDANA NA MAHITAJI,MAHITAJI HAYO NDIYO YANAFANYA WAZUNGU NA WACHINA WAJE AFRIKA.

Leo 19:30hrs 21/05/2021

Tangu 1st hadi sasa 4th industrial revolution, maendeleo ya ubunifu wa viwanda yamekuwa yakiendana na mahitaji maalum ya matumizi ya “Materials” kuzalisha mashine, mitambo,magari na vifaa n.k.; sambamba na mabadiliko ya matumizi ya “Energy” kwa ajili kuendesha mitambo au magari,kwa mfano, ubunifu wa kubadilisha chuma cha kawaida (“iron”) kuwa chuma cha pua (“steel”) iliwezesha kujenga reli (“railway”) na matumizi mengine.

4th industrial revolution ambayo tupo sasa inahitaji na itahitaji materials kwa ajili ya kutengeneza computers, smartphones, servo-motors, energy storage batteries na mashine/vifaa mbalimbali,Mali ghafi hitajika ni pamoja na nickel, lithium,graphite,vanadium, soda ash, copper,manganese. TANZANIA na majirani zetu (ANGOLA, DRC, BURUNDI, MOZAMBIQUE na ZAMBIA) TUNAZO ZOTE KWA WINGI,Ulaya hawana hata moja,watazipata wapi? Kwa namna gani? Wazungu watakuja tu... hilo halina mjadala kwa sababu it is a matter of survival of their economy.

Watatumia kila mbinu. Suala ni kwamba Watanzania na Waafrika kwa ujumla watawapokea na kuwapa masharti gani hao Wageni?? Ukoloni mambo leo unao ubunifu mkubwa.Wanaweza wakatumika Waafrika mara hii tena kama ilivyokuwa wakati wa kuchukuliwa watumwa na rasilimali za Afrika. Walikuja Wazungu wachache tu na hadaa zao wakafanikiwa,kizazi kipya kuweni macho,Wazungu na Wachina lazima watakuja tu,huu ni urithi wa Waafrika ambao tumepewa na Mwenyezi Mungu kwa makusudi kabisa ya kuitajirisha Afrika kila muda unapowadia, tayari tuna weledi lakini tusitumike kama Mkalimani Ramadani alivyotumiwa na "Carl Peter's mkono wa damu"kutafsiri vibaya kwa Chifu Mang'ungo wa Msovelo na hatimaye kuingia mkataba wa kilaghai.

-Msemakweli Chakubanga na
John Leon Simbakalia.
 
Kwa hiyo Africa ni sawa na Faru na pembe lake, swali litabaki tunaweza kuilinda pembe?.
 
Kwa hiyo Africa ni sawa na Faru na pembe lake, swali litabaki tunaweza kuilinda pembe?.
Mie naona kwa nchi zetu hizi za Afrika ni afadhali tu tubaki na faru, mradi pembe tutakuwa tumeuza na kufaidika na kuleta maendeleo kwenye nchi zetu.... manake kwa nchi zetu hizi,ukizing'ang'ania hizo pembe bado uwaitao 'mabeberu' wanaweza bado rudi kwa njia za uwani kwa wawindaji haramu watakao wauza kwa bei ya cheee kabisa......kushindana na jamaa hao inahitaji multi strategies na mbinu muafaka na na sio maneno pekee... Siku zote 'ukitaka kupata, vilevile ukubali angalau uliwe.....au nadanganya jamani....kazi iendelee.
 
Back
Top Bottom